Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi
(Na Fat-hi Al-Jundiy)
Tiba Ya Jicho La Husda
Uwezo wa kuwadhuru wengine kwa kuwatazama au kuonea kijicho ambao hujulikana kama “kijicho” kweli upo. Ibn Abbas kasimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)kasema: “madhara ya Kijicho (al-ayn) kweli yapo. Kwani kama kungelikuwa na jambo la kuitangulia kadari basi lingekuwa ni dhara la kijicho” (Muslim).
Abu Umamah ibn Sahl ibn Hunayf kasimulia hivi: “Baba yangu, Sahl ibn Hunayf, alifanya josho (ghusl) pale al-Kharrar. Akavua juba alilokuwa amelivaa huku Amir ibn Rabia akimtazama, na Sahl alikuwa na ngozi nyororo nyeupe.
Amir akasema: “Sijapata kuona (ngozi) mfano wa hii ambayo nimeiona leo, haifanani hata na ngozi ya mwanamwali.” Papo hapo Sahl akawa mgonjwa na hali yake ikawa mbaya sana.
Kisha Mtume akamwambia Amir, ‘tia udhu kwa ajili ya mwenzio’. Amir akatia udhu. Baada ya Amir kutia udhu, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)akanyunyiza maji ya udhu ya Amir kichwani na mwilini mwa Sahl. Halafu Sahl akaondoka pamoja na Mtume na hakuwa na ugonjwa tena”. (Ahmad).
Endapo mtu aliyemuonea kijicho mwenziwe hajulikani, basi tiba inaweza kufanywa kwa Ruqyahh, duwa zinazoswihi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) zikiambatana na unyenyekevu uliojaa ikhilasi kwa Allaah.
MwenyeziMungu daima huitikia maombi ya wenye shida.kama isemavyo Qur-aan, “Au yule anayemjibu anayedhikika amwombapo na kuondoa dhiki (yake)..?” (27:62).
Ibn Qayyim kasema: “miongoni mwa njia za kuomba ulinzi wa MwenyeziMungu na zile zinazojumuisha Ruqyah ni: usomaji wa mara kwa mara wa Surat al-Falaq, surati An-Nasi, surati Al-Fatiha na Ayatul Kursiyu.
Mtu pia asome dua za Mtume kama hizi:
Tiba Ya Uchawi
Huwa inasemwa kuwa Kinga ni bora kuliko Tiba. Kwa hiyo basi, mtu ajikinge na madhara ya uchawi kabla haujatokea. Pamoja na mambo mengine, kinga hii hupatikana kwa kumtii na kumuabudia Allaah pekee, kuamini Qudra na Qadari Yake, kuomba ulinzi Wake kwa kumdhukuru mara kwa mara na kusoma dua za Mtume katika nyakati zinazofaa.
Kula tende Ajwah ni njia nyingine ya kuzuia madhara ya uchawi kama ilivyobainishwa katika Hadith iliyosimuliwa na Sa’ad ambapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)kasema, “mtu akila tende Ajwah kila asubuhi, hatadhurika kwa sumu au uchawi kwa siku hiyo.” (Al-Bukhaariy na Muslim).
Ni muhimu kutambua kuwa wale wanaostahili kunufaika na Hadith hii ni wale tu wanaoamini kikwelikweli haya aliyoyasema mtume na wanaoamini kwa dhati kabisa kuwa kila alichosema ni ukweli, ama wathibishe ukweli wake au la. Na kuhusu tiba ya uchawi, mtu aliyerogwa aoneshe subira na airidhie kudra ya Allaah. Pia ni jambo la msingi kwake kujirudi kwa dhambi yoyote ambayo ameitenda na afanye toba ya kweli kwa dhambi hiyo.
Anapotafuta tiba, aepuke kabisa tiba za “kitekero” au”kisangoma” zinazotolewa na waganga magirini. Kama ikibidi, basi anaweza kushirikiana na watu wachaMungu kumuomba msaada Allaah kwa utaratibu anaouridhia Allaah.
Inaendelea.../3
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

Assalamu
Assalamu Aleikum,
Nawashukuru kwa hii website...InshaAllah Allah awape baraka juu ya baraka ameen. nina swali..nini maana ya tende Ajwah?
God bless you all this is a
God bless you all this is a very educative website for muslim thank you and keep it up.
asalam alaykum warahmatulahi
asalam alaykum warahmatulahi wabarakatu,
it could be much better if your remember ALMIGHTY ALLAH and say MANSHAALAH MY ALLAH REWARD YOU IN THIS WORLD AND HEREAFTER . and may ALLAH SUBHANA WATA'A'LA PROTECT YOU FROM EVILS OF THIS WOLRD
WASALAM...