Khomeini Ndani Ya Darubini - 4 - Shutuma Zake Za Ukafiri Kwa Abu Bakr Na 'Umar Na Maswahaba

 

 

Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini

 

Toleo la Pili

 

 

Kama walivyo Mazindiyq wengine (ndivyo alivyo Khomeini), ambao wanaegemeza uovu na chuki dhidi ya Uislamu na watu wake, ambao wanampiga vita Mtume wa Allaah na Maswahaba zake, na ambao wanajificha chini ya udhuru wa uongo wa mapenzi ya Ahlul Bayt, Khomeini anasema:

“Hatujadili kwa wakati huu, na Mashaykh wawili (Abu Bakr na 'Umar), na Mashaykh wawili wala jeuri walizotenda dhidi ya Qur-aan, wakaharibu (kwa fujo) pamoja na Maswahaba wa Allaah wakatangaza vitu ruhusa na visivyoruhusiwa kwa makubaliano yao wenyewe wakatenda dhulma dhidi ya Faatwimah, binti halali wa Mtume na watoto wake (Faatwimah). Lakini tunataka kuonesha ujinga wao wa amri za Allaah na dini. Watu kama hao wajinga (na) wapuuzi, madhalimu na wakorofi hawakustahihi kuingia ofisi za Kiimamu, wala kuingizwa miongoni mwa watu wenye madaraka.1

Muongo anazidi kueleza:

“Ni jambo linaloeleweka kwa yote yaliyotangulia kwamba uovu wa Mashaykh wawili dhidi ya Qur-aan haukuwa na muhimu kwa Waislamu. Hayo ni kwa sababu (Waislamu) ama walikuwa miongoni mwa Mashaykh wawili na kushirikiana nao au dhidi yao, lakini hawakujaribu kusema kitu kwa wale waliomtendea Mtume wa Allaah na binti yake namna walivyofanya. Hata kama mmoja wa wapinzani atahitaji kusema kitu, maneno yake yatapita bila ya kufanyiwa kazi hata kama mambo hayo yametajwa ndani ya Qur-aan. (Hao ni) Wale ambao hawakujizuilia njiani mwao, wala kujiuzulu kwenye ofisi zao.2

Khomeini khabithi anamueleza al-Faruuq ‘Umar, Allaah Awe Radhi naye dhidi ya adui zake, anasema:

“Matendo ya ‘Umar yametoa dalili ya kutoamini mafundisho ya imani yasiyopatikana na Qur-aan na uovu wa aya zilizotajwa kwenye Qur-aan.3

Hakuna shaka yoyote kwamba madai haya ya Khomeini yanaonesha ukafiri na kurtadi, na kutoongoka kwa njia ya Waumini kwa sababu zilizo nyingi:

Kuwapiga vita Mashaykh wawili (Abu Bakr na ‘Umar), na kuwatuhumu wao kwa kutoamini na kurtadi, na kuwasingizia wao kwa uovu wa Qur-aan kwa makusudi na kwa ujinga, na kuwatuhumu kwao kwa ujinga na uhaini; kwanza, ni kuyatukana maneno ya Bwana wa Ulimwengu, Subhaanah, Ambaye Amewasifia wao, na kuwachagua kuwa ni Washirika wa Mtume Wake, Mtakatifu wa viumbe vyote, na Akawatofautisha wao kwa muongozo (sahihi) wale ambao wamepigana mtindo mmoja bega kwa bega na Mtume wake kwenye vita vyote. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alioa binti zao, na amewaeleza vyema wao kuwa ni bora wa Maswahaba wengine.

Amewabashiria kuingia kwao Peponi, na wamefurahia Ridhaa ya Allaah. Ummah wote wa Waislamu umethibitisha kwa wema isipokuwa waliortadi na wazushi ambao wamepinga makubaliano ya Ummah. Allaah Mtukufu Anasema:

{{Kama hamtamnusuru (Mtume), basi Allaah alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru, alipokuwa (mmoja tu na mwenziwe) wa pili wake, (peke yao) walipokuwa wote wawili katika pango.}} [9:40]

Huu ni ushahidi kutoka kwa Allaah unaomkubali Abu Bakr al-Siddiq, Allaah Awe Radhi naye, ambaye alikuwa na Mtume pale wote wawili walipojificha kwenye pango walipokimbilia Madiynah, mazingira yaliyokuwa mazito kabisa na hakupatapo Mtume kuyapata.

