Wasiya Wa Kisheria Wa Nyumbani
((وَاتَّقُواْ يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللّهِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لاَ يُظْلَمُونَ))
((Ogopeni Siku Ambayo Mutarudishwa Kwa Allaah Kisha Kila Nafsi Italipa Kila Lile Ililochuma Na Wao Hawatadhulumiwa)) (Al-Baqarah: 281)
Utangulizi
Shukrani zote Anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu wote. Swalah na amani ziwe juu ya aliyetumwa awe ni Rehma kwa ulimwengu wote Mtume Muhammad Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Ahli zake, Swahaba na wale ambao wamefuata Sunnah zake mpaka siku ya mwisho.
Nimefikiri kuhusu mauti mara kadhaa na nimejaribu sana kule kukutana kwangu na Allaah سبحانه وتعالى kuwe ni kwenye kumridhisha na kuwe mbali na uzushi wa zama hizi. Nami nina yakini kabisa kuwa kila bid’ah (uzushi) ni upotevu na kila upotevu malipo yake ni moto. Na pia kila uzushi ni upotevu, japokuwa watu watayaona ni mazuri na mema.
Nimesoma mengi kuhusu janaza na wasiya wa kisheria lakini sijapata kilicho kamilika wala bora kuliko kitabu “Hukumu ya Janaza na Uzushi wake” cha Shaykh Muhammad Naaswirud Diyn Al-Albaaniy Allaah سبحانه وتعالى Amrehemu.
Ewe ndugu yangu… Tukumbuke mauti daima… Mpaka tufanye amali ya baada ya mauti. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema:
((أكثروا من ذكر هادم اللذات..)
((Zidisheni katika kukumbuka mauti)) [At-Tirmidhiy, Ahmad na Ibn Maajah]
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesisitiza kuhusu kuacha wasiya ulioandikwa, akasema:
((ما حق إمرئ مسلم يبيت ليلتين وله شئ يوصى فيه إلا ووصيته مكتوبة عند رأسه)) البخارى ومسلم
((Ni haki gani ya Muislamu anayekaa masiku mawili na ana kitu cha kukitolea wasiya ila na wasiya wake umeandikwa chini ya kichwa chake))
[Al-(Bukhaariy na Muslim]
Wasia Wangu Wa Kijumla
Watu wa nyumbani kwangu watukufu, nawausia:
1) Mpwekesheni Mwenyeezi Mungu Allaah سبحانه وتعالى Pekee (At-Tawhiyd) na mujihadhari na kuingia katika kumshirikisha. Asema Allaah سبحانه وتعالى
((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء .... ))
((Hakika Allaah Hasamehe dhambi za kushirikishwa, na Anasamehe dhambi lisilokuwa hilo kwa Amtakaye…)) [An-Nisaa 4: 48, 116]
2) Muogopeni na kumpenda Allaah سبحانه وتعالى na mufuate sheria zake kwa siri na dhahiri. Hifadhini nguzo za Uislamu, amrisheni mema na mkatazane mabaya, ungeni ujamaa na kizazi na mushikamane na kila kitukufu na twa’a ya Allaah سبحانه وتعالى Aliyetukuka na fuateni Sunnah za Mtume wake صلى الله عليه وآله وسلم
3) Nawausia mfanye taubah ya kweli kweli na sawa kutokana na kila maovu na maasi na ombeni maghfira (msamaha), mkumbukeni na mumtaje Allaah سبحانه وتعالى kwa wingi na muisome Qur-aan kila mchana na usiku.
4) Nawausia muwe na subira na kuridhika wakati wa msiba mara ya kwanza na museme:
إنا لله وإنا إ ليه راجعون اللهم أجرنا فى مصيبتنا واخلف لنا خيرا منها
“Bila shaka tuna toka kwa Allaah سبحانه وتعالى na Kwake ndio marudio. Ewe Allaah Tupe ujira katika msiba wetu huu na Utubadilishiye lililo bora zaidi kuliko huo msiba.”
