029 Yanayotengua Wudhuu - 4
6- Kati ya yanayotengua wudhuu ni kula nyama ya ngamia
Aliyekula nyama ya ngamia sawasawa ikiwa mbichi, iliyopikwa au ya kuchoma, ni lazima atawadhe. Hii ni kwa Hadiyth ya Jaabir bin Samrah anayesema kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, tutawadhe kwa kula nyama ya kondoo au mbuzi?” Akamjibu:
((إن شئت توضأ، وإن شئت فلا تتوضأ))
((Ukitaka tawadha, ukitaka usitawadhe)).
Akamuuliza: “Je, tutawadhe kwa kula nyama ya ngamia?” Akasema:
((نعم، توضأ من لحوم الابل))
((Ndiyo, tawadha ukila nyama ya ngamia)). ([1])
Na imepokelewa toka kwa Al-Barra bin ‘Aazib kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((((توضأوا من لحوم الابل، ولا توضأوا من لحوم الغنم
((Tawadheni kwa kula nyama ya ngamia, na wala msitawadhe kwa kula nyama ya kondoo na mbuzi)).([2])
Na haya ni madhehebu ya Ahmad, Is-haaq, Abu Khaythamah, Ibn Al-Mundhir na Ibn Hazm. Pia ni moja kati ya kauli mbili za Ash-Shaafi’iy na ni chaguo la Shaykh wa Uislamu. Aidha, ni kauli iliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Umar na Jaabir bin Samrah.
Lakini Jamhuri ya Maulamaa kama Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ath-Thawriy na kundi la watangu wema, hawa wanaona kwamba si lazima kutawadha kwa kula nyama ya ngamia bali ni Sunnah([3]) kutokana na Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Amri mbili za mwisho toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kutotawadha kwa kile kilichoguswa na moto (kilichopikwa)”.([4]) Wakiizungumzia kauli hii wamesema: “Neno lake “kile kilichoguswa na moto” linakusanya nyama ya ngamia vilevile, nayo imethibiti kunasikhiwa”.
Hili linajibiwa kwa mambo mawili:([5])
La kwanza:
Ni kwamba Hadiyth ya Jaabir ni jumuishi, na yale yaliyopokelewa katika kutenguka wudhuu kwa kula nyama ya ngamia ni hali maalumu. Na jambo jumuishi hubebeshwa juu ya jambo maalumu, na hapo hutoka lile ambalo limethibitishwa na dalili kulifanya ni maalumu. Na hapa naskhi haizungumziwi kwa vile inawezekana kukusanya.
La pili:
Amri iliyokuja kuamuru kutawadha kwa kula nyama ya ngamia, bila shaka ni hukumu inayohusiana na kilichopikwa au kibichi. Kwa hiyo kuguswa na moto hakuwajibishi kutawadha, na kwa hivyo hukumu yake inakuwa nje ya habari zilizokuja kuhusu kutawadha kwa kula kilichopikwa na kwa ku-naskh wudhuu.
Baadhi
LENYE NGUVU
Ni kuwa ni lazima kutawadha kwa kula nyama ya ngamia kwa hali yoyote ile. Na kwa ajili hiyo, An-Nawawiy katika kitabu cha “Sharh Al-Muslim” (1/328) anasema: Madhehebu haya yana nguvu zaidi ingawa Jamhuri ya Maulamaa wako kinyume nayo.
TANBIHI
Ya kwanza:
Katika “Sharh Al-Muslim” (1/328), An-Nawawiy ameinasibisha kauli ya kutolazimu kutawadha kwa kula nyama ya ngamia kwa Makhalifa Wanne Waongofu!! Madai haya hayana dalili yoyote wala haijulikani sanadi yoyote kwao inayohusiana na
Ya pili:
KISA MASHUHURI CHA UZUSHI([8])
Kimetangaa baina ya watu wa kawaida kisa wanachokihadithia mara kwa mara. Kisa hiki wamekisikia toka kwa wanafunzi wanaoeleza kwamba ni lazima kutawadha kwa kula nyama na ngamia. Kisa hiki kinaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa katika kundi la Maswahaba wake, akasikia harufu (ya upepo) kwa mmoja wao. Swahaba huyo akaona hayaa kunyanyuka kati ya watu (kwenda kutawadha) naye alikuwa amekula nyama ya ngamia. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
((من أكل لحم جزور فليتوضأ))
((Aliyekula nyama ya ngamia akatawadhe)).
Hapo wote waliokuwa wamekula ngamia wakanyanyuka wakatawadha!!
Kisa hiki ni dhaifu kwa upande wa sanadi na munkari kwa upande wa matini.
- Login or register to post comments
- Email this page