Kumpiga vita Abu Bakr kuna maana ya kurtadi maneno ya Allaah:

{{Na amchaye Allaah ataepushwa nao. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. Na hali ya kuwa hakuna yoyote aliyomfanyia ihsani ili awe anamlipa.}} [92: 17, 18, 19]

Wafasiri kwa pamoja wanakubaliana kwamba aya hizi zinamuelezea Abu Bakr as-Swiddiyq ambaye alikuwa akiwanunua watumwa kwa pesa zake na (kisha) kuwaachia huru, akitafuta Radhi za Allaah. Kumpiga vita inamaanisha kumpinga Allaah, Utukufu ni Wake Muweza, kwa maneno ya wazi, kwa sababu Yeye Amemchagua kuwa ni mtu wa mwanzo kuingia kwenye Uislamu, na makundi ya watu yakaongozwa (kuingia kwenye Uislamu) na yeye katika enzi za mwanzo za Uislamu. Allaah Amemchagua kuwa mshirika wa Mtume Wake kipindi chote cha maisha yake, kabla na baada ya Utume. Alipofariki, mwili wake ulilazwa pembezoni mwa mwili wa Mtume wa Allaah na ‘Umar, ya kwamba ushirika wao uendelezwe mpaka Siku ya Mwisho.

Kumpiga vita as-Swiddiyq kunalazimisha kumpinga Mtume wa Allaah Aliyemchagua kuwa ni mshirika wake kipindi chote cha maisha yake. Pale Mtume wa Allaah alipoulizwa. “Ni nani miongoni mwa watu ni mpenzi wako?” akasema “Aaishah” Kisha akaulizwa “Na katika wanaume?” Akajibu “Baba yake” (Al-Bukhaariy na Muslim) Pia alisema: “Kama itanibidi nichukue miongoni mwa watu wa ardhini rafiki, nitamchukua Abu Bark, lakini undugu wa Uislamu na mapenzi yake ni bora.”

Inakubalika na wote kwamba yeyote anayempiga vita as-Swiddiyq amepingana na Allaah Mtukufu na Mtume wa Allaah, aliyemuoa binti yake na kuishi naye kwa maisha yake yote yaliyobaki. Hivyo, kama as-Swiddiyq alikuwa mjinga, kama Khomeini (muongo mkuu na asiye na akili anavyodai), basi hili (shtaka) linaelekezwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa sababu ameshindwa kuwafunza watu wake kipindi chote cha kushirikiana nao, na kama as-Swiddiyq alikuwa ni haini asiye muadilifu, kama waongo wanavyodai, basi (hao) ni Maswahaba zake, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye atakayepelekewa lawama.

Mmoja anaweza kumuuliza Khomeini na Mazindiyq wote kama yeye “Jee Mtume wa Allaah alikuwa akimtambua Abu Bakr as-Swiddiyq kiimani au sio?” Kama jibu litakuwa ‘sio’ basi wamejitangaza wenyewe kuwa hawana Imani na ni Wartadi, kwasababu watakuwa wanamtuhumu kwa ujinga na hukumu mbaya kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kushindwa kuzitambua sifa za mshirika wake wa maisha. Na kama watasema: ‘Ndiyo’, akimtambua kwamba Abu Bark alikuwa mjinga na dhalimu lakini alibaki kimya, badala yake akimsifu, akafanya ndoa na mtoto wake, akafariki ilhali kichwa chake kipo kwenye kifua chake (‘Aaishah), na akamteua kuongoza Swalah ya Jama’ah. Kama watakubaliana na yote haya basi wanajitangazia wenyewe kukosa Imani, kwa sababu haiyumkiniki kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akubaliane na uongo na makosa ya tabia, wala haimpasi kufanya hivyo. Lolote kati ya majibu hayo mawili yatakayotolewa, itaonesha ukosefu wa Imani.

Pia tunawauliza hawa wakaidi wa Imani sahihi: Alikuwa wapi Allaah Mtukufu pale kwa pamoja as-Swiddiyq na al-Faaruuq wakimuendea kinyume Mtume Wake, kama munavyodai, wakiwa na nia ya kupata madaraka baada yake? Kwanini Allaah hakushusha aya za Qur-aan kuwafichua wao wakati Allaah Alipokuwa Akishusha maneno kwa mnasaba wa mambo ambayo si mazito kama uzito wao? Iweje Allaah Ashindwe kuleta habari za kuwafichua uovu wao kama kweli walikuwa waovu kama wanavyodaia Khomeini na Mashia wenzake wapotofu?

