Wa Kulaumiwa Ni Nani?
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Wa Kulaumiwa Ni Nani?
Amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) tumeziacha nyuma ya migongo yetu na kuyafanya matashi yetu kuwa ndio muongozo wa maisha yetu.
Uzinifu tumeufanya kuwa ni ada yetu na pombe ndio muongozo wa maisha ya leo. Imefika hadi ya kuona haramu kuwa halali na halali kuwa ni haramu. Tumejikubalisha kuwa akiba haina faida bila ya riba. Mauziano yasiyokuwa na uongo, utapeli sasa yamepitwa na wakati.
Imekuwa ni desturi kuona kila kona za majengo na sehemu za mikusanyiko ya watu pamoja na barabarani kuwepo picha za utupu zenye kuamsha hisia za uzinifu. Sio matangazo ya biashara halali wala haramu zenye uadilifu wa kutilia mkazo ubinaadamu na haki za imani zisiopendelea picha hizo.
Matangazo ya pombe yameshika kasi huku simu, sigara, vyakula na kadhalika vikiwa havipo nyuma kurusha mabomu ya uzinifu.
Matokeo yake hayo, ni kubakia jamii kwenye matatizo na udhaifu wa mwaadamu wa uchu wa kutosheleza hisia zake kwa kujamiiana tu. Utakuta kwa mfano tangazo la simu lenye msichana aliyevaa jeans yenye kubana akiwa na mvulana aliyesokota nywele zake kwa mtindo wa rasta. Huku ujumbe wa tangazo
“Leo nitakosa masomo, nahitaji kupunga upepo”.
Nini tunawafunza vijana wetu kwa matangazo
Alhamdulillaah, tumepewa macho lakini hakika atakayeyakemea mambo hayo kwa sauti kali ndio ataambiwa kuwa ni kipofu, mpinga maendeleo, mjinga, hafai katika jamii, mshamba na kadhalika. Wale Waislamu wenye imani zisizoeleweka, ndio wataanza kumuita kwa istihzai na kejeli; Ustadh, Shaykh na kadhalika.
Tuikumbuke kauli ya Mola (Subhaanahu wa Ta’ala) Aliposema kuwa tuna viungo lakini hatuvitumii:
{{Na Tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni
Yote yametokana na wigo wa kuwaiga wasio kuwa Waislamu na kuanza kidogo kidogo kufuata tabia na vitendo vyao. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim
Na sasa yamedhihirika kwa upeo wa macho yetu ukweli wa Hadiyth hiyo. Kwani sisi Waislamu ni wakosa kutokana na unafiki wetu wa kuacha kanuni za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kukubali hayo matendo na picha hizo kuanzia majumbani mwetu hadi kwenye ardhi zetu. Zile harakati za kuanzisha taifa la Kiislamu ni budi kuzifuta kabisa kwa sasa au kwa uchache kuzisimamisha kwanza hadi tuanze kusimamisha hizo serikali kwenye nafsi zetu kwanza na familia zetu, kwani hatujawa tayari hata kuanzisha hilo taifa la Kiislamu ndani ya nafsi yetu au familia zetu. Hatuwezi hata kuvaa mavazi au kujiweka katika mtazamo wa Kiislam katika miili yetu kwa kuona aibu au kuogopa kupachikwa sifa na majina kadhaa, vipi tutaweza kusimamisha taifa hilo na hali wenyewe hatujawa tayari? Hata idhaa zenye muelekeo wa Kiislamu zimekuwa zikichanganya ala za muziki na kudhani kuwa ni halali. Je, ni bora kubaki kwenye shaka au kule ambapo hakuna shaka?
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



Assalam Alykkum Shukrani
Assalam Alykkum
Shukrani zote zimwendee Allah(Subhannah wataallah) na twamtakia rehma na amani mtume wetu Muhammad(swalla llwahu alay wassallam)
Napenda kama muislam kutoa maoni yafuatayo nadhani yatakuwa ni katika kuboresha ufanisi wa kazi hii ambayo kwa hakika mwenyezi Mungu awalipe hapa duniani na akhera mkifika!Maoni yahusu mpango wa maswali na namna yanavyojibiwa,nashukuru twajifunza mengi humo ila si vibaya naonelea kungekuwa na mpango wa kuyaweka maswali mapya kwenye sehemu yake tofauti na yaendelee kuwepo kwenye vipengele vyake kama kawaida,hii ina faida gani kwa ninavyoona mimi inasaidia kwa wale tulioweka malengo ya kusoma maswali yakaisha tuweze kujielimisha kufikia maalengo kwasababu kama nitakuwa nimesoma swali japokuwa linajionyesha limesomwa ila naweza jua kama nimebakiza idadi ya maswali mangapi kumaliza kipengele fulani,ILA kama utaratibu huu kwa namna yoyote ile unaweza kuharibu privacy ya watu waulizao maswali yao basi ni sahihi pia kutozingatiwa.Kingine kuna websites pia za kiislam zipo kwa lugha ya kiingereza si mbaya mkafanya mpango kuziangalia kwa faida ya wote maana kuna zingine yawezekana twazitembelea ila mafundisho yako tofauti na mtume Muhammad(swalla llah allayh wassalam) au yawezekana zapandikizwa na makafiri kwa minajili ya mipango ya muda mrefu kama wanavyoakaa na kupanga kupotea kabisa mafundisho ya dini Allah(subhannahu wataalah).Kwahiyo kama mtazijua au mtapata habari kuhusiana nazo mwaweza ziorodhesha pia na Allah atawalipa kwa kuyadhihirisha yaliyo maovu!
Pia nilitaka kusahau kama yawezekana pia mpango wa mawaidha yale yanayoweza kusikilizwa kwa mtindo wa mp3 nayo kama yanaweza kupangwa pia kwa namna ya alphabetical order kulingana na mada inayozungumziwa si vibaya ingawa kwa namna ya watoa khutba nayo yaridhisha ila yakupa muda mrefu kutafuta kile unachokitaka kwa muda huo kwa kuwa yawezekana huyo mkhutubu hana unachokitaka katika files zake ili uweze kuzidownload!
Mwisho nawatakieni afya njema na muendelee kutupa habari kuhusiana na uislamu kama ilivyoandikwa na Quran na Sunnah!
Hayo ni katika maoni tu na yakipatikana mengine yatawasilishwa kwenu Inshaallah na ningeomba kuwe na sehemu ya maoni kama haya maana nimejitahidi kuitafuta ingawa si kwa kina sana nimekuja gundua nimeandika si pake muda umeshakwenda sana!
Assallam Alykum
Assalaamu 'alaykum Tafadhali
Assalaamu 'alaykum
Tafadhali tuma maoni yako kupitia webmaster@alhidaaya.com kwani hii sio sehemu ya kuweka maoni na hizi makala kila wiki zinabadalika hivyo haya maoni nayo huondooka hapa.
Tutakujibu kuhusu maoni yako pindi ukituma kabla ya kuondoshwa hii makala.
Tunaomba ushirikiano wenu katika kutumia hizi nafasi na mawasiliano kupitia anuani zake zipasavyo.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA