Tawassul - 4 Hoja Za Watetezi Wa Tawassul Zisizofaa Kisheria
Idara ya 'Da'awah, Habari, Utafiti, Tahariri Na Uandishi
Ansaar Muslim Youth Centre
Katika makala iliyopita tuliona hatari ya mtu kufanya jambo lililokua nje ya maadili ya Kiislam kwa kutegemea hoja batili vikiwemo visa vya uongo vilivyo simuliwa na wasiokua Waislam katika Mayahudi na Wakristo.
Hivi sasa watetezi wa tawassul zisizofaa wameanza kukiri kua ni kweli wanategemea Hadithi mbovu (dhaifu) lakini eti sio kila hadithi mbovu haitumiwi. Na wametoa ushahidi kwamba mbona Maimamu wakubwa wametoa hukmu juu ya baadhi ya mambo ya kisheria kwa kutegemea hadithi mbovu?
Maneno hayo hapo juu si sahihi na wala hayakubaliki kwa sababu ni jambo lenye kueleweka na kila mwanafunzi wa somo la Hadithi kua wanachuoni wote wanakubaliana kua Hadithi dhaifu haifai kuitolea dalilli au hoja katika mambo ya itikadi au hukmu za kisheria. Ikhtilafu iliyopo ni ile kauli kwamba je, inafaa kutegemea hadithi dhaifu katika matendo ya Fadhila? (Fadhaailul A’amaali)? Kuna wanachuoni wanaosema kua yafaa kutumia hadithi hizo na kuna wanaosema haifai. Kauli yenye nguvu ni kwamba haifai kutumia hadithi dhaifu kwa jambo lolote. (Rejea vitabu vifuatavyo kwa faida juu ya hayo tuliyoyataja: Tadriibur-raawiy juzuu ya 1 uk.268 – 299. Al – kifaya
Ama ile hoja inayotolewa na watetezi wa Bid’aa kua Maimamu wakubwa walitegemea hadithi dhaifu
Ni jambo lenye kueleweka na kila msomi wa somo la Hadithi kwamba kipindi walichokua wakiishi Maimamu wetu mashuhuri: Imam Abu Hanifa (r.a.) Imam Malik (r.a) Imam Shaafii (r.a.) na Imam Ahmad (r.a.) ilikua ni kipindi tayari mafunzo ya Mtume (s.a.w.) yalikua yameshaharibiwa. Maadui wa Uislam walikua tayari wameshatunga Hadithi nyingi za uongo na kusingizia kwamba ni maneno ya Mtume (s.a.w.) (Rejea makala yetu ya Al-Fikrul Islamiy Na. 34 kwa maelezo zaidi). Maimamu wote hao tuliowataja walikataa katakata kufuatwa tu kichwa mchunga kwani wao ni wanaadamu ambao sio maasuum (hawakulindwa kufanya makosa)
Imam Abu Hanifa (r.a.) amesema:-
“Itakaposihi Hadithi basi hiyo ndio madhehebu yangu”.
(Alhaashiyah Juzuu ya 1 uk. 63)
Imam Malik (r.a.) amesema:-
“Hakuna yeyote baada ya Mtume (s.a.w.) isipokua kauli yake huchukuliwa na kuachwa isipokua Mtume (s.a.w.)”
(Irshaadus Saalik Juzuu ya 1 uk. 227)
Imam Shaafii (r.a.) amesema:-
“Itakaposihi Hadithi basi hayo ndio madhehebu yangu”
(Al Majmuu Al Mussawwiy Juzuu ya 1
Na amesema kumwambia Imam Ahmad (r.a.):
“Nyinyi mnajua zaidi Hadithi na wapokezi kuliko Mimi. Basi ikiwa Hadithi sahihi nijulisheni, vyovyote iwavyo, (Iwe ipo mji wa) Kufa, au
(Adabu Shaafii uk. 94 Na 95).
Na amesema:-
“Kila jambo ambalo limesihi ndani yake habari toka kwa Mtume (s.a.w.) mbele ya watu (Wataalamu) wa upokezi, na (ikawa) kinyume na niliyoyasema, basi Mimi ninaliacha jambo
(Al – I’ilaamul Muwaqi'ina Juzuu ya2 uk. 363).