Wakati mmoja Allaah Aliteremsha aya zinazomfichua mnafiki ambaye alisaliti moja kati ya vita (vilivyopiganwa na Mtume) na mwengine aliyemtukana Mtume kwa neno. Wengine walifichuliwa kwa kujenga msikiti kama ni kitu kizuri kwa waumini na hali ulikuwa ni wa shari. Jee ni vipi iwezekane (wewe) Khomeini, Allaah hakuwafichua wale waliomfanyia hila Mtume Wake kama mnavyoendelea kutuhumu, kuipinga Dini Yake, na kuunyanyasa ukoo wa Mtume Wake? Kama mnasema ya kwamba Allaah Alikuwa Akijua yote haya lakini Hakuwafichua, bila shaka mtakuwa mnajikubalisha dhidi yenu wenyewe kwa kurtadi kwa kumpinga Allaah Asiye na kasoro kwa kutomtahadharisha Mtume wake dhidi yao na hivyo kukubaliana na kosa na uongo. Yuko mbali na madai yenu. Na kama mtasema ya kwamba Allaah Hakushusha maneno kuwafichua wao, tutadai kwenu nyinyi kutuletea mbele yetu ushahidhi wenu. Tunaendelea zaidi kuwauliza kwanini Mtume hakuweka wazi maneno hayo au angalau kuwapa hadhari Maswahaba wake na Ummah wake dhidi ya Mashaykh wawili; Abu Bakr na ‘Umar? Na kwanini alificha ukweli kuhusu wao maishani kote?

Mtambue nyinyi waasi na wartadi, kwamba hamumpigi vita Abu Bakr na ‘Umar, bali Mtume wa Allaah. Hakika mnampiga vita Allaah Mtukufu Ambaye Yupo juu ya mbingu zake saba, na kuupiga vita ukoo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao nyinyi mnadai walikuwa ni wasaidizi wa mipango. ‘Aliy alikuwa wapi pale Kitabu cha Allaah kikiharibiwa, na pale Maswahaba walipochukua kwa nguvu? Kwanini hakuzungumzia hilo? Kwanini yeye alikuwa ni msaidizi mkuu na mshauri wa Abu Bakr na ‘Umar? Na walikuwa wapi watu wake wengine wa Mtume kipindi kilichotuhumiwa ni cha hatari?

Mnadai mara kwa mara kwamba Mashaykh wawili wamewapokonya urithi ‘Aliy na Faatwimah kutoka kwa mali ya Mtume, kwamba Faatwimah alishtaki dhidi ya as-Swiddiyq kuhusiana na mada hii, na kwamba ‘Aliy na al-‘Abbaas walijadiliana na Mashaykh (hao) wote, wakidai haki zao za urithi. Tunasema, hili lilitokea, lakini kiwango cha madai dhidi ya Mashaykh wawili, ya (kuwatuhumu) kubadilisha Dini ya Allaah, na kuchukua ukhalifa kwa nguvu, na vita vyenye (kuhitaji) kutiliwa mkazo kuliko mambo yapitayo ya kidunia (kwenye) suala la urithi. Jee ‘Aliy, Faatwimah na al-‘Abbaas wanajali zaidi kuhusu kipande cha ardhi kuliko Dini ya Allaah na uongozi wa Ummah wa Kiislamu? Jee walishtaki kwa Mashaykh wawili kuhusiana na urithi na kukataa shitaka juu ya kubadili Dini ya Allaah na kubadilisha Kitabu Chake? Jee walificha hamasa zao pale ilipokuja kuhusu madai ya haki zao na kuikosa pindi walipodai haki za Allaah? Hili ni tusi kubwa mlilolitoa dhidi ya ukoo wa Mtume. Walikuwa wapi maelfu ya Waislamu pale Dini ya Allaah ilipobadilishwa? Jee walikuwa hao Waislamu waliojitolea mali zao na maisha yao kwa ajili ya kutafuta radhi za Allaah wafedhuli wakubwa (kuliko) kusahihisha makosa? Ni wao ambao Allaah Amewasifia na kuwafanya taifa bora lililopata kutokea kwa wanaadamu. Bila ya shaka yoyote, mnadai kwamba wote walirudi kutoka kwenye Uislamu kwenda kwenye kufru isipokuwa watatu au watano kati yao.

Unageuka kutoka kwenye Uislamu kwenda kufru pale tu ulipotuhumu ujinga kwa Allaah, na kushutumu kwamba Yeye Amekubali dhulma na jeuri, kuwapatia bure wasioamini kucheza uharibifu na Dini Yake, Yuko mbali na yale munayomsingizia Kwake.

