006 Je, Damu Inazingatiwa Kuwa Ni Katika Najisi?
Damu ina vigawanyo:
1- DAMU YA HEDHI:
Damu hii ni najisi kwa makubaliano ya Maulamaa. Dalili ya unajisi wake imekwisha elezewa nyuma.
2- DAMU YA MWANADAMU [1]
Ni damu iliyosababisha mahitalifiano juu ya hukumu yake. Lililo mashuhuri kwa watu wa madhehebu ya kifiqhi ni kwamba damu ni najisi, lakini wao hawana hoja. Isipokuwa damu imeharamishwa kwa matini ya Qur-aan katika neno
((قُل لاَّ أَجِدُ فِي مَا أُوْحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلاَّ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ ))
« Sema: Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu».[2]
Kwa hiyo, wao wamewajibisha unajisi wake kutokana na kuharamishwa kwake,
Ni wakati ambapo kundi la waliokuja baadaye akiwemo Ash-Shawkaany, Siddiyq Khaan, Al-Albaaniy, Ibnu ‛Uthaymiyn (Allaah Awarehemu) wameelekea kusema kuwa damu ni twahara kwa kutothibiti ijmaa kwa upande wao. Wao wametoa dalili vilevile kwa haya yafuatayo:
1- Asili ya vitu ni twahara mpaka iwepo dalili kuwa ni najisi. Na sisi "hatujui" kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru kuosha damu nyingine isiyo ya hedhi ingawa mtu hupatwa mara nyingi na majeraha na mfano wake. Na lau
2- Ni kwamba Waislamu bado wanaswali wakiwa na majeraha
- Amesema Al-Hasan: "Waislamu bado wanaswali wakiwa na majeraha
Na katika kisa cha Swahaba Muanswaar aliyekuwa amesimama usiku akiswali. Mshirikina alimpiga mshale, akauweka, kisha akaunyofoa, mpaka akampiga mishale mitatu. Kisha alirukuu, akasujudu na akaendelea na Swalah yake na huku akivuja damu. [4]
- Al-Albaaniy [5] (Allaah Amrehemu) amesema: "Nayo iko katika hukumu ya Hadiyth Marfuu, kwa vile kwa kawaida haiyumkiniki kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) asilijue
- Na katika kisa cha kuuawa ‘Umar bin Al-Khatw-twaab (Allaah Amridhie): "Umar aliswali, na huku jeraha
3- Ni kwa Hadiyth ya 'Aaishah katika kisa cha kufa kwa Sa'ad bin Mu’adh. Alisema: "Wakati Sa'ad bin Mu’adh alipojeruhiwa siku ya Khandaq, mtu mmoja alimpiga mshale wa kwenye mshipa wa damu mkononi. Mtume alimpigia hema msikitini ili amtazame kwa karibu. Na akiwa katika hali hiyo, usiku mmoja ghafla jeraha
Ninasema (Abuu Maalik): "Na wala haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru maji yamwagiwe juu yake na hasa kwa vile yuko msikitini
4- Kwamba Ibnu Rushdi wakati alipotaja hitilafu za Maulamaa kwa upande wa damu ya samaki, alieleza kwamba sababu ya kuhitalifiana kwao, ni kuhitilafiana kwao katika maiti yake. Basi mwenye kuifanya maiti yake inaingia chini ya ujumuishi wa kuharamishwa, ataifanya damu yake hivyo hivyo. Na mwenye kuitoa maiti yake, ataitoa damu yake kwa kupimia maiti yake.
Na tunasema: "Wao wanasema kuwa maiti ya mwanadamu ni twahara, na kwa hivyo damu yake vilevile (ni twahara) kwa mujibu wa kanuni
Na kwa ajili hiyo, Ibnu Rushdi alisema baada yake: "Na matini bila shaka imeonyesha juu ya unajisi wa damu ya hedhi, na isiyokuwa hiyo, basi iko katika uasili uliokubaliwa na wenye kuzozana, nayo ni twahara. Na haitoki humo ila kwa matini ya kusimamishia hoja…".
Na ikiwa itasemwa: "Je, haipimiwi kwa damu ya hedhi, na damu ya hedhi ni najisi?
Tunasema: "Hiki ni kipimo pamoja na tofauti:
- Kwani damu ya hedhi ni damu ya maumbile ya asili kwa wanawake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((ان هذا شيئ كتبه الله على بنات آدم))
((Hakika hiki ni kitu ambacho Mwenyezi Mungu Amekiweka kwa mabinti wa Aadam (wanawake)) [8]
Na akasema katika istihaadha:
((انه دم عرق))
((Hakika hiyo ni damu ya mshipa (asili)) [9] Kisha hakika damu ya hedhi ni damu nzito iliyovunda na yenye harufu mbaya. Imefanana na mkojo na kinyesi, si damu yenye kutoka katika zisizo njia mbili.