5) Msinitangaze katika magazeti wala vipaza sauti bali wasilianeni na jamaa zangu na marafiki ili wanioshe na kuniswalia….Na kunivisha sanda na kuniombea Du‘aa pamoja na kuniombea msamaha (maghfira).
6) Msikae sehemu ya msiba.…wala katika hema au nyumba za sherehe au nyumba za kawaida. Haikuonekana kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala Maswahaba wala Tabiin kuwa wamekusanyika katika msiba baada ya kuzikwa.
7) Na msiba katika sheria ya Allaah سبحانه وتعالى Na Sunnah ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumsomea mtu wakati wa kukata roho “La ilaaha ila Allaah”. “Hapana mola anayepasa kuabudiwa kwa haki ila Allaah”. Na kisha kumwosha, kumvisha sanda, kufuata jeneza lake, kumzika na kungojea saa baada ya kuzika kwa kumuombea du‘aa na maghfira maiti. Amesema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na yeye akiwa kwenye mazishi kaburini:
((استغفروا لأخيكم وسلوا له التثبيت فإنه الآن يسأل))
((Muombeeni maghfira ndugu yenu na mumtakiye uimara (kutoyumba) kwani sasa anaulizwa)) [Abu Daawuud]
Na hivyo hivyo muwatayarishie chakula watu walio na msiba (waliofiliwa). Huu ndio utaratibu wa msiba wa kisheria na kinyume na hayo ni uzushi (bid’ah).
8) Msinililie kwa sauti….Wala msiyahesabu mazuri yangu. Wala msilie kwa sauti kubwa…wala msikwaruze nyuso zenu. Wala msizichane nguo...wala msijipige.
9) Kunakatazwa kabisa ada zote za uzushi kama kukusanyika Alkhamiys, arobaini, au baada ya maiti kutimiza mwaka, au siku za Iyd na kujiliza na sherehe za wakati mbali mbali. Msisome Qur-aan kwenye makaburi wala msigawanye sadaka na wala msichinje chochote chini ya jeneza.
10) Kwa jamaa zangu na marafiki wapendwa wanilipie madeni kabla ya kuoshwa na kukafiniwa (kuvishwa sanda) na watekeleze nadhiri zangu.
11) Nawausia watoto wangu, msiba na huzuni usizidi siku tatu. Na kwa mke wangu msiba ni miezi minne na siku kumi. Na asivae kwa wakati huo hariri wala nguo za rangi au asitie wanja, mafuta na asijipambe.
12) Pia nawausia watoto na jamaa zangu wazuru kaburi langu, waniombee du’aa pamoja na kuniombea maghfira. Hii itawasaidia kupata mazingatio na mawaidha katika mauti.
13) Vivyo hivyo nawausia watoto, jamaa, marafiki na watu wa msikiti wanikumbuke kwa wema, na kuniombea du’aa na kunitakia maghfira katika wakati wa Swalah zao kwa Allaah سبحانه وتعالى Wanaposujudu, baada ya Swalah na kusoma Qur-aan tukufu… Wakati wanapo hiji kwenye nyumba tukufu ya Allaah ili Allaah Aniondolee adhabu ya kaburi na adhabu ya moto wa Jahannam na Aniingize kwa Rehma yake peponi.
14) Inaruhusiwa kwa mke wangu (na kinyume chake) kuniosha na kunikafini.
15) Inaruhusiwa kungojewa kwa mzazi au mtoto mpaka afike kwa muda unaongilika akilini.
16) Inawezekana kunisalia kwenye makaburi kwa yule aliyekosa Swalah ya jeneza kabla ya kupita mwezi baada ya kuzika.
17) Gawanyeni kopi za wasiya kwa waliohudhuria mazishi na Swalah punde tu wanapoingia ili wapate kusoma na kutekeleza yalio ndani ya wasiya.
18) Ninawapatia habari kama nimemsamehe kila mwanaadamu aliye na haki yangu na ninawaomba nilio na haki zao wanisamehe.
