Skip navigation.
Home kabah

Ujumbe Wa Iysa alayhis-salaam Wa Kweli رســــالة عيسى الصحيحة

 

Na Dkt. Abu Ameenah Bilaal Philips

Kimefasiriwa na Muhammad Al-Ma'aawy

 

UTANGULIZI

 

Yesu Kristo anawakilisha kiungo muhimu baina ya Dini mbili zenye wafuasi wengi zaidi duniani hivi leo, Ukristo na Uislamu. somo lifuatalo kuhusu ujumbe wa Yesu na yeye binafsi imetegemea kiungo hiko. Inatarajiwa kuwa kwa somo hili, Waislamu na Wakristo wataelewa zaidi umuhimu wa Yesu na risala (ujumbe) yake.

 

Hata hivyo, kw asisi kuutambua barabara ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo, nukta ya rai isiyopendelea ni lazima idumishwe kwa mwelekeo wa utafiti wetu wote. Tusipatie jazba zetu fursa kufunika uoni wetu na hivyo kutupofusha kutokana na ukweli. Ni lazima tutazame nukta na mambo yote kimantiki na tutenge kando ukweli kutokana na uwongo – kwa uwezo wa Mwenza Mwenye nguvu.

 

Tunapotazama Dini kadhaa za uwongo na itikadi potofu katika uliwengu na hamasa za wafuasi wao wanavyozishikilia itikadi hizo, inaonekana wazi kabisa kuwa watu hawa hawawezi kuupata ukweli kwa sababu ya misimamo yao ya upofu kwa itikadi zao hizo. Ufuataji wao kwa kung’ang’ania vilivyo hautegemei utambuzi wa kiakili wa mafundisho, lakini kwa ushawishi wa nguvu wa kitamaduni na hamasa. Hiyo ni kuwa wao wamelelewa katika familia fulani au jamii, wanashikilia barabara itikadi za jamii hiyo, wakiamini kuwa wameunga mkono ukweli.

 

Njia ya pekee tunayoweza kupata ukweli kuhusu jambo lolote ni kulifuatilia kwa mpango na kimantiki. Mwanzo, tunapima hoja na dalili na kisha tunahukumu kwa akili aliyotunuku Mwenyezi Mungu. katika ulimwengu wa mada, kimsingi ni akili inayowatofautisha wanaadamu kutokana na hayawani, ambao wanafanya amali kwa ilhamu. Baada kutambua ukweli bila upendeleo, ni lazima sisi tujishikilize kwa hisia na hamasa kubwa. Ndio, ipo nafasi kwa jazba ya msimamo lakini jazba hiyo ni lazima ije baada ya ufahamu wa kiakili wa mambo. Jazba ya msimamo ni muhimu, kwa sababu ni dalili ya ufahamu wa kweli. Pale mtu anapoelewa barabara na kwa ukamilifu uhakika wa jambo, hapo anakuwa amejitayarisha kiakili na kiroho kwa juhudi na nguvu kuunga mkono uhakika huo.

 

Ni kwa rai ya nukta hii ya kiakili na kiroho ndio mada ya ujumbe wa Yesu na uhusiano wake na wale wanaotaka kumfuata Mwenyezi Mungu imechambuliwa vilivyo katika kurasa zifuatazo.

 

Dkt. Bilal Philips

Saudi Arabia, 1989