Ni Nini Hadhi ya Mwanamke Katika Uislamu
Uislamu humwona mwanamke, akiwa, ama mseja au aliyeolewa, kwamba ni yu mpweke katika haki zake, akiwa na haki ya kumiliki na kutumia mali yake na mapato bila ya ulinzi wowote (iwe baba yake, mume au mwingine yeyote). Ana haki ya kununua na kuuza, kutoa hedaya na Sadaka, na anaweza kutumia mali yake katika namna anayoridhi. Mahari hutolewa na mchumba wa kiume na mchumba wa kike huyatumia kwa matumizi yake binafsi, na huyo mwanamke huendeleza jina la familia yake badala ya kuchukua lile la mume.
Akina mama huheshimiwa sana katika Uislamu. Uislamu unaelekeza kuamiliana nao katika njia bora. Mtu mmoja alikuja kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Ni nani miongoni mwa watu anayestahiki kwamba nimfanyie wema zaidi?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Mama yako.)) Yule mtu akasema: “Kisha nani?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: ((Kisha mama yako.)) Akauliza tena yule mtu: “Halafu nani?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu tena: ((Halafu mama yako)). Yule mtu akauliza kwa mara nyingine: “Halafu nani?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Halafu baba yako.)) [108]
(Tafadhali, tembelea www.islam-guide.com/pillars kwa ajili ya maelezo zaidi juu ya wanawake katika Uislamu.)
[107]Imesimuliwa katika kitabu cha Ibn Majah, Na. 1978, na At-Tirmidhiy, Na. 3895
[108]Imeandikwa katika Swahiyh Muslim, Na. 2548, na Swahiyh Al-Bukhaariy, Na. 5971
- Login or register to post comments
- Email this page