Imam Ahmad (r.a.) amesema:-
“Kufuata (kunakotakiwa) ni mtu kufuata aliyokuja nayo Mtume (s.a.w.), na toka kwa Maswahaba wake, kisha yeye baada ya taabiina ni mwenye khiyari”. (Masail Imam Ahmad uk. 276).
Na amesema:-
“Msinifuate mimi kichwa mchunga wala usimfuate kichwa mchunga Maliki, Shaafii, wala Awzaaiy wala Athawriy, na chukueni pale walipochukua wao”.
(I’ilamul Muwaqiina juzuu 2 uk. 302)
Pamoja na yote hayo tuliyoyataja katika kauli za Maimamu, watetezi wa Bid’aa na Tawassul zisizofaa kisheria wamejijengea kufuata tu Maimamu na Masheikh kichwa mchunga wanadai wao ni wafuasi wa Imam Shaafii (r.a.). Lakini ukiangalia matendo
“Na ama kusoma Qur’aan, ni mashuhuri toka Madhehebu ya (Imam) Shaafii kwamba thawabu zake hazimfikii maiti”. (Mwisho wa kunukulu).
Lakini kwa sababu hivi sasa baadhi ya walimu wamejitengenezea rizki kwa kuwasomea watu khitma, basi
Mfano mwingine wa uasi aliofanyiwa Imam Shaafii (r.a.) ni pale aliposema katika kitabu chake (Al-Ummu, Juzuu ya 1 uk. 317):
“Na ninapenda kwa jirani wa maiti au jamaa zake wa karibu kuwafanyia watu wa maiti chakula siku aliyokufa na usiku wake (kiasi cha) kuwashibisha, kwani hilo ni Sunnah na dhikri karimu, na ni katika tendo la watu wa kheri kabla yetu na baada yetu. Kwa sababu zilipokuja khabari za kifo cha Jaafar, Mtume wa Mwenyeezi Mungu (s.a.w.) alisema:-
“Wafanyieni ukoo wa Jaafar chakula kwani wamefikwa na jambo lenye kuwashughulisha”. (Mwisho wa kunukulu).
Maneno haya, ni Mashekhe na walimu wachache
Vile vile Imam Shaafii (r.a.) ni katika waliopinga matanga aliposema:-
“Na ninachukia matanga; nayo ni mkusanyiko wa watu (nyumbani kwa maiti) hata kama hawana kilio, kwani
Leo imekua kila kukifiwa utasikia kuna matanga ya jumla na matanga ndugu siku tatu hadi saba. Hakuna lifanywalo humo isipokua kusengenyana na kula ubwabwa. Na hatujasikia hayo yakikemewa, kwani ukiyakemea hayo utawaudhi watu na utakosa ubwabwa wa bure!
Basi hali ndio
Katika makala hii hii tutaendelea kukutajia hoja zinazotegemewa na watetezi wa Tawassul zisizofaa na zitajibiwa ipasavyo InshaAllah.
HOJA YA NNE:
Wanadai watetezi wa Tawassul zisizofaa kwamba Swahaba Ibn Umar alitawassal kwa jaha ya Mtume (s.a.w.)
Imepokewa kwa Al – Haytham bin Hanash akisema:-
“Tulikua kwa Abdullahi bin Umar (r.a) mguu wake ukashikwa na ganzi. Basi mtu mmoja akamwambia: “Mtaje mtu alie kipenzi zaidi kwako katika watu. Akasema (Ibn Umar) Ewe Muhammad; basi (hapo hapo) aliamka (ganzi ikatoka)
(Imepokewa na Ibn Sunniy).
Na kisa kingine ni
Imepokewa na Mujahid akisema:-
Ulipata ganzi mguu wa mtu mmoja mbele ya Ibn Abbaas (r.a.) (Swahaba). Ibn Abbaas Akamwambia (mtu huyo): taja alie kipenzi zaidi kwako katika watu. (Yule mtu) akasema: Muhammad (s.a.w.).
(Imepokewa na Ibn Sunniy).
