018 Ni Lazima Kusukutua Na Kupaliza
Kusukutua ni kuosha mdomo na kuyazungusha maji ndani yake. Ama kupaliza, ni kuyafikisha maji mpaka ndani ya pua na kuyavuta kwa pumzi hadi mwisho wake. Na kupenga, ni kuyatoa maji puani (kwa mpumuo) baada ya kuyapaliza.
Kusukutua na kupaliza maji, ni mambo ya lazima kwa mujibu wa kauli sahihi zaidi za Maulamaa. Ni kwa dalili zifuatazo:
1- Ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameamuru kuosha uso
Tunajibu tukisema: “Vilevile vitefute viwili, kipaji, nje ya pua, nyusi mbili na sehemu nyingine za uso zimepewa majina maalumu, na kwa hivyo haviitwi uso!” ([1])
2- Ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameamuru kuosha uso kiujumla, na Mtume alilifasiri
3- Amri ya kupaliza na kupenga imethibiti kutokana na neno
((من توضأ فليستنثر))
((Mwenye kutawadha, basi apenge)).
Na katika riwaya nyingine:
(( إذا توضا أحدكم فليجعل في أنفه ماء ثم ليستنثر))
((Anapotawadha mmoja wenu, basi aingize maji puani mwake kisha apenge)).([3])
(( إذا توضأ أحدكم فليستنشق..))
((Anapowatadha mmoja wenu, basi apalize maji puani…))([4])
(( وبالغ في الاستنشاق إلا أن تكون صائما..))
((….na ubalighishe katika kupaliza isipokuwa
Shaykh wa Uislamu([6]) anasema: “…Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoa amri maalumu ya kupaliza, hakumaanishi kwamba ni muhimu zaidi kuliko kusafisha mdomo. Itawezekana vipi nailhali mdomo ndio sehemu tukufu zaidi ya kufanyia dhikri na kusoma, na mara nyingi hubadilika na kuwa na harufu mbaya?! Lakini kinachofananishwa hapa - na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi Zaidi – ni kuwa, mdomo ulipowekewa usheria wa kupigwa mswaki na jambo hilo likasisitizwa, na pia kuuosha kabla na baada ya kula, itakuwa imejulikana kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ametoa kipaumbele zaidi cha kuusafisha kinyume na pua ambayo imetajwa kwa ajili ya kubainisha hukumu yake ili isipuuzwe…”.
4- Ni kwamba amri ya kusukutua imekuja vile vile katika Hadiyth nyinginezo zenye uhakika zaidi. Ni
(( إذا توضأت فمضمض))
((Ukitawadha, sukutua)).([7])
Ninasema: “Na lau
(( إنها لا تتم صلاة أحدكم حتى يسبغ الوضوء كما أمره الله تعالى، فيغسل وجهه ويديه إلى المرفقين ويمسح رأسه ورجليه إلى الكعبين...))
((Hakika haikamiliki Swalah ya mmoja wenu mpaka akamilishe wudhuu wake
Hapa hakutaja kusukutua au kupaliza katika hayo ambayo Mwenyezi Mungu Amemwamuru, na kwa hivyo amekwenda sambamba na aya tukufu.
FAIDA:
Fahamu kwamba Wanazuoni wamehitalifiana juu ya hukumu ya kusukutua na kupaliza katika wudhuu na kuoga katika kauli nne.([9])
Kauli ya kwanza:
Ni wajibu kusukutua na kupaliza wakati wa kuoga tu, lakini kwa wudhuu haipasi. Yamesemwa haya na Ath-Thawriy, Abu Haniyfah na wengineo.
Kauli ya pili:
Ni Sunnah wakati wa kuoga na kutawadha. Haya yamesemwa na Maalik, Ash-Shaafi’iy, Al-Layth, Al-Awzaa’iy na jama‘ah.
Kauli ya tatu:
Yote mawili ni wajibu wakati wa kuoga na kutawadha. Haya yamesemwa na ‘Atwaa, Ibn Jurayj, Ibn Mubarak, Is-Haaq na riwaya iliyonukuliwa toka kwa Ahmad. Suala hili ni mashuhuri katika madhehebu ya Hanbali.
Kauli ya nne:
Kupaliza ni wajibu wakati wa kuoga na kutawadha, lakini kusukutua ni Sunnah. Yamesemwa haya na Ahmad katika riwaya, Abu ‘Ubayd, Abu Thawr na jopo la Maulamaa wa Hadiyth. Ibn Al-Mundhir ameichagua kauli hii.
KUOSHA NDEVU
Ikiwa nywele zilizoota usoni (ndevu, masharubu, kilambamchuzi, kope na nyusi) ni nyingi kiasi ambacho ngozi inakuwa haionekani, basi itatosheleza kuosha juu yake tu. Na
Ama ndevu refu za singa, si lazima kuziosha zile zilizoshuka, bali inatosheleza kuosha zile tu zilizo katika mpaka wa uso, kwa vile kinachokusudiwa katika uso ni ngozi basi. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Abuu Haniyfah na riwaya toka kwa Ahmad.
Ama kwa mujibu wa Ash-Shaafi’iy na madhehebu ya Ahmad, ni lazima kuosha nywele singa vyovyote zitakavyokuwa zimeshuka, kwani nywele hizo zimeota katika mahali pa faradhi, na kwa ajili hiyo zinaingia katika wigo wa vyenye kuonekana. Na rai hii ina nguvu zaidi. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi Zaidi.
([1]) Angalia katika “Nayl Al-Awtwaar” (1/174) chapa ya Al-Jiyl na “Ahkaam Al-Quraan” cha Ibn Al-‘Araby (2/563).
([7]) Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud (140), At-Tirmidhiy (38), An-Nasaaiy (1/66) na Ibn Maajah (448).
([8]) Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Abuu Daawuud (859), At-Tirmidhiy (302), An-Nasaaiy (2/20, 193), Ibn Maajah (460) na wengineo.
- Login or register to post comments
- Email this page
