Kuamini Wanga – Je, Wapo Kweli Na Vipi Kujikinga Nao?

 

Kuamini Wanga – Je, Wapo Kweli Na Vipi Kujikinga Nao?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ama baada ya salamu, kuna hizi issue za mambo ya wanga. Je una weza kuni tafutia au kuniulizia ni mfululizo wa dua zipi au nyiradi zipi za kusoma kama zindiko au kinga juu ya hawa viumbe wanga wasiwe wanacheza ngoma zao eneo lako na wala kuja kukusumbua nyumbani kwako. In fact haya mambo nayasikia lakini ni vizuri kujua kama kuna vitu kama hivyo.

 

Je kwa watu wenye majini eiza wa kheri au wabaya, ni vitu gani na gani una wafanyia ili kuwapunguzia matatizo hayo. Kwani ina onyesha ni jinsi gani wanavyo teseka wakati wanapojiwa na hao viumbe.

 

Nita shukuru sana kama uta nipatia aidha ushauri au hizo nyiradi ili niwe najaribu kupitia kama kujua tuu ili niweze kuwasaidia watu wenye vitu kama hivyo. Ni vizuri kutumia vitu kutoka kwenye Qur an na ndivyo hasa ninvyo viulizia na sio kutoka kwa waganga.

Wako katika kujifunza

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hakika ni kuwa swali kama limekaririwa mara nyingi na kila wakati linakuwa ni lenye kuulizwa kwa njia nyingine. Ni vyema tuelewe kuwa watu huwa wanasumbua watu kwa njia moja au nyingine au mazingaombwe au uchawi au kwa njia nyingine zozote zilizokuwa zikitumika hapo zamani na pia sasa.

 

Muislamu anafaa ajilinde na vitu hivyo kwa kuwa ni mwenye kusoma kila wakati baadhi ya Aayah au Suwrah na du’aa alizotufundisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni kama zifuatazo:

  1. Al-Faatihah (Suwrah ya kwanza).
  2. Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
  3. Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
  4. Suwrah At-Tawbah (9: 129 mara saba).
  5. Al-Israa’ (17: 110 – 111).
  6. Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
  7. Al-Hashr (59: 22 – 24).
  8. Al-Kaafiruun (109).
  9. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).

La muhimu zaidi ni kujikinga kwa Nyiradi za Asubuhi na Jioni ambazo hakika ni kinga kubwa ya Muislamu na kila shari za kila siku. Nyiradi hizo zisomwe kwa mfululizo bila ya kuachwa. Wengi waliokumbwa na shari kama hizo wameweza kutibika na kujikinga kwa kufuata hizi nyiradi ambazo zinapatikana katika kitabu kifuatacho:

 

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

 

Na hasa dua ifuatayo:

 

128-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuzuia Vitimbi Vya Mashaytwaan

 

 

Ama kumsomea mwengine inafaa usome Aayah zifuatazo:

 

Mwanzo unaanza na A’udhu Billaahi Minash Shaytwaanir Rajiym.

  1. Al-Faatihah (Suwrah ya kwanza).
  2. Al-Baqarah (Aayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
  3. Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
  4. Suwrah al-A‘raaf (7: 54 – 56, 117 - 122).
  5. Yuunus (10: 81 – 82).
  6. Twaahaa (20: 69).
  7. Al-Hajj (22: 19 – 22).
  8. Al-Muuminuun (23: 115 – 118).
  9. An-Naml (27: 30 – 31).
  10.  Asw-Swaafaat (37: 1 – 10).
  11.  Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
  12.  Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
  13.  Al-Fat-h (48: 29).
  14.  Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
  15.  Al-Hashr (59: 21- 24).
  16.  Al-Jinn (72: 1 – 9,
  17.  Al-Buruuj (85).
  18.  Az-Zilzalah (99).
  19.  Al-Humazah (104).
  20.  Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas.
  21.  

Ama unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umesitiri sehemu zako zinazotakiwa kustiriwa.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share