Skip navigation.
Home kabah

002 Aina Za Twahara

 

Maulamaa wanaigawanya Twahara ya kisheria katika vigawanyo viwili:
1- Twahara ya kihakika: Nayo ni Twahara ya kuondosha najisi. Hii inakuwa katika mwili, nguo na mahala.
 
2- Twahara ya kihukumu: Ni Twahara kutokana na hadathi, nayo  inahusiana na mwili. Aina hii ya Twahara ni sampuli tatu:
 
Twahara kubwa, nayo ni kuoga, Twahara ndogo, nayo ni kutawadha, na badala ya viwili hivyo vinaposhindikana, nayo ni kutayamamu.
 
KWANZA:
TWAHARA YA KIHAKIKA
Makusudio ya najisi:
Najisi  ni kinyume ya Twahara. Na najisi (kilichonajisika), ni jina la kitu chenye kuonekana kichafu kisheria. Ni lazima Muislamu ajiepusha nacho na akioshe kile kilichompata katika kitu hicho.