Skip navigation.
Home kabah

Tofauti Ya Nashiyd Na Nyimbo – Nashiyd Zinafaa?

 

SWALI:

 

NAOMBA KUJUA NINI TOFAUTI KATI YA HIZI NASHEED NA NYIMBO, NA KAMA NASHEED NI HALALI NAOMBA DALILI KATIKA QURAN NA SUNNAH NA MSIMAMO WA MAULAMAA, JAZAKUM LLAAH KHER



 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mas-ala ya nyimbo na Nashiyd. Hakika hili ni suala ambalo limetatiza wengi miongoni mwetu nasi hapa tutajitahidi kukuelimisha kuhusu hayo.

Nashiyd ni neno la Kiarabu ambalo lina maana ya wimbo (nyimbo), imba, wimbo wa taifa, wimbo wa kidini. Kwa maana hizi tunapata kuwa hakuna tofauti wa nyimbo na nashiyd kimaana, ila Nashiyd zimezoeleka kuwa ni nyimbo za Dini zaidi lakini si kimaana.

Kwa hiyo, msingi wa Kiislamu katika nyimbo au Nashiyd ni lazima ufuatwe. Nyimbo au Nashiyd inaweza kukubalika au kukatazwa Kiislamu kutegemea mambo kadhaa. Ikiwa itakwenda sambamba na maadili ya Kiislamu itakubaliwa na kukataliwa ikienda kinyume na Uislamu.

Katika masharti ambayo yanafaa yatekelezwe ili kuifanya nyimbo au Nashiyd ikubalike ni kama yafuatayo:

  1. Kusiwe na ala za muziki zilizokatazwa na sheria kama mazumari, magoma na kadhalika. Ala inayoruhusiwa kwa wanawake na watoto ni matwari (dufu) tu.
  2. Ujumbe unaotoka katika nyimbo usiende kinyume na sheria. Isiwe ni nyimbo za matusi, kusifu mambo machafu kama zinaa au dhambi nyingine yoyote. Allaah Aliyetukuka Anasema: "Na katika watu wako wanaohitari maneno ya upuuzi ili wawapoteze watu na njia ya Allaah, pasipo wao kujua lolote, na wanaichezea shere hiyo njia ya Allaah" (31: 6).

Twatumai kuwa haya yatatupatia mwangaza wa kutosha katika suala hili.

Na pata ufahamu zaidi wa masuala haya kwenye jibu lifuatalo:

Nashiyd, Qaswiydah Na Hukmu Zake

 

Na Allaah Anajua zaidi