Allaah Ameahidi kukilinda Kitabu Chake, Anasema:

{{Hakika Sisi ndio Tulioteremsha ukumbusho huu (hii Qur-aan); na hakika Sisi ndio Tutakayoyalinda.}} [15: 9]

Lakini bila ya shaka yoyote wewe ni murtadi kwa kupinga kwamba Allaah Ametimiza ahadi Yake, kwamba Yeye Hakuleta kwa Mtume Wake na taifa lake baada yake dini, Abu Bakr na Umar hakutoa mali iliyoachwa na Mtume kwa warithi wake kwa ile sababu ya kwamba Mtume (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielekeza “Sisi Mitume haturithiwi: Mali yetu tunayoiacha nyuma inagaiwa sadaka...”

ukawasifu watu waovu, kuwafanya marafiki. Mliingia kwenye kurtadi mlipodai kwamba Allaah Alichagua kwa Mtume wake wapenzi wanafiki, waongo na wasaliti. Mliingia kwenye ukafiri pale mlipomshutumu Mtume wa Allaah (kutowapa) dharau kwa Mashaykh wawili. Hamkumuamini Allaah pale mliposhtaki kwamba Mtume wa Allaah alitoa mabinti wa wanafiki na wasioamini, na mlipodai kwamba alikaa nao wote ‘Aaishah na Hafswah kama ni wake zake akielewa fika kuwa sio wenye kuamini. Ulirudi kwenye kutokuwa na imani pale ulipotoa uongo kwa Allaah, Mtakatifu ni Yeye Muweza, kwa kuusifu Ummah wa Muhammad kwenye Kitabu Chake:

{{Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (pamoja), wakiitafuta fadhila za Allaah na radhi (Zake). Alama zao zi katika nyuso zao, kwa taathira, (athari) ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili (umetajwa hivi); Kuwa (wao) ni kama mmea uliotoa matawi yake; kisha (matawi hayo) yakautia nguvu, ukawa mnene ukasimama sawasawa juu ya kigogo chake, ukawafurahisha walioupanda; ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao. Allaah Amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.}} [48: 29]

Utaniwia radhi, hakika hukurudi kwenye ukafiri, kwasababu (tokea mwanzo) hukuwa na imani wala hukupata kuingia kwenye Uislamu, wala hakupata kuamini Kitabu cha Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Madai yako si kitu ila unapiga chenga na kusema uongo na madai yako ya kuwa pamoja na ukoo wa Mtume ni uongo, kwasababu wewe kwa kweli ni adui mkuu wa ukoo. Kila muongo mbaya mno na mwenye kwenda kombo, umedai kwamba alikuwa ni miongoni mwa watu wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Iwezekane hao wenye ndimi chafu kuwa ni watu bora na jamaa kwa ukoo wa Mtume?

Tambua, kuwa Allaah Anakuelewa na Ameutawala ukoo wa Mtume bila ya tuhuma zako mbovu, na mbali sana kutokana na uongo wako, na Anawalinda kutokana na njama zako.

Kwa ufupi, kwa kuwaendea kinyume Mashaykh wawili, Khomeini amemuendea sivyo Allaah, Mtume Wake na Ukoo wake safi, na pia Ummah wake Mtukufu ambao Allaah Ameusifu, Akaegemeza mashahidi dhidi ya wa mwanzo na taifa la mwisho. Akisema:

{{Na vivyo hivyo kumekufanyeni umati bora (kamaQiblah chenu tulivyokifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu.}} [2: 143]

Sifa ni zake Allaah Ambaye Amebashiria kwa uzuri, wema na ubora wa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa imani thabiti ya Abu Bakr as-Swiddiyq na ‘Umar al-Faaruuq, na kwa kuwabashiria kwao Pepo. Laana za Allaah ziwe juu ya kila mkorofi na mchongezi mwenye chuki ambaye yupo dhidi ya Ummah mtukufu na muongofu.

 

Inaendelea in shaa Allaah...

1 Khomeini, Kashf al-Asrar, pp. 107,

2 ibid, pp. 118

3 ibid pp. 117

 

Khomeini Ndani Ya Darubini - 1 Fatwa Za Wanazuoni Wa Kiislamu Kuhusiana Na Khomeini

 

Khomeini Ndani Ya Darubini - 2 Hoja Yake Kwamba Maimaamu Wa Shia Ni Bora Kuliko Malaika Wote Na Mitume

 

Khomeini Ndani Ya Darubini - 3 Masingizio Ya Khomeini Kwa Mtume Wa Allaah

 

Khomeini Ndani Ya Darubini - 5 Kikao Cha Khomeini Na Kundi Lake Kuhusiana Na Mtume Mtukufu

 

 

Share