Skip navigation.
Home kabah

28 Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

Imepokelewa kutoka kwa  Anas  رضى الله عنه   amesema;  Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم   “Kukaa pamoja na watu wanaomtaja Mwenyezi Mungu  سبحانه وتعالى  kuanzia Swala ya Al-Fajiri  mpaka kuchomoza jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuacha huru watu wanne miongoni mwa wana wa Ismael na kukaa na watu wanaomtaja Mwenyezi Mungu  سبحانه وتعالى kuanzia baada ya Swala ya Al-Asiri mpaka kuchwa jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuwaacha huru watu wanne”

(75)

)اللّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْم...... (

Mwenye kusoma (Ayatul-Kursiy) pindi anapoamka atalindwa  kutokana na majini mpaka jioni, na atakaeisoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi.

(76)

 ) قُـلْ هُـوَ اللهُ أَحَـدٌ …..(      

) قُـلْ أَعـوذُ بِرَبِّ الفَلَـقِ…..(

) قُـلْ أَعـوذُ بِرَبِّ  النّـاسِ…..(  

(Mara tatu tatu)

(Mwenye kusisoma (sura hizi) mara tatu asubuhi na jioni zinamtosheleza na kila kitu.

(77)

 أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله وَالحَمدُ لله ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير ، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هَذا الْيَوْمِ  وَخَـيرَ ما بَعْـدَهُ   ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هَذا الْيَوْمِ  وَشَرِّ ما بَعْـدَهُ     ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر

“Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu , na sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu , hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Mwenyezi Mungu , hali yakuwa peke yake, hana mshirika.  Niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ewe  mola, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajilinda Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Ewe Mola, najilinda Kwako, kutokana  na uvivu, na ubaya wa uzee (uzee ubaya) Ewe mola najilinda Kwako kutokana na adhabu ya  moto na adhabu ya kaburi”

(Na ikiingia jioni useme)

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير ، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر .

(78)

اللّهُـمَّ بِكَ أَصْـبَحْنا وَبِكَ أَمْسَـينا ، وَبِكَ نَحْـيا وَبِكَ نَمـوتُ وَإِلَـيْكَ النِّـشور .

“Ewe Mwenyezi Mungu  kwa sababu yako tumeingia katika asubuhi, na kwa ajili yako tumeingia jioni, na kwa ajili yako ndio  tumekuwa hai, na kwa ajili yako tutakufa, na kwako tutafuliwa”

(Na ikifika jioni useme )

اللّهُـمَّ بِكَ أَمْسَـينا، وَبِكَ أَصْـبَحْنا، وَبِكَ نَحْـيا، وَبِكَ نَمـوتُ وَإِلَـيْكَ المَصـير

“Ewe Mwenyezi Mungu  kwa ajili yako tumefika jioni, na kwa ajili yako tumefika asubuhi, na kwa ajili yako tuko hai na kwa ajili yako tutakufa na ni kwako tu marejeo.

(79)

اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك ، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت ، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت ، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ  عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .

“Ewe Mwenyezi Mungu  Wewe ni Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja wako, nami niko juu ya  ahadi yako, na agano lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda kwako kutokana  na shari ya nilicho kifanya, nakiri  kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe”

(80)

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَصْبَـحْتُ أَُشْـهِدُك ، وَأُشْـهِدُ حَمَلَـةَ عَـرْشِـك ، وَمَلائِكَتِك ، وَجَمـيعَ خَلْـقِك ، أَنَّـكَ أَنْـتَ اللهُ لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَريكَ لَـك ، وَأَنَّ ُ مُحَمّـداً عَبْـدُكَ وَرَسـولُـك .(أربع مرات حينَ يصْبِح أوْ يمسي)

“Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nimefika asubuhi nakushuhudia na nina washuhudia wabeba wa arshi yako na malaika wako, na viumbe vyako vyote kwamba Wewe ndiye Mwenyezi Mungu  hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa peke yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wako na ni Mtume wako”

(Utasema hivi mara nne, asubuhi au jioni) 

Atakaye yasema haya asubuhi au jioni mara nne Mwenyezi Mungu  سبحانه وتعالى   atamuepusha na moto.

(81)

اللّهُـمَّ ما  أَصْبَـَحَ بي مِـنْ نِعْـمَةٍ أَو بِأَحَـدٍ مِـنْ خَلْـقِك ، فَمِـنْكَ وَحْـدَكَ لا شريكَ لَـك ، فَلَـكَ الْحَمْـدُ وَلَـكَ الشُّكْـر

“Ewe Mwenyezi Mungu  sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe chako chochote, na neema ila inatoka kwako hali ya kuwa peke yako huna mshirika wako, ni zako  sifa njema na nizako shukurani” 

Atakae yasema haya kila asubuhi basi atakuwa ametekeleza  shukurani ya siku nzima, na atakae yasema jioni atakuwa ametekeleza shukurani ya usiku mzima

(82)

اللّهُـمَّ عافِـني في بَدَنـي ، اللّهُـمَّ عافِـني في سَمْـعي ، اللّهُـمَّ  عافِـني في  بَصَـري ، لا إلهَ إلاّ اللّه أَنْـتَ . (ثلاثاً)

اللّهُـمَّ  إِنّـي أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكُـفر ، وَالفَـقْر ، وَأَعـوذُبِكَ مِنْ عَذابِ القَـبْر ، لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ . (ثلاثاً)

“Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya mwili wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya usikizi wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya uwoni wangu,hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe”

 (mara tatu )

“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe”  (mara tatu )

(83)

حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم

“Mwenyezi Mungu ananitosha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, kwake Yeye nimetegemea, na Yeye ni Mola wa Arshi Tukufu”

(mara saba asubuhi na jioni)

(84)

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ  وَأهْـلي وَمالـي ، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي ، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي ، وَمِن فَوْقـي ، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

“Ewe Mwenyezi Mungu  nakuomba msamaha na afya duniani na akhera.  Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na jamaa zangu, na mali yangu, Ewe Mwenyezi Mungu  nisitiri uchi wangu, na unitulize  khofu yangu, Ewe Mwenyezi Mungu  nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, najuu yangu, na najilinda kwa utukufu wako kwakutekwa chini yangu”

(85)

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيْبِ وَالشّـهادَةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه ، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت ، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ   نَفْسـي  وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه ، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى  نَفْسـي  سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم .

