Mambo Matano Uwezayo Kuwafanyia Wazazi Waliofariki Kama Kwamba Wako Hai –2
Tunaendelea kumalizia mambo matatu mengineyo ya kuwafanyia wazazi waliofariki
3. Kuwalipa deni au ahadi zao:
Deni la Swawm:
Kuwalipia deni la Swawm ikiwa ni la fardhi (Ramadhaan) au Swawm ya nadhiri au ya kafara. Ama ikiwa amefariki kabla ya kumalizika Ramadhaan na amewahi kufunga siku za nyuma, hakuna haja kumlipia.
عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال :جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه و سلم فقال : يا رسول الله إن أمي ماتت، و عليها صوم شهر أفأقضيه عنها ؟ قال : (( لو كان على أمك دين أكنت قاضيه عنها ؟)) قال : نعم. قال: (( فدين الله أحق أن يُقضى)) البخاري و مسلم
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ambaye amesema: Alikuja mtu kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, Mama yangu amefariki naye ameacha deni la mwezi la Swawm, je nimlipie [nifunge kwa ajili yake]? Akasema: ((Je angelikuwa mama yako ana deni [la fedha] ungelimlipia?)) Akajibu: Ndio. Akasema ((Basi deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika Hadiyth:
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسول الله صلى الله عليه و سلّم: ((من مات و عليه صيامٌ صام عنه وليُّه)) البخاري و مسلم
Kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyefariki akiwa na [deni la] Swawm, walii wake amfungie)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Kuwafanyia Hajj:
عن ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، فَقَالَتْ : إِنَّ أُمِّي نَذَرَتْ أَنْ تَحُجَّ ، فَمَاتَتْ قَبْلَ أَنْ تَحُجَّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ ، حُجِّي عَنْهَا أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ أَكُنْتِ قَاضِيَتَهُ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . فَقَالَ : ((اقْضُوا اللَّهَ الَّذِي لَهُ ، فَإِنَّ اللَّهَ أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ )) رواه البخاري
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ambaye amesema: Alikuja mwanamke kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nina mama ambaye aliweka nadhiri kuwa atahiji, akafariki kabla ya kuhiji, je nimhijie? Akasema: ((Ndio, mhijie je ingelikuwa mama yako ana deni ungelimlipia?)) Akasema: Ndio. Akasema: ((Mkidhieni Allaah (deni)
Pia:
عن عَبْد اللَّهِ بْن بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ رَضِي اللَّه عَنْهما ، قَالَ : بَيْنَما أَنَا جَالِسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، إِذْ أَتَتْهُ امْرَأَةٌ ، فَقَالَتْ: إِنِّي تَصَدَّقْتُ عَلَى أُمِّي بِجَارِيَةٍ ، وَ إِنَّهَا مَاتَتْ . فَقَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : (( وَجَبَ أَجْرُكِ وَ رَدَّهَا عَلَيْكِ الْمِيرَاثُ)) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ كَانَ عَلَيْهَا صَوْمُ شَهْرٍ أفأصُومُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((صُومِي عَنْهَا)) قَالَتْ : إِنَّهَا لَمْ تَحُجَّ قَطُّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا؟ قَالَ: ((حُجِّي عَنْهَا)) مسلم
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ambaye amesema: Nilipokuwa nimekaa kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mwanamke akasema: Nimemtolea mama yangu sadaka ya kijakazi. Naye amefariki. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Umewajibika kupata ujira na mirathi itakurudia. Akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, alikuwa ana deni la mwezi la Swawm, je nimfungie? Akasema: ((Mfungie)). Akasema: Yeye hakuwahi kuhiji, je nimhijie? Akasema: ((Mhijie)) [Muslim]
Kuwatolea Sadaka:
عن أمّ المؤمنين عَائِشَةَ رَضِي اللَّه عَنْهَا ، أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا ( أي ماتت فجأةً ) وَ أَظُنُّهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أَجْرٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ)) البخاري
Kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Mama yangu imesokoteka nafsi yake [kwa maana amefariki ghafla] na nadhani
عن ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِي اللَّه عَنْهمَا ، أَنَّ سَعدَ بْنَ عُبَادَةَ رَضِي اللَّه عَنْهما تُوُفِّيَتْ أُمُّهُ وَ هُوَ غَائِبٌ عَنْهَا فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أُمِّي تُوُفِّيَتْ وَ أَنَا غَائِبٌ عَنْهَا أَيَنْفَعُهَا شَيْءٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ )) قَالَ: فَإِنِّي أُشْهِدُكَ أَنَّ حَائِطِيَ الْمِخْرَافَ ( اسم لبستان كان له) صَدَقَة ٌ عَلَيْهَا .- البخاري
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ambaye amesema: Sa’ad bin Ubaadah (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alifiwa na mama yake naye alikuwa hayupo akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, Mama yangu amefariki nami sikuweko. Je, itamfaa lolote nikimtolea sadaka? Akajibu: ((Ndio)) Akasema: Basi nashuhudia kwako kwamba ukuta wangu wa al-Mikhraaf [jina la bustani yake] ni sadaka kwa ajili yake. [Al-Bukhaariy]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أَبِي مَاتَ ، وَ تَرَكَ مَالاً وَ لَمْ يُوصِ ، فَهَلْ يُكَفِّرُ عَنْهُ أَنْ أَتَصَدَّقَ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ)) روى مسلم و ابن ماجة و النسائي
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Baba yangu amefariki na ameacha
4- Kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana na wao:
Kuwasiliana na ndugu, jamaa wenye uhusiano wa damu, wa karibu na wa mbali, mfano ‘ammu (kaka wa baba) ‘ammat (shangazi), khaal (kaka wa mama), khaalat (mama mdogo au mkubwa), watoto wao wote, bibi wa baba, bibi wa mama na wanaouhusiana wote kwa damu kwa kila upande.
