Skip navigation.
Home kabah

35 Dua'a Ukiwa Na Hamu Na Huzuni

(120)

اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ ابْنُ عَبْـدِكَ ابْنُ أَمَتِـكَ نَاصِيَتِي بِيَـدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤكَ أَسْأَلُـكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّـيْتَ بِهِ نَفْسَكَ أِوْ أَنْزَلْتَـهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْـتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِـكَ أَوِ اسْتَـأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْـبِ عِنْـدَكَ أَنْ تَجْـعَلَ القُرْآنَ رَبِيـعَ قَلْبِـي، وَنورَ صَـدْرِي وجَلَاءَ حُـزْنِي وذَهَابَ هَمِّـي

“Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi ni mtumwa wako, mtoto wa mtumwa wako, mtoto wa kijakazi chako, utosi wangu uko mikononi mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu yako, ni usawa kwangu kunihukumu kwako, nakuomba kwa kila jina ambalo ni Lako ulilojiita kwako mwenyewe au uliloliteremsha katika kitabu chako, au ulilomfundisha yoyote yule kati ya viumbe vyako, au ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijuwa) katika ilimu iliofichika kwako, nakuomba ujaaliye  (uifanye) Qur’ani kuwa ni raha na uchanuzi wa roho yangu na nuru ya kifua changu, na utatuzi wa  huzuni yangu, nasababu ya kuondoka majonzi yangu”

(121)

اللّهُـمَّ إِنِّي أَعْوذُ بِكَ مِنَ الهَـمِّ وَ الْحُـزْنِ، والعًجْـزِ والكَسَلِ والبُخْـلِ والجُـبْنِ، وضَلْـعِ الـدَّيْنِ وغَلَبَـةِ الرِّجال.

“Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni na kutoweza uvivu na ubakhili na uoga na uzito wa deni na kushindwa na watu”