Kisa Cha Haabiyl (Abel) na Qaabiyl (Cain)
Imekusanywa na: Ummu Iyyaad
Kisa hiki cha Qur-aan tumeelezwa na Allaah سبحانه وتعالى katika Sura Al-Maida Aya no 27 mpaka aya no 31.
)) وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِن أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ((
27. Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu.
)) لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَاْ بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لَأَقْتُلَكَ إِنِّي أَخَافُ اللّهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ((
28.Ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote
) إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ وَذَلِكَ جَزَاء الظَّالِمِينَ))
29. Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako, kwani wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya wenye kudhulumu
)) فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ))
30. Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika
)) فَبَعَثَ اللّهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءةَ أَخِيهِ قَالَ يَا وَيْلَتَا أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءةَ أَخِي فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِين((
31. Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi kumsitiri nduguye. Akasema: Ole wangu! Nimeshindwa kuwa
Qabil na Habil ni watoto wanaume wa mwanzo wa Adam عليه السلام ambao, kutokana na Wataalamu wengi na Wema Waliotangulia (Salaf Swalih) wamesema kuwa Allaah سبحانه وتعالى alimruhusu Adam عليه السلام awaozeshe watoto wake wa kike kwa watoto wake wa kiume ili kizazi kiongezeke.
Na wamesema kuwa katika kila mimba aliyokuwa akibeba Bibi Hawa, alikuwa akizaa pacha mwanamume na mwanamke. Ikawa kuozeshwa kwa Qabil na Habil kukawa kwamba pacha wa Qabil (mwanamke) aolewe na Habil na pacha wa Habil (mwanamke) naye aolewe na Qabil.
Pacha wa Habil hakuwa mzuri wa sura bali pacha wa Qabil alikuwa mzuri, kwa hiyo Qabil akakataa kumuoa dada yake Habil akataka kumuoa dada yake mwenyewe aliyezaliwa nae pacha. Adam عليه السلام akakataa jambo hili na akawaambia wote wawili watoe َQurbani (dhabihu au kafara) na yule atakayetakabaliwa Qurbani yake atakuwa ndie mwenye haki . Allaah سبحانه وتعالى Akatakabali Qurbani ya Habil.
Maelezo kuhusu Qurban kutoka Tafsiir ya Sh. Abu Bakar Al-Jazairi
Ilikuwa ni Sunna ya Allaah سبحانه وتعالى kuteremsha moto kutoka mbinguni na kuunguza Qurbani (kafara ) ya mtu aliyemtakabalia, na asiyemtakabalia hateremshi moto.
((إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ))
{Mwenyezi Mungu huwapokelea wacha Mungu}
Uthibitisho wa kauli hii tunapata katika hadithi sahihi kuhusu kondoo wa Bani Israil walipoharimishiwa nao na ikawa halali kwa Umma wa Kiislamu kama alivyotueleza Mtume صلى الله عليه وسلم katika kutaja fadhila za utume wake kulinganisha na watume wa mwanzo katika hadithi Sahihi iliyosimuliwa na Muslim :
(( وأحلت لي الغنائم، ولم تحل لأحد قبلي ))
((Na nimehalalishiwa kondoo wala hakuhalalishiwa kabla yangu mtu))
(kondoo hawa wanaokusudiwa ni
Baada ya kutakabaliwa Habil Qurbani yake, Qabil akaingiwa na wivu na hasira akataka kumuuwa ndugu yake ambaye alimjibu:
)) لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَاْ بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لَأَقْتُلَكَ إِنِّي أَخَافُ اللّهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ))
{Ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote} Al-Maida 28
)) إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ وَذَلِكَ جَزَاء الظَّالِمِينَ))
{Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako, kwani wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya wenye kudhulumu} Al-Maida 29
Lakini Qabil alifuata matamanio ya nafsi yake na akamuuwa ndugu yake Habil.
