Jihisabu Kabla Hujahisabiwa
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Ihisabu nafsi yako katika kila jambo hapa Duniani kabla ya kufariki na kabla ya kuhisabiwa Siku ya Malipo mbele ya Mola Mlezi. Kutengenea kwa tabia na amali zetu kutategemea namna Muislamu anavyozichunga amali zake kwa namna sawa na ilivyo kwa tajiri na biashara yake. Rasilimali ya tajiri huwa inachungwa, basi vivyo hivyo iwe kwa Muislamu kuchunga fardhi zake. Sunnah zote zitazame
Muislamu anatakiwa akae kila kukicha na kwa muda mrefu ili atengeneze matatizo kwa kuihisabu nafsi yake kwa kila kitendo katika siku yake. Akae kwa kupiga hisabu aliyoyatenda kuanzia asubuhi hadi usiku, na akiona upungufu afanye upesi kulipa faradhi na afanye pupa ya nyongeza katika mambo ya Sunnah na mambo mengine yenye fadhila.
Khasara ya kupitwa na fadhila pamoja na faradhi ajutie mno fursa hiyo. Atubu haraka kutokana na kufanya maasi na madhambi kwa kuisawazisha nafsi yake na Mola wake. Ajutie hali hiyo iliyompita na aendelee kila kukicha kufanya mema ili alipe yale aliyoyapoteza.
Hivyo ndivyo namna ya kuilea nafsi na kuielekeza katika njia iliyo sahihi. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema katika Kitabu Chake:
{{Enye mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu; na kila mtu aangalie, (atazame) anayoyatanguliza kwa ajili ya kesho (Akhera); na Mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu Anazo habari za mnayoyatenda (yote)}} [Suratul-Hashr: 18]
Kwani nafsi ni
{{…kwa hakika (kila) nafsi ni yenye kuamrisha
Njia muafaka ya kuizuia nafsi kutenda maovu ni kujiweka karibu na Mola Mlezi kwa kuhisabu amali ulizozitenda kila siku. Hivyo, ni vyema tuzifanyie hisabu amali zetu kabla hatujahisabiwa na tuzifanyie wizani kabla hatujapimiwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
