Skip navigation.
Home kabah

27 Dua'a Ya Swalatul-Istikhara (Swala Ya Kutaka Muelekezo Au Kukata Shauri Katika Jambo)

(74)

Amesema Jaabir Bin Abdillah رضى الله عنه  “alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur’an.  Anasema صلى الله عليه وسلم   ‘Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِاْـمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ  (وَيُسَـمِّي  حاجته)  خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه)   فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ  لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه) فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ  وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ  حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِِـه .

“Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yaliyofichikana.   Ewe Mwenyezi Mungu  iwapo jambo hili kutokana na ujuzi wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali ) basi nakuomba uniwezeshe nilipate, na unifanyie wepesi, kisha  unibariki, na iwapo unajua kwamba  jambo hili ni shari kangu katika dini yangu namaisha yangu na mwisho wa  jambo langu (karibu na mbali) basi liepushe na mimi naminiepushe nalo, na  nipangie  jambo jengine lenye  kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo”

(Na hajuti mwenye kumtaka ushauri (muelekezo) Mwenyezi Mungu  na akawashauri waja waumini na akajidhatiti jambo lake)

(Amesema Mwenyezi Mungu  سبحانه وتعالى  kumwambia Mtume Wake صلى الله عليه وسلم  

 ) وَشَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ(  

(Na ushauriane nao katika mambo, na ukiazimia kufanya jambo, basi tegemea kwa Mwenyezi Mungu) Suratul Imraan: 159)