Ibn Jarir amesema kuwa alipokuwa anataka kumuuwa ndugu yake kaanza kwanza kumnyonga shingo yake. Ibilisi akachukua mnyama na akaweka kichwa chake katika jiwe kubwa (rock) akachukua jiwe lengine na akavunja kichwa cha yule mnyama. Hii yote ni kumuonyesha Qabil vipi amuuwe ndugu yake, maana
Qabil akafanya vile vile kumuuwa ndugu yake Habil
Bibi Hawa akaanza kulia mpaka Adam عليه السلام alipokuja na kumuuliza mkewe "Unalilia nini?" lakini Bibi Hawa hakumjibu akawa anaendelea kulia tu. Adam عليه السلام akamuuliza mara mbili tatu hivi lakini Bibi Hawwaa hakumjibu akiendelea kulia tu. Adam عليه السلام akamwambia Bibi Hawwaa "Wewe na kizazi chako cha kike mtarithi kulia huku na mimi na kizazi changu cha kiume tutaepukana nacho" (Na hii labda ndio maana wanawake huwa wao machozi yao yako karibu na wakati wa misiba wao ndio hulia zaidi) Wallaahu A'aalam.
Baada ya kumuuwa ndugu yake, Qabil akamwacha chini akawa hajui amfanye nini. Hapa tena Allaah سبحانه وتعالى Akatuma kunguru wawili wapigane mbele yake ili wamuonyeshe nini la kufanya maiti ya ndugu yake. Wakapigana wale kunguru, alipomuuwa mmoja mwenzake akachimba shimo ardhini akamtia ikisha akamfukia kwa mchanga .
))فَبَعَثَ اللّهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءةَ أَخِيهِ))
{Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi kumsitiri nduguye }
Qabil alipoona hivyo akaanza kujuta na kujilaumu nafsi yake kwa kusema:
((قَالَ يَا وَيْلَتَا أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءةَ أَخِي فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ))
{Akasema: Ole wangu! Nimeshindwa kuwa
‘Aliy bin Abi Talhah kasema kuwa Ibn Abbas kasema: "Kunguru alikuja kwa kunguru aliyekufa akamwagia mchanage juu yake mpaka akafunikika katika ardhi. Yule aliyemuuwa ndugu yake kasema:
((يَا وَيْلَتَا أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءةَ أَخِي))
Ole wangu! Nimeshindwa kuwa
(At-Twabariy 10. 226)
MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKA KISA HIKI
· Kutokumtii Allaah سبحانه وتعالى huwenda kukampeleka mtu kufanya maasi makubwa.
· Jihadhari na Ibilisi Muovu!!
· Bora kujilinda kutokufanya maasi kuliko majuto.
· Mafundisho ya kwanza kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى kuhusu kuzikana tunapokufa.
· Binaadamu tumeumbwa kutoka udongo wa ardhi na huko ndiko tutakaporudi kuzikwa.
· Allaah سبحانه وتعالى Ametufahamisha kuwa kufanya ufisadi duniani au kuuwa nafsi moja ni kama mfano wa kuuwa jamii ya wa watu , kwa hiyo madhambi yake ni makubwa
· Na ukimsaidia mtu katika siha yake, kama kwa mfano ukamlipia gharama za matibabu na kadhalika ni kama mfano wa kuokoa jamiii ya watu kutokana na mauti (Na Allaah سبحانه وتعالى Ndie mwenye kufisha na Kuhuyisha) lakini sababu nyingine huwa zinatoka kwetu binaadamu.
Kaendelea Allaah سبحانه وتعالى baada ya kisa hiki kwa kusema hayo.
))مِنْ أَجْلِ ذَلِكَ كَتَبْنَا عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا وَلَقَدْ جَاء تْهُمْ رُسُلُنَا بِالبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَلِكَ فِي الأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ))
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni
· Visa vya Qur-aan vina mafundisho mazito, mazuri ya manufaa ya maisha yetu na hidaaya kwetu
لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ ِلأُوْلِي الأَلْبَابِ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَى وَلَكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Kwa hakika katika visa vyao yamo mazingatio kwa wenye akili. Si maneno yaliyo zuliwa, bali ni ya kusadikisha yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu yenye kuamini.
(Sura Yusuf 111)
Allaahu A'alam
(Maelezo kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr na Aysarut-Tafaasiyr - Shaykh Abu Bakr Al-Jazaairy
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