19) Jueni kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema:
((ينقطع عمل ابن آدم من الدنيا إلا من ثلاث : صدقة جارية أو علم ينتفع به أو ولد صالح يدعو له))
((Amali ya binadamu hukatika baada ya kufa ila kwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, elimu yenye manufaa au mtoto mwema anayekuombea)) [Muslim na Ibn Maajah].
20) Ninawaageni kwa jina la Allaah Ambaye mwagano wake haupotei.
Wakati Wa Kutoka Roho (1)
Enyi wapenzi wangu!
Wakati unapokaribia wa kukata roho waiteni watu wema. Wahesabuni hivyo, wala simtakasi yeyote kwa Mwenyezi Mungu.
|
Jina |
Simu |
Jina |
Simu |
|
|
|
|
|
Wakati Wa Kukata Roho
Enyi vipenzi vyangu:
1) Msiwe na wasiwasi na msubiri kwani napenda kukutana na Allaah na kuweni na dhana nzuri. Na nisomeeni kalimah ya Tawhiyd, “La ilaaha illa Allaah” kwa ulaini na upole mpaka hayo yawe maneno ya mwisho ya kukutana na mola wangu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema
((من كان آخر كلامه لا إله إلا الله دخل الجنة))
((Yeyote yatakayokua maneno yake ya mwisho La illah illa Allaah ataingia peponi))
2) Nifungeni macho… zikazeni ndevu zangu kwa kitambara, kwa mapana juu ya kichwa changu. Na museme Khayr (wema) kwani Malaika wanaamini munayosema:
اللهم اغفر له .. وارحمه..
وارفع درجته فى المهديين المقربين..
واخلفه فى عقبه فى الغابرين..
واغفر لنا وله يا رب العالمين..
وافسح له قبره.. ونور له فيه.
“Ewe Mola Msamehe… na Umrehemu…Muinue daraja yake awe wa karibu walioongoka… Wabadilishie kizazi chake kwa yaliyopita….Na Utusamehe sisi na yeye ee Mola wa Ulimwengu…Mpanulie kaburi lake….na Umtilie mwangaza.
3) Nifunikeni kikamilifu na mnisitiri mwili wangu mzima na mniweke kitu kizito juu ya tumbo langu. Na semeni:
بسم الله وعلى سنة رسول الله إنا لله وإنا إليه راجعون اللهم أجرنا فى مصيبتنا واخلف لنا خيرا منها
“Kwa jina la Allaah na katika Sunnah ya Mtume wa Allaah. Bila shaka tunatokakwa Allaah na Kwake tutarudi, Ee Mola wetu tupe ujira katika huu msiba wetu na utupe badali bora zaidi”.
4) Na ikiwa nimehirimia kwa Hijjah au Umrah, basi msinifunike kichwa, uso wala msinitie manukato.
5) Na nikiwa niko katika vita vya jihadi, basi asinioshe yeyote, bali niacheni na nguo zangu hizo na nizikeni na damu yangu.
6) Msinielekezeni Qiblah na niacheni katika hali yangu hiyo wala msinisomee Qur-aan.
7) Nizikeni katika sehemu ambayo itakua rahisi kwenu.
8) Nilipieni madeni kabla ya kunikafini kutoka kwa mali yangu mwenyewe. Ikiwa sina mali basi waulizeni watu wa kheri katika jamaa na marafiki zangu… Allaah Atawajaza (atawapa) kila la kheri. Ikiwa hawatapatikana basi Allaah Aliyetukuka Atanilipia deni langu.
Wakati Wa Kuoshwa
1) Asihudhurie kuoshwa kwangu ila mwaminifu na aliye mwema.
2) Nisitirini wakati wa kuoshwa tupu yangu kutoka kitovu mpaka magoti.
3) Mwanzo nitoeni najasa. Kisha ziosheni viungo vya wudhuu na mwili wangu wote kwa maji na sabuni.
4) Kisha nitieni wudhuu wa Swalah kwa maji tohara lakini msiingize maji kwenye mdomo wala pua yangu. Kisha utieni mwili wangu kwa maji twahara mara tatu au tano… au saba.
