Ni Nini Waislamu Wanachowafanyia Wazee
Katika ulimwengu wa kiislamu, ni mara chache mtu kukuta “nyumba ya makazi ya wazee.” Mkazo wa mtu kuwatunza wazazi katika kipindi hiki kigumu zaidi maishani mwao huchukulika kuwa ni heshima na baraka tena ni fursa kwa ajili ya kukua kukubwa kiroho. Katika Uislamu, inatosha tu kwamba tunawaombea wazazi wetu, lakini tunapaswa tuwafanyie huruma isiyo na ukomo, kwa kukumbuka wakati tulipokuwa watoto wadogo tusiomudu chochote, ilhali wao walitukhitari katika nafsi zao. Akina mama huwa na heshima ya namna ya pekee. Pindi wazazi wa Muislamu wanapofikia uzeeni, hufanyiwa huruma,ukarimu na kutokuwa na ubinafsi.
Katika Uislamu, mtu kuwakhudumia wazazi wake ni jukumu la pili baada ya Swalah, tena ni haki yao kutarajia hayo. Inachukulika kuwa ni jambo lenye kustahili dharau ikiwa watafanyiwa maudhi pindi ambapo hakuna kosa lolote kwa upande wao, wazee wanajikuta katika matata.
Mwenyezi Mungu Amesema: “Na Mola wako Mlezi Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyonilea utotoni.” (Qur-aan, 23-24)
- Login or register to post comments
- Email this page