Hadithi hizo mbili zimetumiwa na Sharifu Al-Malikiy katika kitabu chake Mafahim Yajib an Tuswahah
Hoja inayojengwa katika Hadithi mbili hizo hapo juu ni kwamba mtu akipatwa na tatizo katika kiwiliwili chake, basi ataondokwa tu atakapo Tawassall kwa jina la Mtume (s.a.w.) au atakapomwita kwa jina lake, na eti ndio maana Muislamu akijikungwaa au akipatwa na msiba husema Mtumeeee!! Au Muhammad! Au hammad! Basi msiba ule humuondokea na sio kwamba kwa kufanya hivyo ni kumuomba Muhammad (s.a.w.) lakini ni sawa na kumuomba Mungu kwa jaha ya Muhammad (s.a.w.). Vile vile wanayatia nguvu madai haya kwa sababu eti Hadithi hizo mbili zimetajwa na Sheikh Ibn Taymiya eti pia (gogo la wana-Sunnah) na kuzitolea ushahidi katika kitabu chake Al-Kalimu Attwayyib
JAWABU YA HOJA HIYO NI KAMA IFUATAVYO:-
Inashangaza kuona kwamba pamoja na kutangaza misimamo yetu kua sisi Ansaar hatuabudu Mashekhe
Na mwanafunzi yeyote mwenye kujiunga na Madarisi zao hupewa kitabu kinachoitwa ‘Taalimul Mutaallim’ katika kitabu hiki anafundishwa mwanafunzi jinsi ya kunyenyekea Mashekhe na kuwafanya wawe tayari hata kuegemewa na Mashekhe wao kama mito, kuwasimamia kila wanapowaona kuwapigia magoti bali sio Mashekhe tu bali hata watoto wa Mashekhe wanatakiwa wasimamiwe kwa heshima ya shekhe. Haya utayakuta katika kitabu tulichokitaja
“Na katika kumuheshimu (Shekhe) Ni kuwaheshimu wanawe na kila mwenye kutaalaqi (kuhusiana) nae, Na ilikua Ustadhi wetu Sheikhul Islaam Burhanuddin mwenye (kitabu cha Alhidaaya (r.a.) akisimulia mmoja katika wanachuoni wakubwa wa (Nchi ya)
Basi mafunzo
Katika hadithi nyingi tunaona jinsi Maswahaba walivyokua wakimuadhimisha Mtume (s.a.w.), kwani walipokua wakikaa mbele yake walikua watulivu, wanyenyekevu kana kwamba juu ya vichwa vyao kuna ndege. Lakini pamoja na kumuadhimisha kote huko, walikua nao, hawajathubutu kumuudhi Mtume (s.a.w.) kwa lile asilolipenda kufanyiwa, kwa mfano hata siku moja hawajawahi kumsimamia Mtume (s.a.w.) kwa kumuadhimisha kwa vile alinyowaelimisha kwamba kumsimamia mwanadamu mwenzio kwa madai ya kumuadhimisha hakufai, kwani hiyo ni njia ya kuwapelekea watu kufanya ushirikina wa kuwaabudu binadamu. Na ndio haya tunayoyaona leo. Na katika Hadithi alizotukataza Mtume (s.a.w.) kusimamia watu ni:-
“Yeyote anaependa watu wajimathilishe mbele yake wakiwa wamesimama (kwa kumuadhimisha) basi ajiandalie makazi yake motoni”.
Vile vile Swahaba Anas (r.a.) anaelezea hali waliyokua nayo Maswahaba na amesema:-
“Hakukuwa na mtu yeyote katika dunia ambae (Swahaba) walikua wanampenda zaidi kumuona kuliko Mtume wa Mwenyeezi Mungu (s.a.w.) na walikua hawamsimamii kwa kujua kwao kua Mtume (s.a.w.) analichukia
(Imepokewa na Bukhari katika Al-Adabul-Mufrad).
Haya basi tunaona Mtume (s.a.w.) ambae ndie anaestahiki kupewa heshima zote katika viumbe wa Mwenyeezi Mungu (S.W.) alikua akichukia kabisa kitendo hicho. Hata hivyo aliruhusu baadhi ya wakati kusimamiwa mgeni atokae mbali kwa nia ya kumpokea au aingie kwenye nyumba. Na ziko hadithi sahihi zenye muongozo huo, ispokua Ahlul Bid’aa kama kawaida
“Kusimama kwangu kwa ajili ya mtukufu wangu ni faradhi, na kuacha faradhi si jambo lilonyooka. Nimeona ajabu kwa yule mwenye akili na fahamu, anaona uzuri huu kisha akawa hasimami “. (Angalia kitabu ‘Aswaika’ uk. 32 chapa ya Tamta mwaka 1987).
