Fadhila Za Suratul-Kahf Surah Namba :18
Imeandikwa na Alhidaaya.com
بِسْمِ اللَّه والْحَمدُ لِلَّه والصَّلاَةُ والسَّلاَم عَلى رَسوُلِ اللَّه صلى الله عليه وعلى آله وصحبه وسلم
1. Ukihifadhi aya kumi za mwanzo utahifadhiwa na shari ya Dajjal
((عن أبي الدرداء أن النبي صلى الله عليه وسلم قال : " من حفظ عشر آيات من أول سورة الكهف عصم من الدجال (( رواه مسلم
((Imetoka kwa Abu Ad Dardaa kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema, Atakayehifadhi Aya kumi za mwanzo wa Suratul-Kahf atalindwa na Dajjaal))Muslim
2.
(( قال عليه الصلاة والسلام : من قرأ سورة الكهف ليلة الجمعة، أضاء له من النور ما بينه وبين البيت العتيق) ) صححه الألباني في صحيح الترغيب والترهيب
((Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم Atakayesoma Suratul-Kahf usiku wa Ijumaa, ataangaziwa na nuru Baina yake na baina ya nyumba ya zamani (Al-Kaaba)) Sahiih Albani
3.
((وقال صلى الله عليه وسلم : من قرأ سورة الكهف كما أنزلت كانت له نورا يوم القيامة ، من مقامه إلى مكة ، و من قرأ عشر آيات من آخرها ثم خرج الدجال لم يضره ....)) صححه الألباني في سلسلة الأحاديث الصحيح
((Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم Atakayesoma Suratul-Kahf kama ilivyoteremshwa, atakuwa na mwangaza siku ya Kiama aliposimama mpaka Makkah, na atakayesoma Aya kumi za mwisho kisha akitokea Dajjaal hatomdhuru )) Sahiih Albani katika mfululizo wa Hadithi Sahiihi
Sura hii miongoni mwa sura tano katika Qur'aan zinazoanza na 'Alhamdulillah'
Suratul-Kahf
((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَى عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجَا))
1. Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo.
Sura nne nyingine ni hizi zifuatazo.
Suratul-Fatiha
((بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ )) (( الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ((
1. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
2. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;
Suratul-An'aam
((الْحَمْدُ لِلّهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِم يَعْدِلُونَ ))
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya
((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي الْآخِرَةِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ))
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni
Mwenye hikima, Mwenye khabari
((الْحَمْدُ لِلَّهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَى وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاء إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ))
1. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
Kwa hivyo tuanze kwanza kwa kutaja Fadhila za 'Al-Hamdulillah' (kumshukuru Allaah):
Neema za Allaah سبحانه وتعالى ni nyingi sana na Amezitaja katika Qur'aan nzima katika aya mbali mbali Neema Zake hizo, na zaidi zimetajwa katika Suratun-Nahl. Lakini kwa jinsi wingi wa Neema za Allaah سبحانه وتعالى zilivyo hawezi mtu katu kuzihesabu neema hizo kwani Mwenyewe Ameshatuthibitishia kuwa hatuwezi kabisa kuzihesabu kama Alivyosema katika aya hizi mbili:
((وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ وَإِن تَعُدُّواْ نِعْمَتَ اللّهِ لاَ تُحْصُوهَا إِنَّ الإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ))
((Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema))
Surat Ibrahiim:34
((وَإِن تَعُدُّواْ نِعْمَةَ اللّهِ لاَ تُحْصُوهَا إِنَّ اللّهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ))
((Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu))
An-Nahl:18
Neema hizo zote pia tutambue kuwa zinatoka Kwake Allaah سبحانه وتعالى pekee, na wala hakuna yeyote anayemiliki chochote bila ya kuwa amewafikiwa neema hiyo kutoka Kwake Mwenye Kumiliki Mbingu na Ardhi.
((لِلّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ))
((Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Naye ni Muweza wa kila kitu)) Al-Maidah:120
((وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ ... ))
((Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu…))
An-Nahl:53
Kwa hiyo inatupasa tuwe tunamshukuru Allaah سبحانه وتعالى kila mara kwa kila neema alizotujaalia. Na Mtume wetu mpenzi صلى الله عليه وسلم ametufundisha aina nyingi za kumshukuru Allaah سبحانه وتعالى
Kwanza tujue kuwa kila tunapomshukuru Allaah سبحانه وتعالى hutuzidishia neema zake. Naye Ametoa tangazo kwa wote kuthibitisha hilo:
((وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لأَزِيدَنَّكُمْ ... ))
((Alipotangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru nitakuzidishieni …))
Surat Ibrahiim :7
NAMNA YA KUMSHUKURU ALLAAH KAMA ILIVYO KATIKA QUR'AAN
Aya za Shukr katika Qur'aan
((...رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ ((
((Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema)) An Naml:19
((...رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ ((
((Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu)) Al-Ahqaaf 15
Shukr katika Sunnah
Hii ni dua nzuri kabisa ya kuomba kila baada ya Tashahhud ili iweze kukusaidia kuweza kumshukuru Allaah سبحانه وتعالى kwa vizuri kabisa.
اللّهُـمَّ أَعِـنِّي عَلـى ذِكْـرِكَ وَشُكْـرِك ، وَحُسْـنِ عِبـادَتِـك
Allaahumma A'inniy 'Alaa Dhikrika Wa Shukrika Wa Husn 'Ibaadatik
“Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukukumbuka, na kukushukuru, na kukuabudu kuliko kuzuri kabisa"
Alikuwa Mtume صلى الله عليه وسلم ikimjia habari ya kufurahisha akisema:
الْحَمْـدُ للهِ الَّذي بِنِـعْمَتِهِ تَتِـمُّ الصّـالِحَات
Alhmduli-LLahi-lladhiy Bini'matihi Tatimmus-Swaalihaat
“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye kwa neema yake yanatimia mambo mema”
Na ikimjia habari ya kusikitisha husema:
الْحَمْـدُ للهِ على كُـلِّ حاَلٍ
Alhamdulillahi 'Alaa Kulli Haal
“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa hali zote”
Atakaye yasema haya kila asubuhi basi atakuwa ametekeleza shukurani ya siku nzima, na atakaye yasema jioni atakuwa ametekeleza shukurani ya usiku mzima.
اللّهُـمَّ ما أَصْبَـَحَ بي مِـنْ نِعْـمَةٍ أَو بِأَحَـدٍ مِـنْ خَلْـقِك ، فَمِـنْكَ وَحْـدَكَ لا شريكَ لَـك ، فَلَـكَ الْحَمْـدُ وَلَـكَ الشُّكْـر
Allaahumma Maa Aswbah-biy Min-Ni'matin Aw Bi-ahadin Min Khaliqik Faminka Wahdaka Laa Shariyka Laka, Falakal-hamdu Wa Lakas-shukr
“Ewe Mwenyezi Mungu sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe chako chochote na neema, ila inatoka kwako hali ya kuwa peke Yako huna Mshirika, ni Zako sifa njema na ni Zako shukurani"
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


