Tofauti Baina Ya Dhikr Ya Unapoingia Sokoni Na Inayofanana Nayo

 

SWALI:

 

Swali langu nauliza katika adhkar, niliwahi kuelezwa kwamba ni bora kuongeza wahu wayamitu, kama ilivyoandika katika sehemu ya pili ya adhkar hiyo hiyo.. Je hii bora kuisoma hivyo na nini maana yake..

 

1. Ashhadu anlailaha ila lwahu, wahdahu lah sharika lahu lahumulk, wala ul hamdu wahuwa ala kuli shain kadir,

 

2.  Ashhadu anlailaha ila lwahu, wahdahu lah sharika lahu lahumulk, wala ul hamdu wahu wayumitu wahuwa ala kuli shain kadir,

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu utajo (dhikri) ya kuingia sokoni.

 

Kwanza tunapenda kurekebisha hayo tuliyopigia mistari. Yanapaswa kuandikwa na kusomeka hivi:

 

Ash-hadu Alla Ilaaha Illa Allaah, Wahdahu La Shariyka Lahu, Yuhyi Wa Yumiytu, Wa Huwa ‘Alaa Kulli Shay-in Qadiyr’

 

Du’aa ambayo tumeiona ya kuingia sokoni ni kama ifuatayo:

“Laa Ilaaha Illa Allaahu, Wahdahu Laa Shariyka Lahu Lahul Mulku, Walahul Hamdu Yuhyii wa Yumiytu Wa Huwa Hayyun Laa Yamuwt Biyadihil Khayr Wa Huwa ‘Alaa Kulli Shay-in Qadiyr

Hakuna muabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni zake sifa njema. Anahuisha na Anafisha, Naye Yu hai asiyekufa, khayr yote iko mikononi Mwake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza” [At-Tirmidhiy na Al-Haakim]

 

Kuna du’aa nyingine inayofanana na hiyo sana lakini si sahihi:

“Laa Ilaaha Illa Allaahu, Wahdahu Laa Shariyka Lahu Lahul Mulku, Walahul Hamdu Biyadihil Khayr Yuhyii wa Yumiytu Wa Huwa ‘Alaa Kulli Shay-in Qadiyr"

 

Na inadaiwa fadhila zake ni kama hizi:

"Mwenye kuisoma du’aa hii sokoni, ataandikiwa na Allaah thawabu milioni moja, kufutiwa madhambi milioni moja na kujengewa nyumba Peponi." Lakini hii ni HadiythiMunkar (Si Sahihi). Tumejaribu kutafuta du’aa hiyo kama ulivyoandika lakini hatukuipata kabisa.

 

Kwa hiyo ni bora kabisa kutumia hiyo du’aa ya mwanzo kwani ni sahihi haina mushkila wowote.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share