Maneno hayo yanayosingiziwa kua ni ya Swahaba Hassan bin Thaabit (r.a.) mbali na kwamba ni maelezo yasiyokua na upokezi unaokubaliwa yanaonyesha wazi kupingana kwake na upokezi thabiti wa hadithi ya Anas (r.a.) iliyopokewa na Bukhari kwa sababu kwanza – Hassan atakua amewafanya Maswahaba wote kua ni watu wasiokua na akili wala fahamu. Kwani kwa maoni yake eti kumsimamia Mtume (s.a.w.) ni wajibu na wao hawakutekeleza wajibu huu, isipokua yeye tu. Kwa hiyo Maswahaba, kwa kutomsimamia Mtume (s.a.w.) watakua pia wamemvunjia heshima Mtume (s.a.w.).
Vile vile ushairi huu wa Hassan bin Thaabit ni kinyume cha wanavyoitakidi watetezi wa Bid’aa ambao wanaitakidi kwamba Mtume (s.a.w.) huhudhuria maulidini na ndio maana wao wanasimama pale anapohudhuria. Lakini pamoja na yote hayo, bado wanaitakidi kusimama ni jambo linalopendeza tu na si faradhi.
(Angalia kitabu cha Ziyadatu Lydhwaah uk.22 kilichochapishwa na Tamta).
Hivyo hata wao nao wamempinga Hasaan bin Thaabit (r.a.) juu ya hukmu aliyoitoa ya ufaradhi wa kumsimamia Mtume (s.a.w.). Basi hivi ndivyo ilivyo ndugu msomaji Sunnah sahihi ya Mtume (s.a.w.) inapothibiti, batili hujitenga na wenye kushikamana nayo hufedheheka.
Maelezo haya marefu tumeyaleta kutokana na kauli ya watetezi wa Bid’aa na Tawassul zisizofaa kutaja majina ya Mashekhe Fulani kua ni vigogo vyetu wakidhani kua sisi tunawafuata kichwa mchunga
Pili:
Ni kweli kwamba hadithi hizo tulizotaja hapo juu kuhusu kuondoa ganzi kwa Tawassul jaha ya jina la Mtume (s.a.w.) zimetajwa katika kitabu cha Ibn Taymiya (Alkalimu Attwayyib). Lakini hadithi hizo hazikubaliki kwa mujibu wa fani ya uchambuzi wa Hadithi na zimehesabiwa kua ni mbovu, kwa hiyo hazifai kutolea ushahidi wa jambo hata kama huyo alietaja ni Shekhe alievaa kilemba kirefu. Na inafahamika kwa kila mwanafunzi wa somo la Hadithi kwamba hao Maimamu wakubwa waliomtangulia Ibn Taymiya wametaja Mahadithi mabovu chungu nzima katika vitabu vyao vya Hadithi na vya Fiqhi, na haiwi kwa waliyoyasema kua ni hoja. Ndio maana tunaambiwa vitabu sahihi kuliko vyote ni Bukhari na Muslim ama vilivyobakia vinaeleweka wazi kua wamechanganya nzima na mbovu.
Sasa hebu tuzichambue zile hadithi mbili za ganzi tuone ubovu wake uko wapi. Riwaya ya kwanza imetolewa na Ibn Sunniy katika kitabu chake “Amalul Yawni wa Laylat” na ametaja wapokezi wa Hadithi. Na katika hao aliowataja ni Muhammad bin Mus’ab Alqaqusani. Huyu amehesabiwa kua ni dhaifu, hafai kutolewa ushahidi, kwani ni mwenye kughafilika mno na mwenye kuchanganya upokezi. Hivyo hivyo kuna mpokezi Al Haitham bin Hanash. Huyu nae ni (Majhulal ayni) Mtu asie julikana. Vile vile kuna Abu Is’haaq Assubaiiy. Huyu ni mwenye kufanya ‘Tadliis’ (Ghushi katika upokezi). Ama Hadithi ya pili vile vile imepokewa na Ibn Sunniy katika kitabu chake Amalil Yawmi wa Laylati, na ametaja wapokezi wa hadithi. Na katika aliowataja ni Ghayyaath bin Ibraahim. Huyu amehesabiwa kua ni muongo na khabithi.
