Skip navigation.
Home kabah

Umuhimu Wa Zakaah - 5: Zakaah Ya Fedha Taslimu

 

Abu ‘Ammaar

Zakaah Ya Fedha Taslimu

Fedha taslimu hutolewa Zakaah endapo zitakuwa zimetimiza masharti ya kuwajibika.

Fedha hizi ziwe zinamilikiwa na mwenye kutoa Zakaah kama anazo mwenyewe au ameziweka Benki, ameazima au kukopesha. Katika hali zote fedha hizi bado zitakuwa katika milki yake.

Ikiwa ni fedha ambazo amezirithi na kupita Nisaab na tayari kuwepo nazo kwa zaidi ya Hawl (mwaka [wa Kiislam]) nazo pia zinaingia katika hukumu ya kutolewa Zakaah.

Ikiwa mwenye kumiliki fedha taslimu atakuwa na kiwango cha fedha zinazofikia kiwango wakati wa kuanza mwaka wake wa Zakaah basi chochote kitakachoongezeka baada ya hapo katika mali kitaingizwa katika hesabu ya Zakaah ya mwaka ule kama mshahara, faida, urithi, msaada na kadhalika. Ikiwa kama vitabakia hadi mwisho wa mwaka wa Zakaah. Kama vitatumika ndani ya mwaka wa Zakaah basi havitoingizwa katika hesabu ya Zakaah.

Hata hivyo kitakachoongezeka kiwe kinaenda sambamba na mtaji au fedha iliyopo. Ama kikitokana na mbinu nyengine mbali na mtaji au fedha zilizopo Hawl yake itaweza kutofautiana kwani zitaanza kuhesabiwa pale zilipoanza kumilikiwa umilikaji kamili. Ingawa kisheria inaruhusika kama zitajumuishwa na mali iliyopo na kutolewa Zakaah kabla ya muda wake.

Mifano:

1       Nilikuwa na £10,000.00 na nikazifanyia biashara katika Hawl na mwisho wa Hawl zilifikia £15,000.00, nitawajibika kuzitolea zote kwani zimetokana na mtaji uliopo.

 

2       Nilikuwa na £10,000.00 na kati kati ya Hawl nikarithi £5,000.00, nitawajibika kuzitolea £10,000.00 na hizi za ziada nisubiri mpaka ifikie Hawl yake. Ila kama nitazitolea mapema (in advance) inaruhusika na hivyo nitaweza kuzitolea zote £15,000.00 kwa sababu fedha iliyopo na iliyopatikana zimetoka katika njia tofauti.

 

3       Kila nikipokea mshahara hujiwekea akiba £200.00 au £300.00, miezi mengine sipati cha kuweka.. Kisheria ninaweza kuzitoa kiwango chote cha akiba katika hawl niliyojiwekea au kupata usumbufu wa kuzitolea kila zilizowekwa akiba Zakaah yake zikitimia Hawl yake.

 

Kiwango cha mwanzo kutolewa katika fedha taslimu ni kiasi cha thamani ya gramu 85 za dhahabu (safi na mpya) au gramu 595 za fedha kwa mujibu wa nchi aliyepo mwenye kutaka kutoa Zakaah.

Na hutolewa 2.5 % au robo ya fungu la kumi.

 

MASHARTI YA ZIADA YA KUZINGATIA

1       Fedha hizi ziwe ziada ya mahitaji yake ya lazima.

 

2       Zisiwe deni ambalo amekopa na kama akililipa hatobakiwa na ziada yoyote ya mali (Ama ikiwa deni hata likilipwa bado mali iliyobaki haitopungua chini ya Nisaab basi mali iliyobaki hutolewa Zakaah baada ya kutoa gharama za deni).

 

3       Isiwe fedha hizi zimepatikana kwa njia ya haramu (tutalifafanua kwa urefu)

Mfano:

Ni mfanyakazi niliyeajiriwa (Mfano huu kwa muajiriwa aliye Uingereza):

 

MAPATO

 

Kwa mwaka mzima

Pauni

1

Mshahara

 15,000.00

2

Tax Credit          

   3,000.00     

3

Child Benefit          

   1,500.00

4

Tax Refund

      250.00

5

Nina nyumba nimekodisha

   1,000.00

6

Bonus

      300.00

7

Pesa iliyokuwepo Benki

   3,000.00

 

JUMLA

 24,050.00

 

 

MATUMIZI

 

 

 

1

Matumizi*  kwa mwaka mzima  

11,000.00

 

2

Deni ninadaiwa na nililipa        

  1,000.00

 

JUMLA

12,000.00

 

*Matumizi yanajumuisha chakula, kodi ya nyumba, matumizi ya mafuta (gari) kwa usafiri na gharama za kutengenezea na kadhalika.

 

KIWANGO KITAKACHOBAKI NI MAPATO - MATUMIZI

24,050.00 – 12,000.00 = 12,050.00

Kiwango hiki kitakachobaki tukitoa matumizi yote ndicho nitakachopaswa kukitolea Zakaah mwisho mwa Hawl.

12,050.00 × 0.025 = £301.25

Nitapaswa kutoa Zakaah £301.25

 

 

Itaendelea inshaAllaah…