Funga Ya Ramadhaan Na Ugonjwa Wa Kisukari
Lengo la makala hii ni kutazama mabadiliko muhimu yanayoweza kutokea kwa wagonjwa wa Kisukari wakati wa Swawm ya Ramadhaan, na pia kutazama usalama wa kufunga mwezi huu kwa mgonjwa wa Kisukari.
Licha ya tafiti mbalimbali zinazohusu athari za kimwili za funga ya Ramadhaankwa wagonjwa wa kisukari, watafiti bado mpaka sasa hawajaona kwa mgonjwa yeyote wa kisukari anayefunga, mabadiliko ya kimwili katika uzito wa mwili, glukosi ya damu, Insulini au lehemu.
Katika kipengele cha maelekezo cha makala hii, tunapendekeza kuwa wagonjwa wa kisukari waendelee na utaratibu wao wa kazi na lishe. Pia inakataliwa wagonjwa hao kubadili utaratibu wao wa dawa hasahasa wale waliogundulika kuwa na kisukari cha tabaka la Kwanza (type 1).
Kwa uangalifu, elimu sahihi na kwa udhibiti bora wa ugonjwa wa kisukari, tunahitimisha kuwa wagonjwa wengi wenye tabaka la pili (type 2) na baadhi ya wagonjwa wa tabaka la kwanza (type 1) wanaotaka kufunga, wanaweza kufunga kwa uangalifu.
Funga ya Ramadhaan ni amri ya kutekelezwa mwaka hadi mwaka. Katika zoezi hili, Uislamu unataka watu wajizuie kuanzia Alfajiri hadi Magharibi.
Ile adha ya kufunga inalenga kuwafunza Waislamu nidhamu ya ndani ya nafsi na uwezo wa kujizuia na kuwafanya wajuwe dhiki ya masikini. Waislamu hutakiwa sio tu kujizuia kula na kunywa bali pia wajizuie kutia mdomoni dawa au kutumia maji ya vitamini.
Mwezi wa Ramadhaan huchukua kipindi cha siku 28 hadi 30. Tarehe za kufunga hupishana kila mwaka kwa sababu Ramadhaan hufuata kalenda ya mwezi (lunar calendar).
Kila mwaka funga huanza muda ule ule wa Alfajiri hadi kuzama kwa jua, kipindi hiki hutofautiana mahali na mahali na msimu na msimu. Katika miezi ya kiangazi na katika latitudo kaskazini, Swawm yaweza kuchukua saa 18 au zaidi.
Uislamu unashauri kuwa Waislamu wanaofunga wale chakula kiitwacho "daku" kabla ya Alfajiri. Baadhi ya watu huondolewa wajibu wa kufunga kutokana na ugonjwa ambao unaweza kuleta madhara kwa kufunga. Watu hawa huruhusiwa kuacha kufunga kwa siku hadi zote thelathini kutegemeana na hali ya ugonjwa.
Watu waliogundulika kuwa na kisukari nao huingia katika kundi hili. Ingawaje wameondolewa katika wajibu wa kufunga lakini baadhi yao hupendelea kufunga.
Madaktari katika nchi na jamii za Waislamu mara nyingi hukabiliana na kazi ngumu ya kuwashauri wagonjwa wa kisukari juu ya usalama wa kufunga pamoja na kushauri kuwa vyakula maalum na dawa zifuate ikiwa wameamua kufunga.
Uhaba wa vitabu vinavyozungumzia jambo hili ndio unaoleta ugumu katika kujibu maswali haya. Kuamua kwa usahihi kumruhusu kitabibu mgonjwa wa kisukari afunge, ni lazima madaktari wawe na ufahamu wa ndani wa athari za funga ya Ramadhaan kwa wagonjwa wa sukari.
Katika makala haya kwanza tunatazama kanuni za mfumo wa uchomaji wa kabohaidreti na mabadiliko ya baadhi ya nyendo za baiokemia kwa wagonjwa wa kisukari wanaofunga Ramadhaan.
Kisha tutazame mashauri ya hivi sasa ya tiba ambayo huwaruhusu wagonjwa kadha wa kadha wa kisukari kufunga na kutoa maelezo kwa wagonjwa wa kisukari hasa wale wa tabaka la kwanza (Type 1) ambao hawahitajiki kufunga lakini wao wanang'ang'ania kufunga.
Hali ya mwili wa mgonjwa wa kisukari katika mwezi wa Ramadhaan
Athari za funga ya muda mfupi tu ya majaribio juu ya uchomaji wa kabohaidreti imetafitiwa kwa mapana na marefu. Kwa ujumla imegundulika kuwa upungufu mdogo wa Glukosi (serum glucose) hutokea kwa watu wa makamo saa chache tu baada ya funga kuanza.
Hata hivyo, upungufu huo wa glukosi hukoma kutokana na ongezeko la glukoneogenesis katika ini. Hali hii hutokea kwa sababu ya kupungua kwa mchanganyiko wa Insulin.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