Kwa kila (dosari) zilizotajwa hapo juu, hadithi hizo mbili hazikubaliwi wala hazina hoja yenye kutegemewa.
Tatu:
Isitoshe hata
Ahlul Bid’aa wal Hawaa ili ionekane kua hiyo ni aina ya Tawassul ya kutaja Mtume (s.a.w.) aliekufa au alie mbali ili kukidhi haja ya mtu.
Ni jambo lenye kueleweka kwa msomi yeyote kwamba hili la mtu kushikwa na ganzi ya mguu na kutaja jina la mtu ampendae sana ndipo ganzi hutoka ni katika itikadi za aina ya matibabu walizokua nazo Waarabu tangu zama za ujahilia (kabla ya kuja kwa Mtume (s.a.w.) na katika zama za uislam. Katika kitabu ‘Bulughul Irab cha Al-Aluusiy
Amesema Jamil Buthainah kumwambia mwanamke kipenzi chake:-
“Wewe ni kitulizo cha jicho langu wakati tukikutana,
Na utajo wako huniponya mguu wangu wakati unaposhika ganzi.
Na mwanamke nae Amesema:-
Unapokufa ganzi mguu wangu ninamwita Ibn Muswabi, basi
Nikisema: Abdullah – ganzi huondoka.
Na vile vile kauli ya Swahaba Abdullahi bin Umar kama ungethibiti upokezi wake, basi ingekua na maana ile ile kua alipopatwa na ganzi alimtaja Mtume (s.a.w.) sio kwa maana ya kutawassal, bali ni ile itikadi aliyokua nayo ambayo ndio tunayotakiwa Waislam wote tuwe nayo kwamba mtume (s.a.w.) anatakiwa awe kipenzi zaidi katika watu kuliko wazazi wetu wawili, watoto wetu au kuliko watu wote, hivyo atakua amemtaja kwa sababu hiyo, na kama angelikua sie Muislam kama vile Mkristo basi angelimtaja Yesu! Kwa hivyo hatuwezi kusema kua hao waliotajwa hapo juu waliondokewa na ganzi la mguu kwa kutawassal kwa majina ya vipenzi vyao hata wawe mahawara au watu waovu, hii itapelekea wapenzi wa Bob Marley na Michael Jackson kutawassal kwa jaha za watu hao pindi wakipatwa na majanga.
Na Waarabu walikua na itikadi ya matibabu sampuli hii, huenda ni kutokana na mtu kumtaja ampendae kunaongeza joto la Damu na kuifanya ipite kwa haraka zile sehemu zilizokufa ganzi, lakini hili linahitaji utafiti wa kielimu (kisayansi) kwani matibabu mengi ya kizamani yalikua ya kiitikadi tu yaliyorithiwa toka kwa mababu na sio ya majaribio ya kielimu (kisayansi) ni sawa na vile walivyokua wakiitakidi wazee wetu humu mwetu kwamba mtu akipaliwa wakati anakunywa maji basi kuna mtu aliembali anamtaja kwa ubaya wakati ule.
Kutegemea mahadithi mabovu Na itikadi zisizo sahihi ndiko kulikowafanya Waislam wengi leo humu mwetu wakipatwa na msiba au hata kujikungwaa kumtaja Mtume (s.a.w.) badala ya Mwenyeezi Mungu (S.W.) ni nadra sana kumsikia mtu akipatwa na janga kumtaja Mwenyeezi Mungu (S.W.) au sifa zake ilihali Mwenyeezi Mungu (S.W.) ametaka tumpende Yeye zaidi kuliko chochote kisha ndipo tumpende Mtume (s.a.w.) kuliko wanaadamu wote. Lakini watu wamempenda Mtume (s.a.w.) kuliko Mwenyeezi Mungu (S.W.) kiasi ambacho kukiwa Na mkusanyiko wa watu kama vile Muhadhara kukatokea mtu kumtukuza Mwenyeezi Mungu (S.W.), basi watu wa Bid’aa huchukia
“Enyi mlioamini mkumbukeni Mwenyeezi Mungu kwa wingi. Na mtukuzeni asubuhi na jioni”. (Al-Ahzaab /41-42)
UZINDUSHI KUHUSIANA NA MASINGIZIO KWAMBA ANSAAR HAWATAKI KUMSIFU NA KUMSWALIA MTUME (S.A.W.)
