Skip navigation.
Home kabah

Tufufue Sunnah Ya Takbiyrah Iliyosahauliwa Katika Siku Zilizobakia Za Hajj

Tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyratul Muqayyad ambayo ni Takbiyrah inayotakiwa kusomwa kila baada ya Swalah za fardhi kuanzia siku ya 'Arafah kuanzia baada ya Swalaatul-Fajr hadi mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalah ya Alasiri ndio kumalizika kwake. Kufanya hivyo haikuchukui hata dakika 2. Na inapasa kuwakumbusha ndugu wengine ili kila mmoja apate thawabu za kuifufua Sunnah hii ambayo wengi wameiacha. Thawabu hizo zitazidi kuongozeka kwa yule atakayeanza kumfunza mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kufunzwa: Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 

  ((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً .... )) أخرجه مسلم في صحيحه

((Atakayefanya kitendo chema  katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake  bila ya kupungukiwa thawabu zao chochcte…)) [Muslim]

 

Inavyopasa kufanya Takbiyrah baada ya kutoa salaam ni hivi:

 

  الله أكبر. الله أكبر. لا إله إلا الله. والله أكبر. الله أكبر ولله الحمد

"Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Laa Ilaha Illa Allaah Wa-Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Walillahil-hamd 



Sikiliza Takbiyrah Za 'Iyd