5) Kisha nitieni maji ya waridi (marashi) kwenye nywele na vitanga vya mikono na sehemu zinazosujudu baada ya kumaliza kuniosha na kukauka.
6) Nivisheni bafta (kitambara) tatu nyeupe na mtie manukato baina yake na munistiri uso na miguu yangu.
7) Na ikiwa nimekufa shahidi katika vita basi asinioshe yeyote, niacheni na nguo hizo na munizike (nilivyokufa) na damu (kama imetoka).
Swalah Ya Jeneza
Imamu wa Swalah hiyo ni……………………………au awe ni mtu yeyote mwema. Swalah ya maiti (au jeneza) ina takbiyr nne:
1. Utasoma Suratul Faatihah baada ya Takbiyr ya kwanza.
2. Na dua ya Ibraahiym عليه السلام yaani,
(اللهم صلى على محمد ...)
“Allaahumma swali ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad kama Swallayta ‘alaa Ibraahyim wa ‘alaa aali Ibraahiym…” mpaka mwisho baada takbiyr ya pili.
3. Na mniombee baada ya takbiyr ya tatu.
اللهم إنا جئناك شفعاء له .. فشفعنا فيه
اللهم اغفر له وا رحمه .. وعافه واعف عنه
وأكرم نزله .. ووسع مدخله
وأغسله بالماء والثلج والبرد ..
ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من والدنس
وأبدله دارا خيرا من داره .. وأهلا خيرا من أهله
وزوجا خيرا من زوجه وأعذه من عذاب القبر وعذاب النار .
اللهم أبدل سيئاته حسنات
اللهم إن كان مسيئا فتجاوز عن سيئاته
Allaahumma inna ji-inaaka shufa’a-an lahu fashfi‘na fiyhi.
“Ee Mola sisi tumekuja kwako kumuombea Shifaa basi mpatie shufaa”
Allaahumma ghfir lahu waarhamhu wa ‘afihi waa‘fu ‘anhu
“Ee Mola Mghufirie na Umrehemu”.
Wa akrim nuzulahu wa wasi‘i mudkhalahu.
“Na Ukirimu kushuka kwake na Yapanue maingilio yake”.
Waaghsilhu bilmai wath-thalji walbard. Wanaqih minal Khatwaaya kama yunaqqath-thawabul abyadhw minad-danas. Wa-abdilhu daaran Khayran min daarihi wa ahlan khayran min ahlihi. Wazawjan khayran min zawjih Wa a ‘idhhu min adhabil Qabr wa adhaabin-naar Allaahumma abdili sayyiatahu hasanaat. Allaahumma in Kaana musiy-an fatajawaz ‘an sayyiatihi.
‘Na muoshe kwa maji, theluji na ubaridi (barafu)’ Na yasafishe makosa yake kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu. Na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake. Ikiwa anayeswaliwa ni mwanamke basi maneno haya hayatajwi (Na mke bora kuliko wake). Na mwepushe na adhabu ya kaburi na adhabu ya moto. Ee Mola mbadilishie makosa yawe ni thawabu. Na akiwa ni muovu basi yasamehe maovu yake.
4. Baada ya takbiyr ya nne soma du‘aa ifuatayo:
االلهم لا تحرمنا أجره ولا تفتنا بعده واغفر لنا وله وللمسلمين .
Allaahumma laa tahrimnaa ajrahu walaa taftinnaa ba ‘adahu waghfirlanaa walahu walilmuslimiyn.
‘Ee Mola Usituharamishie ujira wake wala Usitufitini baada yake na Utusamehe sisi na yeye na Waislamu wote’.
Katika Kulichukua Jeneza
1) Liharakisheni jeneza langu enyi wapenzi wa Mtume wa Allaah.
2) Na nyamazeni kabisa katika jeneza kama kwamba katika vichwa vyenu kuna ndege.
3) Wala wasifuate jeneza langu wanawake.