3- DAMU YA MNYAMA MWENYE KULIWA
Mjadala kuhusu damu hii, ni
Kusema kuwa ni twahara kunaungwa mkono vilevile na:
Yaliyoelezewa na Ibnu Masoud, amesema: "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali mbele ya Ka’abah, na ilhali Abuu Jahli na marafiki zake wamekaa. Pale walipoambiana: Ni yupi kati yenu atakayewaendea ngamia wa akina fulani, akakusudia taka zake, damu zake, na miji yake (wombs), kisha akamsubiri mpaka anaposujudu, halafu akamwekea mabegani mwake? Basi mwovu wao akachomoka haraka, na aliposujudu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), aliyaweka kati ya mabega yake, na Mtume Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam alitulia tuli katika sijdah, na wao wakacheka.[10].
Na lau
Na imethibiti kwa njia sahihi kwamba Ibnu Mas’uud aliswali nailhali katika tumbo
Na ingawa tukiona pokezi hili "athar" linaweza kufanyiwa mvutano katika kutolea ushahidi juu ya utwahara wa damu ya mnyama, kwa vile Ibnu Mas’uud hakuwa akiona kwamba utwahara wa mwili na nguo ni sharti ya kusihi Swalah, bali anaona kuwa ni jambo linalopendeza (mustahab).
Ninasema (Abuu Maalik): Lau kama imethibiti kwa ijmaa kwamba damu ni najisi, basi hatutaziangalia dalili za waliofuatia baadaye. Na
Ibnu Al-Qayyim katika "Ighaathat Allahafaan" (1/420) amesema:
Ahmad aliulizwa: "Je, damu na usaha kwako ni sawasawa"? Akasema: "Hapana, watu hawakuhitilafiana kuhusu damu".
Na alisema mara moja: "Usaha kwangu ni afadhali kuliko damu…".
Na imenukuliwa toka kwa Ibnu Hazm katika "Maraatib Al-Ijmaa": "Kukubaliana Maulamaa juu ya unajisi wa damu".
Vile vile Al-Haafidh katika "Al-Fat-h" (22/420) amekunukuu kukubaliana huko.
Na Ibnu Abdul-Barri katika "At-Tamhiyd" (22/230) anasema:
"Na hukumu ya kila damu ni kama damu ya hedhi, isipokuwa damu kidogo husamehewa kwa vile Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameweka sharti ya unajisi wa damu kuwa iwe ni yenye kuchuruzika, na hapo inakuwa ni uchafu, na uchafu ni najisi. Na hii ni ijmaa ya Waislamu kwamba damu yenye kuchuruzika ni uchafu na najisi..".
Na Ibnu Al-Araby katika "Ahkaam Al-Qur-aan" (1/79) anasema:
"Maulamaa wamekubaliana kwamba damu ni haramu na ni najisi kwa kinacholiwa na kisichopatiwa manufaa. Na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameiainisha hapa kwa kuifanya ni yoyote ile (mutwlaq), na katika
Na An-Nawawy katika Al-Majmu’u (2/576) amesema:
"Na dalili juu ya unajisi wa damu zinatiliana nguvu zenyewe kwa zenyewe, na mimi sijui kama kuna hitilafu yoyote toka kwa Muislamu yeyote ila tu yale aliyoyaelezea mtunzi wa Al-Haawiy toka kwa baadhi ya Maulamaa wa tawhiyd. Amesema kuwa ni twahara, lakini Maulamaa wa tawhidi maneno
Ninasema (Abuu Maalik): Ninalolipa nguvu na uzito ni kuwa damu ni najisi kwa kuthibiti ijmaa mpaka inukuliwe toka kwa Imaam mwingine atakayempiku Imaam Ahmad – (Allaah Amrehemu) – kwa kusema kuwa damu ni twahara. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
[1] Tafsiri ya Al-Qurtuby (2/ 221), Al-Majmuu (2/511), Al-Muhalla (1/102), Al-Kaafy (1/110), Bidaayatul Mujtahid, As-Saylul Jarraar (1/31), Ash-Sharhul Mumti'i (1/376), As-Silsilatu Asw-Swahiyhah na Tamaamu Al-Minnah (uk.50).
[2]
[3] Isnadi yake ni sahihi. Imepokelewa na Al-Bukhaariy ikiwa "muallaq" (1/336). Na Ibnu Abu Shaybah ameiunganisha kwa sanad sahihi
[4] Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy ameifanya "mu’allaq" (1/336), na Ahmad na wengineo wameiunganisha, nayo ni sahihi.
[5] Tamaam Al-Minnah (51,52)
[6] Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Maalik (82), na amepokea toka kwake Al-Bayhaqiy (1/357) na wengineo kwa sanad sahihi.
[7] Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud (3100) kwa ufupi, na At-Twabaraaniy katika (Al-Kabiyr) (6/7).
[8] Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy (294), na Muslim (1211).
[9] Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy (327), na Muslim (333).
[10] Hadiyth Sahihi: Al-Bukhaariy (240) na Muslim (1794).
[11] Isnadi yake ni sahihi: Muswannaf Abdur-Raaziq (1/25), na Ibnu Abuu Shaybah (1/392).
- Login or register to post comments
- Email this page