Ahlul Bid’aa wal Hawaa wanajaribu kuwadanganya watu kua sisi kwa kukumbusha watu utajo wa Mwenyeezi Mungu (S.W.) kwa wingi basi tunakua tunapinga Mtume (s.a.w.) asiswaliwe au asisifiwe. Tunataraji kua tuliwabainishia Waislam tofauti kati ya kumswalia Mtume (s.a.w.), kumsifu na kusherehekea mazazi yake (Angalia makala yetu Al-Fikrul Islamiy Na. 24) Tunachopinga ni sherehe za mazazi ya Mtume (s.a.w.) kwa sababu ni jambo lilozushwa katika dini tena na Mashia huko Misri (
Nimesema: Naam hakika katika kujikusanya watu kwa kusikiliza kisa cha mazazi ya Mtume (s.a.w.) ni jambo lilozushwa, halikuwepo zama za Utume bali halikudhihiri isipokua katika karne ya
Alhamdulillahi leo wamekiri watetezi wa Bid’aa waziwazi kwamba kujikusanya kwa ajili ya kusikiliza kisa cha mazazi ya Mtume (s.a.w.) ni jambo ambalo halikufanywa na Mtume (s.a.w.) wala Maswahaba, wala Taabiina bali watu wote walioishi karibu miaka mia saba baada ya kufa kwa Mtume (s.a.w.) wala hawakuliona bora, isipokua hao hao Mashia wanaowatukana Maswahaba wa Mtume (s.a.w.) ndio walioona jambo hilo ni bora na Ahlul Bid’aa wa zama zetu, kwa madai kwamba kwa kufanya hivyo ndio wanadhihirisha mapenzi na kumsifu kwao Mtume (s.a.w.), lakini ukiangalia hakika yao utagundua mara moja kua wao ndio maadui wa mwanzo wa mafunzo ya Bwana Mtume (s.a.w.).
Hebu mtu aende katika Mahospitali
Wanakwenda kufanya sherehe za kumsifu Mtume (s.a.w.) kwenye nyumba ya watu ambao ndio maadui wakubwa wa Mafunzo ya Mtume (s.a.w.), mtu ambae anauza Kaseti (kanda) za miziki ya Kitwaaghuuti (bela bela, kwasakwasa, Bongoman na zile zenye kuamsha hamasa za zinaa. Vipi mtu huyu atakua anampenda Mtume (s.a.w.)? Iwapo yule ambae hugeuza mita ya redio tu wakati ikisomwa Qur’aan akaweka muziki wa Kongo (
Mwenye kufanya au kusema moja katika haya ametoka katika Uislam… je, wamesahau makatazo na makemeo ya Mwenyeezi Mungu (S.W.) juu ya wale wenye kutangaza uovu, Aliposema:-
“Kwa yakini wale wanaopenda uenee uovu kwa wale walioamini, watapata adhabu iumizayo katika Dunia na Akhera….”
(An Nuur/ 19).
Basi hawa ndio watu wanaojidai wanampenda Mtume (s.a.w.) ilihali mafunzo yake wanayapiga vita kimatendo. Huu ni unafiki uliodhahiri, kwani Mwenyeezi Mungu (S.W.) amemleta Mtume wake ili atiiwe na kufuatwa kwa yote aliyokuja nayo.
Amesema Allah (S.W.):-
“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyeezi Mungu, basi nifuateni, (hapo) Mwenyeezi Mungu Atakupendeni na Atakusameheni madhambi yenu”. (Aali Imraan / 31).
Ndugu Muislam tutaendelea InshaAllah katika makala ijayo kukuletea hoja zinazotegemewa na watetezi wa Tawassul zisizofaa na za ushirikina na zitajibiwa ipasavyo.
|
MAKALA HII HUTOLEWA NA: IDARA YA DA’AWAH, HABARI, UTAFITI NA TAHARIRI ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTER STR. 19 S.L.B. 1542 SIMU 272646620
|
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