4) Wala asilie yeyote kwa sauti…. Bali waseme wote:
إنا لله وإنا إليه راجعون اللهم أجرنا فى مصيبتنا .. واخلف لنا خيرا منها
Inna liLlaahi wa inna ilayhi raaji ‘uun. Allaahumma ajirnaa fii musiybatina… wakhluflanaa khayran minha.
‘Bila shaka tunatoka kwa Allaah na Kwake tutarudi. Ee mola Tupe ujira katika huu msiba na Utupe badali iliyo bora zaidi’.
4) Subira wakati wa msiba mkubwa. Na kubwa zaidi ya hiyo kuna ujira wa ridhaa katika Qadhaa (hukumu) ya Allaah yote… kheri na shari…. Tamu na chungu.
(قل كل من عند الله فمال هؤلاء القوم لا يكادون يفقهون حديثا)
((Sema: Yote yanatokana na Mwenyezi Mungu Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno?)) An-Nisaa: 78
5) Kueni wanyenyekevu wakati wa jeneza mkitafakari jambo hili kubwa la mauti. Wala musizungumze kwa hadithi za dunia na musifanye dhihaka. Musiseme pia, “wahhiduhu” ‘mpwekesheni’ au “Astaghfiru Allaah” bali semeni “Bismillahi Wa’ala Sunnati RasuuliLlaah” “Kwa jina la Allaah na katika Sunnah ya Mtume wa Allaah”. Na amkumbuke Allaah yule mwenye kuchukua jeneza.
6) Msiguse jeneza kwa mikono, vitambara au vitu vingine kwa nia ya kujipata baraka: Hii ni haram.
Wakati Wa Kuzika Na Baada Yake
1) Mnapoingia kwenye makaburi semeni:
Assalaamu ‘alaykum daara qawmin muuminiyna antum saabiquuna wa ghadan inshaAllaah nahnu bikum laahiquun. Nas-alu Allaahu lana walakumu l’afiya.
“Amani iwe juu yenu nyumbani mwa watu waumini Nyinyi mumetutangulia na sisi kesho Anapopenda Allaah tutakua ni wenye kuwafuatia. Tunamuomba Allaah Atupatie sisi na nyie.
2) Enyi watu, wanizike marafiki zangu walio wema. Mnaponiingiza kaburini semeni:
(بسم الله وعلى سنة رسول الله)
“BismiLlaahi wa ‘alaa Sunnati Rasuuli Allaah.”
Kwa jina la Allaah na kwa Sunnah ya Mtume wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم
3) Baada ya kusawazisha mchanga na kumaliza kuzika semeni:
(اللهم أجره من الشيطان .. ومن النار ومن عذاب القبر , اللهم جافى الأرض عن جنبيه .. وصعد روحه ولقه منك رضوانا .. اللهم أسلمه إليك الأهل والمال والعشيرة .. وذنبه عظيم .. فاغفر له .. )
Allaahuma ajirhu mina shaytwaan wa minan naar wa min ‘adhabil qabr. Allaahumma jaafil ardhi ‘an jambayhi wa swa‘ad rawhahu walaqqih minka ridhwaana. Allaahuma aslimhu ilaykal-ahl walmaal wal ashiyrah wa dhambahu adhiym faghfirlahu…”
Ee Mola! Muepushe na shetani na moto na adhabu ya kaburi. Ee Mola! Ipokee roho yake na huku upo radhi nae. Ee Mola! Tumemsalimisha Kwako watu, mali na kizazi na dhambi zake kubwa kwa hiyo Msamehe.”
4) Enyi wapenzi wangu, marafiki na ndugu zangu katika imani ambao niliwapenda duniani kutafuta radhi za Allaah. Msiniache peke yangu wakati huu ambao nina haja kubwa nanyi. Kaeni pamoja nami kwenye kaburi kiasi cha saa huku mkiniombea du‘aa Allaah Atawaruzuku mwenye kuwaombea du’aa mnapokufa.