“Ewe Mwenyezi Mungu , Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyowazi, muumba wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu, na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki  ila Wewe, najilinda kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na shari ya shetani na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu”

(86)

بِسـمِ اللهِ الذي لا يَضُـرُّ مَعَ اسمِـهِ شَيءٌ في الأرْضِ وَلا في السّمـاءِ وَهـوَ السّمـيعُ العَلـيم   (ثلاثاً)

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu  ambae hakidhuru kwa jina lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, nae ni Msikivu na ni Mjuzi"

(mara tatu )

(87)

رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّـاً وَبِالإسْلامِ ديـناً وَبِمُحَـمَّدٍ  صََلى الله عليه وسلم  نَبِيّـاً . (ثلاثاً)

“Nimeridhika kuwa Mwenyezi Mungu ndie Mola wangu, na Uislamu ndio dini yangu, na Muhammad صََلى الله عليه وسلم   kuwa ni Mtume wangu”

(mara tatu)

(88)

يا حَـيُّ يا قَيّـومُ بِـرَحْمَـتِكِ أَسْتَـغـيث ، أَصْلِـحْ لي شَـأْنـي كُلَّـه ، وَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـين

“Ewe Uliyehai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu  yote, wala usiniachie  mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia) hata kwa muda (mdogo kama muda) wa kupepesa jicho”

(89)

أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم ، فَـتْحَهُ ، وَنَصْـرَهُ ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ ، وَهُـداهُ ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه .

“Tumeingia asubuhi  na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote, Ewe Mwenyezi Mungu   hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii”

(Na ikiingia jioni useme)

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة ، فَتْحَهـا ، وَنَصْـرَهـا ، وَنـورَهـا وَبَـرَكَتَـهـا ، وَهُـداهـا ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا .

“Tumeingia jioni  na imefika jioni na Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote, Ewe Mwenyezi Mungu   hakika mimi nakuomba kheri ya usiku huu,  ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu”

(90)

أَصْـبَحْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام ، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص ، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن .

“Tumeingia asubuhi na maumbile ya kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم   na mila (dini) ya baba yetu Ibrahim iliyo sawa hali yakuwa  musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu"

(Na ikiingia jioni useme)

أَمْسَيْنا  علـى فِطْـرَةِ الإسْلام ، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص ، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

“Tumeingia jioni na maumbile ya kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم   na mila (dini) ya baba yetu Ibrahim iliyo sawa hali yakuwa  musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu “

(91)

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ

“Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote nizake”

 (mara mia moja)

(92)

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake sifa njema zote na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza”

(mara kumi, au mara moja ukisikia uvivu)

(93)

Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Mwenye kusema inapoingia asubuhi

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu  peke yake hana mshirika wake, niwake Ufalme na nizake  sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza”

……….kwa siku mara mia, basi ana thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikwa thawabu mia  moja na atafutiwa madhambi mia moja, na atakuwa na kinga ya shetani kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake”

(94)

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه

“Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake, kwa hisabu ya viumbe vyake, na radhi yake, na uzito wa arshi yake, na wino wa maneno yake “

 (mara tatu kila asubuhi )

(95)

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً وَرِزْقـاً طَيِّـباً ، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً

“Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa”

(96)

أَسْتَغْفِرُ الَّلهَ وَ أَتُوبُ إِلَيْهِ

“Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu  na ninarejea Kwake”

(mara  mia kwa siku )

(97)

Alikuwa Mtume صلى الله عليه وسلم akisema asubhuhi  na jioni :

أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

“Najilinda na maneno ya Mwenyezi Mungu  yaliyotimia kutokana na shari aliyoiumba”

(mara tatu jioni)

Mwenye  kuisema jioni mara tatu hatodhuriwa na mdudu wa sumu (kama nyoka au kitumbo-nge) usiku huo .

(98)

اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ  وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه،  كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم . وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه،  كَمـا بارِكْتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم . إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد

“Ewe Mwenyezi Mungu  mrehemu Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowarehemu jamaa wa Ibrahim.  Na mbariki  Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowabariki jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe Umesifika na Umetukuka”

  …."Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shifaa (msamaha) siku ya kiama " 

 

 

Assalaam alaikum, Hivi

Assalaam alaikum,

Hivi vitabu hakuna nakala ya PDF

A.a,kila sifa njema ni za

A.a,kila sifa njema ni za allah s.w,ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Ndugu zangu wa alhidaya,wallahi mumetufungua macho yetu,masikio ,na nyoyo zetu,Mungu awajaze kheri hapa Duniani na Akhera Amin,nimepata mafunzo mengi sana ambayo nilikuwa siyajui na nimeilimika sana na naendelea kupa ilmu kutoka kwenu kwa Amri ya Allah,tangu nianze kuwa na nynyi,huwakumbuka kila niniposwali na nikawaombea Mungu sana Awadumishe na mafunzo pamoja na darsa zenu za kufahamika,Mungu awabariki nyote kwa jumla,Amin,w.s.