Tutamube kwamba kuunga ukoo ni kitendo ambacho kimesisitizwa
((فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ))
((أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ ))
((Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na muwatupe jamaa zenu))
((Hao ndio Allaah Aliowalaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho
((الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الأَرْضِ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ))
((Wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kwisha ifunga, na wakayakata Aliyoamrisha Allaah kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara)) [Al-Baqarah: 27]
Na Kwenye Sunnah kuna usimulizi mwingi ambao kuna fadhila na faida nyingi na pia maonyo makali. Tunanukuu hapa usimulizi mmoja:
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يدخل الجنة قاطع رحم)) رواه الترمذي
Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Haingii Peponi mwenye kukata udugu)) [At-Trimidhiy]
5- Kuwakirimu rafiki zao
عن عبد الله بن دينار عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما أن رجلا من الأعراب لقيه بطريق مكة فسلم عليه عبد الله بن عمر وحمله على حمار كان يركبه وأعطاه عمامة كانت على رأسه . قال ابن دينار : فقلنا أصلحك الله إنهم الأعراب وهم يرضون باليسير , فقال عبد الله بن عمر إن أبا هذا كان ودا لعمر بن الخطاب وإني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( وإن أبر البر صلة الولد أهل ود أبيه )) مسلم
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Diynaar na kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba bedui mmoja alikutana naye njiani akielekea Makkah, akamsalimia ‘Abdullaah bin ‘Umar kisha akampakia juu ya punda aliyekuwa amempanda akavua kilemba chake na kumpa. Akasema Ibn Diynaar: Tukasema Allaah Akuwekee vizuri. Hao ni mabedui nao wanaridhika na kichache. Akasema ‘Abdullaah bin ‘Umar: Baba yake huyu alikuwa mpenzi wa ‘Umar ibnul Khattwwaab [Baba yangu] nami nimesikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kitendo chema kabisa ni mtoto kumpenda (kuungana na) rafiki wa baba)) [Muslim]
عن أبي بردة قال: قدمت المدينة فأتاني عبد الله بن عمر فقال أتدري لم أتيتك ؟ قال قلت لا . قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((من أحب أن يصل أباه في قبره فليصل إخوان أبيه)) وأنه كان بين أبي عمر وبين أبيك إخاء وود فأحببت أن أصل ذاك - ابن حبان في صحيحه
Pia kutoka kwa Abu Bardah ambaye amesema: Nilikuwa naelekea Madiynah akanijia ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: Je, unajua kwa nini nimekujia? Akasema: Nikasema: Hapana! Akasema: Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Anayependa kuungana na baba yake katika kaburi
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ajaalie haya mafunzo yawe yenye kuzingatiwa na Atuzidishie hima ya kuwafanyiwa wema wazazi wetu waliofariki.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



assalamu caleykum
assalamu caleykum waraxmatulaah wabarakatu, ba ada ya salamu, i am so happy to register my self in this website, maashalaah nimi penda saana na furahi saana.
my name is Ali Jeylani, I am from London, i am so happy to revieve this hadith and mawaida from this website, je i wonder kama netaweza ku iliza suali kisha natapata majibu, question aboutreligion. i hope to get a good answer from you brother as soon as possible.
a/s waraxmatulilaah wabarakatu.
Wa 'alaykumus-salaam wa
Wa 'alaykumus-salaam wa RahamtuLLaahi wa Barakaatuh
Unaweza kuuliza maswali kupitia maswali@alhidaaya.com au unaweza kutuma kwa kuingia hapo juu kwenye 'Wasiliana Na Sisi' kisha uchague 'Tuma Maswali' kisha utume swali lako.
Tafadhali fuata sheria za kutuma maswali kama zilivyotajwa humo- kutuma kila swali pekee na kila swali uweke maudhui inayofahamika ili iwe wepesi kufuatilia na kujibu.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA