01 Wasiya Kumi Wa Allaah - Utangulizi-1
عَنْ عُبَادَة بْن الصَّامِت قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَيّكُمْ يُبَايِعنِي عَلَى ثَلَاث)) ثُمَّ تَلَا رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبّكُمْ عَلَيْكُمْ ...)) حَتَّى فَرَغَ مِنْ الْآيَات ((فَمَنْ وَفَى فَأَجْره عَلَى اللَّه وَمَنْ اِنْتَقَضَ مِنْهُنَّ شَيْئًا فَأَدْرَكَهُ اللَّه بِهِ فِي الدُّنْيَا كَانَتْ عُقُوبَته وَمَنْ أَخَّرَ إِلَى الْآخِرَة فَأَمْره إِلَى اللَّه إِنْ شَاءَ عَذَّبَهُ وَإِنْ شَاءَ عَفَا عَنْهُ))
Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nani atakayefanya agano nami katika matatu [Aayah tatu] Kisha akasoma hadi alipomaliza Aayah, akasema: ((Yeyote atakayetimiza (agano/ahadi hii) basi atapata thawabu zake kutoka kwa Allaah, lakini yeyote atakayefanya kasoro kwazo kisha Allaah Akamuadhibu duniani itakuwa ni malipo yake. Yeyote ambaye Allaah Atamcheleweshea (adhabu yake) hadi Akhera, basi hii ni amri ya Allaah. Akipenda Atamudhibu, na Akipenda Atamsamehe)) [Al-Haakim: 2:318]
Wasia hizi zilikuwa ni wasiya za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) za mwisho zenye muhuri wake.
عَنْ اِبْن مَسْعُود رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : مَنْ أَرَادَ أَنْ يَنْظُر إِلَى وَصِيَّة رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّتِي عَلَيْهَا خَاتَمه فَلْيَقْرَأْ هَؤُلَاءِ الْآيَات ((قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا)) - إِلَى قَوْله ((لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))
Kutoka kwa Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu) ambaye amesema: “Anayetaka kusoma wasiya wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambao ulikuwa na muhuri wake, basi asome Aayah zifuatazo: ((Sema: Njooni nikusomeeni Aliyokuharamishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote …)) hadi kauli Yake: ((ili mpate kumcha Mungu)) [Tuhfat Al-Ahwadhi]
Wasia huo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao unatokana na Qur-aan na ambao hauhusiani na mtu binafsi, kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha wasia kwa mtu –hasa hasa kuhusu Ukhalifa - , bali ameleta yaleyale yaliyomo kwenye Qur-aan ambazo zote zinapatikana katika Aayah tatu zifuatazo:
((قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلاَّ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَلاَ تَقْتُلُواْ أَوْلاَدَكُم مِّنْ إمْلاَقٍ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ وَلاَ تَقْرَبُواْ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَلاَ تَقْتُلُواْ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ))
((وَلاَ تَقْرَبُواْ مَالَ الْيَتِيمِ إِلاَّ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّى يَبْلُغَ أَشُدَّهُ وَأَوْفُواْ الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ لاَ نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُواْ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى وَبِعَهْدِ اللّهِ أَوْفُواْ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ))
((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ))
((Sema: Njooni nikusomeeni Aliyokuharamishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayoonekana, na yanayofichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Allaah Ameharamisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo Amekuusieni ili myatie akilini))
((Wala msiyakaribie
((Na kwa hakika hii ndiyo Njia Yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia Yake. Hayo Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu)) [Al-An’aam: 151-153]
Itaendelea InshaAllaah…/
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


