36 Dua'a Ya Kupatwa Na Janga Au Balaa
(122)
لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ رَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم
“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu aliye Mtukufu Mpole, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu Mola wa Arshi tukufu, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu na Mola wa ardhi na Mola wa arshi tukufu" .
(123)
اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـوفَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت
“Ewe Mwenyezi Mungu rehema zako nataraji, usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, naunitengenezee mambo yangu yote, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe”
(124)
لاَ إِلَهَ إِلَّا أنْـت سُـبْحانَكَ إِنِّي كُنْـتُ مِنَ الظّـالِميـن
“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, kutakasika ni Kwako. Hakika mimi ni miongoni mwa waliodhumu nafsi zao”
(125)
اللهُ اللهُ رَبِّي لا أُشْـرِكُ بِهِ شَيْـئاً
“Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu , Mola wangu simshirikishi na kitu chochote kile"
- Login or register to post comments
- Email this page


