Kuweka Urari Baina Ya Kazini Na Nyumbani
(Na Dkt Aisha Hamdan)
Imefasiriwa na Shaibu H. Kifea
Katika zama za leo, tunashuhudiya wanawake wakizidi kuingiya katika ulimwengu wa kazi. Wakati mwingine bila ulazima na wakati ni kwa sababu ya mwanamke kuhitajika kutowa mchango wake katika jamii na kutumiya elimu na ujuzi wake.
Kwa baadhi ya watu suwala la mwanamke kufanya kazi hutokana na utashi tu wa wanandowa, wazazi au wanafamiliya. Kwa wengine suwala hili hutokana na msukumo wa kiuchumi hasa kwa sababu ya shida na matatizo.
Vyovyote iwavyo, ukweli ni kwamba idadi kubwa ya wanawake wa Kiislamu wako makazini. Na wakati huwo huwo wengi miyongoni mwao wanakabiliwa na majukujukumu ya ulezi na usimamizi wa nyumba.
Wanawezaje kumudu yote haya? Wanawezaje kuweka mizani sawa baina ya kazini na nyumbani? Ni ni yepi mashauri bora kwa mwanamke na familiya yake?
Wanawake wa Kiislamu katika sehemu nyingi duniyani wanapandikizwa kasumba ya kuamini kuwa ili wawe na thamani basi lazima wawe na makazini. Yaani watoke majumbani.
Hii , yadaiwa, ni sehemu ya harakati za “ukombozi wa wanawake.”zinazotiwa nguvu na Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ulimwenguni kote.
Harakati hizi zimekuwa na athari kadha wa kadha ambazo zinadhihika. Wanawake huwamuwa kukawiza au kuacha kabisa maisha ya ndowa ili kuweza kushughulika na elimu na kazi. Wengine nao wamejiamuliya kuwa hata ikibidi kuolewa basi watazaa watoto wachache tu.
Hawatafikiriya hata kidogo kuwa na watoto kumi au kumi mbili kama walivyozaa mama zao!
Wapo wengine wanaotaabika kwa matatizo ya kihisiya na kimwili kwa kujaribu kushindana na ulimwengu wa wanaume.
Jambo ambalo wanawake wanapaswa kulielewa ni kuwa hakuna ubaya wao kuelimika na kujiendeleza kwa njiya ya kufanya kazi, lakini wasipuuziye wajibu wao muhimu wa kimaumbile-uzazi.
Wakati ambapo yaweza kulazimu baadhi ya wanawake kufanya kazi nnje ya majumba yao, lakini kama inawezekana hasa hasa kwa wanawake wenye watoto wadogo basi wangebaki nyumbani.
Hii ingekuwa njiya bora zaidi kwa wanawake na watoto. Watoto wana mahitaji mengi ambayo hukidhiwa vema zaidi na mama zao. Uzazi ni kazi inayostahiki ujira mkubwa.
Kwa kinamama wasio na njiya nyingine, basi nukta zifuwatazo zaweza kuwasaidiya:
1. Jaribuni kuangaliya kazi zinazoendana na sifa za kimaumbile za mwanamke. Zisiwe kazi za ushindani na zisiwe za sulubu. Kujaribu kushindana kwa kazi zinaswihi zaidi kwa wanaume kwaweza kuwa na athari mbaya kwa wanawake. Hili, matokeo yake, huweza kuathiri familiya.
Wanawake wanaofanya kazi katika sehemu zenye wanaume wengi hulazimika kuwapamoja na wanaume jambo ambalo huongeza vishawishi kati ya jinsiya hizo mbili.
Kazi za kufundisha (uwalimu), huduma za jamii, uuguzi na utunzaji watoto ni mifano ya kazi zinazofaa zaidi kwa umbile la mwanamke. Aina hizi za kazi hushajiisha sifa za kimaumbile za mwanamke na kutowa wasaa baina ya nyumbani na kazini. Aidha zinatowa mchango muhimu kwa jamii.
2. Tafuteni kazi zinazotowa wasaa zaidi kwa upangaji wa ratiba na saa. Uwalimu ni mfano mzuri wa kazi hizo kwani ratiba ya mama na ya watoto ni moja. Kazi ya muda maalum ingefaa zaidi kuliko kazi ya muda wote kama inawezekana kufanya hivyo. Baadhi ya makampuni huwa na programu kwa waajiriwa wenye familiya. Kujifanyiya kazi au biyashara nako kungelikuwa njiya nyingine bora kwa wanawake.
3. Tufuteni mtu wa kuaminika kwa kazi ya kutunza watoto, hasahasa binti wa Kiislamu au ndugu wa karibu wa kifamiliya. Watoto huweza kuzoweyana na watu wengi kwa kulelewa vizuri na kupendwa.
Dada wa Kiislamu au ndugu wa kifamiliya anaweza kuwa mama wa pili kwa watoto jambo ambalo linaweza kumpunguziya mtoto adha ya kuwa mbali na mama na athari za kuisha peke yake.
Malezi ya watoto nyumbani ni bora zaidi kwa watoto wadogo. Watoto wakubwa wao wanaweza kulelewa katika vituo vya kutwa au katika shulu za awali.
4. Tumiya muda mzuri kukaa na watoto nyumbani. Watoto wanahitaji muda na uwangalizi zaidi kuliko kitu kingine chochote lakini muda wa mama afanyaye kazi ni mchache.
Pale mama anapokuwa na wanawe, anapaswa kuwaangaliya na kufurahi nao kwa michezo na kwa kusoma. Muda wa kufaa ni muhimu kuliko muda mwingi.
5. Panga kazi za usafi wa nyumba na upishi ikiwezekana. Sulubu kubwa kwa kina mama ni ile ya kufanya kazi kutwa nzima na kurudi jiyoni kuwanza kupika na kufanya usafi. Hili nalo linapunguza zaidi wasaa wa kukaa na familiya.
Ufumbuzi bora zaidi ni kupata msaididzi wa kazi za ndani. Kwa kufanya hivyo wasaa wa mama kuwaangaliya watoto utakuwepo. Kwa mujibu wa Shariya mwanamama afanyaye kazi ana haki ya kupata usaidizi huu.
Jambo muhimu kwa wanawake kuzingatiya ni kuwa familiya ndiyo iwe kipaumbele chao.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


