Skip navigation.
Home kabah

Du'aa Gani Kusoma Ili Upate Kumuota Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?

 

SWALI:

Poleni na kazi ya kutuelimisha na kutuelekeza katika njia ya ALLAH Inshaalah malipo mtayakuta kesho akhera. swali langu Kuna dua yeyote ya kusoma ili kumuota katika ndoto Mtume Muhammad S.W.A? 

shukran 



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Hakika ni kuwa hakuna du'aa yoyote ya kusoma ili umuote katika ndoto Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ili kufanikiwa kupata hadhi hiyo inabidi ujikurubishe sana kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kufanya Ibaadah na kufuata Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wingi na kumswalia kila mara pia na kujiepusha na maasi na uzushi.

Ifahamike kuwa anayemuota Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huwa amemuota kweli kwani shetani hawezi kujifananisha naye. Hii ni kutokana na kauli yake:

(((من رآني في المنام فقد رآني حقاً فإن الشيطان لا يتمثل بي))  البخاري  ومسلم  

((Atakayeniona katika ndoto basi hakika ameniona [ameniota] kwani shaytwaan hanifafanishi)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na Allaah Anajua zaidi