5) Kisha kisimame kikundi miongoni mwa watu wangu na ndugu zangu katika imani wangojee saa baada ya kuzikwa. Waniombee dua kisha wamalize kwa kusema:
اللهم أجرنا فى مصيبتنا .. واخلف لنا خيرا منها إنا لله وإنا إليه راجعون
Allaahumma Ajirnaa Fiy Musiybaatinaa Wa-khluf lanaa khayram-minhaa, Inna Lillaahi Wa Inaa Ilayhi Raaji'uun
‘Ee Mola! Tupe ujira katika huu msiba na Utupe badali iliyo bora zaidi. Bila shaka tunatoka kwa Allaah na Kwake tutarudi.”
Allaah Awalipe wote…
Msiba wa kisheria umemalizika kwa kulifuata janaza na wala hakuna msiba kabisa kwa wanawake….Allaah Awarehemu.
6) Mimi niko mbali na maneno au vitendo vinavyokwenda kinyume na sheria ya Allaah na Sunnah ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.
7) Muogopeni Allaah mwisho wa kumuogopa na sikilizeni na kutii na muwe na hadhari na maneno ya Allaah Aliyetukuka:
((إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَى مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ أُولَئِكَ يَلعَنُهُمُ اللّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ))
((إِلاَّ الَّذِينَ تَابُواْ وَأَصْلَحُواْ وَبَيَّنُواْ فَأُوْلَئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ))
((Hakika wale wanaoficha Tuliyoyateremsha nazo ni hoja zetu zilizo wazi na uongozi, baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu kitabuni, hao Anawalaani Allaah, na wanawalaani kila wenye kulaani))
((Ila wale waliotubu na kutengeneza na kubainisha, basi hao Nitawapokea na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye Rehema)) (Al Baqarah: 159-160).
8) Zingatieni maneno ya Allaah:
((أَلاَّ تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى)) ((وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلاَّ مَا سَعَى)) (( وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَى)) ((ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاء الْأَوْفَى)) ((وَأَنَّ إِلَى رَبِّكَ الْمُنتَهَى))
((Kwamba haichukui nafsi dhambi za nafsi nyengine)) ((Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya)) ((Na kwamba amali yake itaonekana)) ((Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili)) ((Na kwamba mwisho unarejea kwa Mola wako)). (An-Najm: 38-42)
Wasia Wangu Wa Mwisho
1) Nawausia mugawe mirathi kulingana na Sheria ya Allaah na yenye kumridhisha Yeye na kuweni enyi vipenzi vyangu ni wenye kupendana nyinyi kwa nyinyi. Na pendaneni na wapatieni wenzenu nafasi ya mwanzo ingawa hali zenu ni ndogo. Kila mmoja atapitia njia hii ya mauti kama mimi. Fanyeni amali kwa siku hii, mutapata furaha kukutana na Allaah mukiwa katika hali ya amani na utulivu. Siku ya Qiyaamah Ataita Allaah Aliyetukuka:
((أين المتحابون بجلالى ؟ اليوم أظلهم فى ظلى يوم لا ظل إلا ظلى))
(رواه مسلم)
((Wawapi waliopendana kwa ajili ya Utukufu wa Allaah leo nitawaweka kwenye kivuli Changu siku ambayo hakutakuwa na kivuli ila kivuli Changu)) [Muslim]
2) Kuweni karibu na mama yenu katika kheri na mpatieni badali kwa safari yake pamoja nami na nyinyi. Na kuweni wenye kumshughulikia kihakika, mtapata furaha hapa duniani na kesho akhera. Nami najikosha na kila kitendo au maneno yanayokwenda kinyume na sheria ya Allaah na Sunnah ya Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم.
Ninawaageni kwa jina la Allaah ambaye muagano Wake haupotei.
Imeandikwa tarehe………………………………
Mwenye kuusia………………………………………
Mashahidi……………………………………………
Wasiya Wangu Hasa
“Inafaa kwa Mwenye kuusia, kuusia thuluthi ya alivyoacha kwa mwenye kupenda.”
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

