Skip navigation.
Home kabah

'Aqiydah Yetu Hivi Leo



  Imetayarishwa na gazeti la Al-Hudaa

 

Licha ghuba hiyo pana isiyo na kivuko baina ya zama za nyuma na zama  hizi na tofauti kubwa kati ya jamii hizi mbili bado watu wa jamii zote hizi mbili wanadai kuwa wao ni Waislamu. Imani sahihi ndiyo bendera iliyosimamishwa na  jamii zote hizi mbili.

Jamii ya kwanza ilisimamisha bendera hii kwa Ikhilasi na ikajiendesha na kuyaendesha maisha yake kwa kufuwata misingi ya Uislamu. Na jamii nyingine imesimamisha bendera hii kama urathi na mila tu lakini inaishi kwa namna ambayo inauficha undani wa bendera hiyo.

Sasa, je tumepata funzo kuwa tamko tupu la imani halina tija iwapo haliambatani na mwenendo unaowiana nalo pamoja na maisha ya kujitoa muhanga? MwenyeziMungu Amrehemu Imam Shafii aliyesema:

 “Lau watu wangeliisoma Surati Asri tu, basi ingewatosha”. Katika Sura hii, Allah anasema:

“Naapa kwa zama  kuwa binadamu yuko katika hasara. Isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri na wakausiana  (kushikamana) na subira ( 103:1-3).

Tunazungumzia Aqida, ile ya Tawhiid. Aqida ya Mitume na Manabii kuanzia Adam (as) hadi Muhammad (swalallahu alaihi wasalam). Ile Aqida ya wenzetu wachaMungu waliotangulia Salaf-us-Salih na ya wale waliofuata uchaMungu miyongoni mwa wanazuoni na watu wa kawaida.

Tunazungumzia Aqida si kwa minajili ya mabishano ya kifalsafa au majadiliano ya kifalsafa bali ni kwa ajili ya kusahihisha imani ya umma wetu na kuitakasa Aqida yao na mambo ya uzushi na mambo potofu ambayo yamepandikizwa.

 Tunarudia kulisisitiza hili ili lijikite katika nyoyo na ziishi kwa mujibu wa taratibu zake. Tunatamka mbele ya Allah kuwa tunajikinga na bidaa yoyote inayopingana na Aqida ya wachaMungu waliotangulia. Na tunaomba msaada wake kwamba matendo yetu yasiende kinyume na maneno yetu.

                              Hii ndiyo Aqida yetu

-Iman ni kutamka kwa ulimi, kutenda kwa viungo na kuwa na yakini moyoni. Iman huongezeka kwa matendo ya utii na huporomoka kwa matendo ya uasi, na kwa hali hiyo waumini wanatofautiana daraja.

-Dhambi na matendo ya uasi huporomosha iman lakini haziuwi kabisa kiini chake. Lakini Kufuru kubwa (al-Kufr al-Akbar) huuwa kabisa Iman

-Kufuru ziko za aina mbili; kubwa (akbar) na ndogo (asghar). Kufuru kubwa humtoa mtu kabisa katika dini ya Uislamu na hivyo kumfanya aitwe kafiri. Kufuru ndogo ni kitendo  cha uasi ambacho kimeitwa kufuru ndogo ili kumtahadharisha mtu na kumzuia asiendelee nayo. Dhambi ndogo na kubwa zote hunasibiana na Shirk, Unafiki (Nifaq), Udhalimu (dhulm) na Ufasiki (Fisq).

-Muislamu hawi kafiri kwa kutenda mambo ya uasi hata yakiwa mengi kiasi gani na hata kama hakutubia kwa mambo hayo maadam hayaridhii moyoni. Fasiki anayeamini makatazo ya dhambi na uovu haitakidiwi kuwa ni kafiri hata kama anaendelea kutenda maovu yake na hatubu na hata akifa katika hali hiyo. Hukumu yake ya Akhera anaachiwa MwenyeziMungu. Ambaye anaweza kumsamehe au kumuadhibu katika moto wa Jahanamu kwa muda fulani na kisha kumtoa na kumuingiza Peponi.

 -Pale Iman na Uislamu vinapotajwa pamoja, imani huwa na maana ya kuamini kwa moyo na Uislamu huwa na maana ya utendaji wa kiwiliwili. Vinapotajwa kwa nyakati tofauti vyote huhusiana na dini ya Uislamu kwa ujumla.

-Hatumuhukumu mtu ukafiri mpaka ukafiri wake udhihiri, utolewe ushahidi usio shaka na watu wanaostahili kufanya hivyo ili ithibitike kuwa mtu huyo ametenda matendo ya kufuru kwa kujua na kwa makusudi ya nafsi yake.

-Tunaamini kuwa Allah (SW) ndiye Muumba na Mola anayeturuzuku, ndiye Muhuishaji na ndiye Mfishaji, ndiye Mfufuaji, ndiye Mrithi, ndiye Mwenye kunufaisha na kudhuru. Hatuna mola mwingine ila Yeye, “sema nimuombe Mola Mwingine badala yake, ilihali Yeye Ndiye Mola wa Viumbe vyote?” (6:164)

-Yeye Ndiye Aliyetukuka na aliye juu, hana mke, mwana, mshirika wala mshindani, “Yeye ni Allah, Wa Pekee, Hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna anayefanana Naye (112)

-Allah Ta’ala Ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa na ndiye anayestahiki ibada. Waja wake waelekee kwake kwa kila jambo, wamuogope Yeye, wamtegemee, wamdhukuru, wamuombe, wampende na kumtii, waombe msaada nanusura Kwake