Skip navigation.
Home kabah

02 Wasiya Kumi Wa Allaah - Utangulizi-2

 

Wasiya Kumi Wa Allaah

Utangulizi-2

 

Wasia hizi zenye amri zimekuja baada ya kutangulia Aayah zinazoelezea madai ya makafiri Quraysh kuharamisha baadhi ya wanyama na vyakula na kuhusisha kwao vitu hivyo na masanamu yao, kuua watoto wao na kuzua mengi mengineyo yasiyokuwa katika sheria.  

 

((وَجَعَلُواْ لِلّهِ مِمِّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُواْ هَذَا لِلّهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَذَا لِشُرَكَآئِنَا فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمْ فَلاَ يَصِلُ إِلَى اللّهِ وَمَا كَانَ لِلّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَى شُرَكَآئِهِمْ سَاء مَا يَحْكُمُونَ))  

 

((Na wamemwekea sehemu Allaah katika mimea na wanyama Alioumba, nao husema: Hii ni sehemu ya Allaah - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Allaah na vilivyo kuwa vya Allaah huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu)) [Al-An’aam: 36]

 

 

(( وَكَذَلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلاَدِهِمْ شُرَكَآؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُواْ عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ وَلَوْ شَاء اللّهُ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ))

 

 (( وَقَالُواْ هَذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لاَّ يَطْعَمُهَا إِلاَّ مَن نّشَاء بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لاَّ يَذْكُرُونَ اسْمَ اللّهِ عَلَيْهَا افْتِرَاء عَلَيْهِ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفْتَرُونَ))

 

 (( وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَذِهِ الأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَى أَزْوَاجِنَا وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاء سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ إِنَّهُ حِكِيمٌ عَلِيمٌ))

 

 (( قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُواْ أَوْلاَدَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ اللّهُ افْتِرَاء عَلَى اللّهِ قَدْ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهْتَدِينَ))

 

((Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwaua watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Allaah Angelipenda wasingefanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua))

 

((Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Allaah juu yao. Wanamzulia uwongo tu Allaah Atawalipa kwa hayo wanayomzulia))

 

((Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni kwa ajili ya wanaume wetu tu, na wameharamishwa kwa wake zetu. Lakini ikiwa nyamafu basi wanashirikiana. Allaah Atawalipa kwa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye Hikma, Mwenye Kujua))

 

((Hakika wamekhasirika wale ambao wamewaua watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua, na wakaharimisha alivyo waruzuku Allaah kwa kumzulia Allaah Hakika wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka)) [Al-An’aam: 137-140]

 

Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anawauliza na kuwakanusha:

 

((ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الأُنثَيَيْنِ نَبِّؤُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ))

 

 (( وَمِنَ الإِبْلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الأُنثَيَيْنِ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاء إِذْ وَصَّاكُمُ اللّهُ بِهَذَا فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللّهِ كَذِبًا لِيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ))

 

 

((Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, Ameharamisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli))

 

((Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, Ameharamisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Allaah Alipokuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliyemzulia Allaah uongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Allaah Hawahidi watu madhaalimu)) [Al-an’aam: 143-144] 

 

Ni ujinga, upotofu kutokana na akili na matamanio yao yaliyowafanya waweke madai kama hayo ya shirk na kufru.

 

 Tunaelezea  baadhi ya madai yao kwa ufupi: 

 

  1. Baadhi ya vyakula na wanyama ni kwa ajili ya Allaah na wengine ni kwa ajili ya miungu yao (masanamu). Na hao wanyama walikuwa wakiachwa warande kwa uhuru bila ya kutumiliwa kwa kufaidika nao chochote ikiwa kuwapanda au kuwachinja. Wanyama walipewa majina ya masanamu yao Bahira, Saaibah, Waswiyla na Haam.

 

  1. Kichinjo chochote kilichohusishwa na Allaah, hakikuliwa isipokuwa kilichotaja majina ya masanamu yao wakati wa kuchinja. Ama walichokichinja kwa ajili ya masanamu yao, hawakuwa wakitaja jina la Allaah wakati wa kuchinja. 

 

  1. Wanapogawa hivyo vitu na ikatokea kwamba kilichokuwa cha masanamu yao kimeharibika, hubadilisha na kile kitu walichomhusisha Allaah. Ama ikiwa kilichoharibika ni cha Allaah, basi hukiacha hivyo hivyo Kwake.

 

  1. Ikiwa ni wanyama, na mfano mnyama huyo amezaa watoto wane, hugawa wawili wa Allaah, na wawili wa masanamu yao. Pindi ikiwa wanyama waliowahusisha na Allaah, ni wenye nguvu kuliko wa masanamu yao, waliwabadilisha na kuwahusisha masanamu yao.

 

  1. Wanyama walipokuwa waja wazito, waliharamisha maziwa yao kunywewa na wanawake, wakaruhusu wanaume pekee wanywe.

 

  1. Kondoo alipozaa kondoo dume, walimchinja na nyama ilikuwa halaal kwa wanaume pekee, wanawake hawakuruhusiwa kuila.

 

  1. Kondoo dume anapozaa jike, hawakuwa wakimchinja. Lakini anapozaa mnyama asiyekamilika (still-born) walimchinja na kuwaruhusu wanawake wamle.

 

Funzo gani au faida gani tunapata baada ya kutambua upotofu na ujinga wa hao Washirikina na madai yao hayo? Jibu ni kwamba:

 

Kwanza:

 

Sisi Waislamu tumejaaliwa neema kubwa kuepukana na shirk kama hizo. Hivyo inapasa tuwe tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutuongoza katika Uislamu na kututoa katika kiza cha ujinga kama huo.

 

Pili:

 

Kuisoma Qur-aan, kuifahamu maana yake, kujua sababu za kuteremshwa Aayah, humzidishia mtu kuzidi kupenda kujifunza Qur-aan na kuzidi kutambua neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) juu yetu kama neema kubwa ya Uislamu na ndipo tutakapoweza kuithamini dini yetu na kuipenda.

 

 

Itaendelea InshaAllaah…/