Husda Inayofaa Na Isiyofaa
SWALI:
assalamaaleykumwarahmatulallataalawabarakatuh
napenda kuuliza
waaleykumsalaamwarahmatuallataalawabarakatuh.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ingelikuwa ni vizuri
Husda (al-hiqd) ziko aina mbili; husda nzuri na mbaya; nzuri ni ile ambayo umemuona mwenzio amejaaliwa neema ya
عن أبي سعيد قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((لا حسد إلا في اثنتين : رجل آتاه الله القرآن فهو يتلوه آناء الليل وآناء النهار , فيقول الرجل : لو آتاني الله مثل ما آتى فلانا فعلت مثل ما يفعل , ورجل آتاه الله مالا فهو ينفقه في حقه فيقول الرجل : لو آتاني الله مثل ما آتى فلانا فعلت مثل ما يفعل)). أحمد
Hivyo husda kama hii haimdhuru mtu na wala mtu mwenye kuhusudu kwa kutamani kupata neema kisha afanye mema hapati dhambi kuwa na husda
(( وَلاَ تَتَمَنَّوْاْ مَا فَضَّلَ اللّهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَى بَعْضٍ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُواْ وَلِلنِّسَاء نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ وَاسْأَلُواْ اللّهَ مِن فَضْلِهِ إِنَّ اللّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا))
((Wala msitamani alichowafadhili Allaah baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika waliovichuma, na wanawake wana fungu katika waliovichuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu)) [An-Nisaa: 32]
Kwa hiyo aliyekosa neema fulani inampasa aridhike na alivyojaaliwa na akipenda amuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ambaye Ndiye mtoaji rizki na neema zote Naye ni Rahiymun-Kariym (Mwenye kurehemu na Mkarimu).
Na kutoka katika Sunnah:
عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم : ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً، المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا – (ويُشِيرُ إلى صَدْرِه ثَلاثَ مَرَّاتٍ ) بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمِ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ: دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ)) مسلم
Kutoka kwa Abu Hurayra (Radhiya Allaahu 'anhum) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Msioneane choyo, wala msizidishiane bei (za vitu), wala msichukiane, wala msipigane mapande (msitengane), wala msishindane kwa kupunguza bei. Lakini kuweni ndugu, enyi waja wa Mwenyeezi Mungu, Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamvunji, hamwambii uongo wala hamdharau. Ucha Mungu uko hapa (huku akiashiria kifuani kwake kwa vidole vyake) mara tatu. Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu. Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake; damu yake,
Husda hiyo huenda imamdhuru mtu akafikwa na maovu,
- Kusoma Qur-aan kwa wingi kwani Qur-aan ni uongofu, nuru, poza na tiba ya nyoyo na mwili.
- Aayah tano za mwanzo katika Suratul-Baqarah.
- Aayatul-Kursiy na Aayah mbili zinazofuatia.
- Aayah mbili za mwisho katika Suratul-Baqarah.
- Kusoma Suratul-Ikhlaasw (Qul-Huwa Allaahu Ahad) na Al-Ma'udhaataan (Qul-A'uudhu Birbbil-Falaq na Qul-A'uudhu Birabbin-Naas) mara tatu kila asubuhi na jioni.
- Nyiradi za asubuhi na jioni zilioko katika kitabu cha Hiswnul Muslim.
Hizi pekee zinamtosheleza mtu kumkinga na kumtoa katika husda na kila aina ya shari ikiwa atazidumisha kila siku ipasavyo. Lakini wengi hawalitii manani hili jambo muhimu la kujikinga na pia kujipatia neema nyingi, na jambo ambalo hata halimchukui mtu zaidi ya dakika kumi. Wanasubiri hadi mtu yamfike maovu ndipo anapoanza kuhangaika.
Kwa maelezo zaidi soma mada zifuatazo:
Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqya - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi
Duaa ya kupatwa na janga au balaa
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
