Skip navigation.
Home kabah

03 Wasiya Kumi Wa Allaah - Utangulizi-3

 

Baada ya Aayah za madai yao Washirikina na baada ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kuwauliza madai yao, ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika  Aayah inayofuatia Anamwambia Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aseme kuwa hayo Hakuyaharamisha Yeye bali ni uzushi wao na uongo wanaomzulia Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Ama Aliyoharamisha yanayohusiana na wanyama ni yafuatayo:

 

((قُل لاَّ أَجِدُ فِي مَا أُوْحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلاَّ أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللّهِ بِهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلاَ عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ))

 

 

((Sema: Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiyekuwa Allaah Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye Kusamehe, Mwenye Kurehemu)) [Al-An’aam: 45]

 

Baina ya hizo Aayah Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametaja Neema Zake na mimea, matunda na wanyama kwamba vyote hivyo Ametuuumbia kwa ajili ya manufaa yetu na Akatuonya tusifuate nyao za Shaytwaan akaja kutupotoa. 

 

((وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُواْ حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ وَلاَ تُسْرِفُواْ إِنَّهُ لاَ يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ))

 

 (( وَمِنَ الأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ))

 

((Na Yeye Ndiye Aliyeziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisiotambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbalimbali, na mizaituni na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye Hawapendi watumiayo kwa fujo))

 

((Na katika wanyama Amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah wala msifuate nyayo za Shaytwaan. Hakika yeye ni adui yenu dhaahiri)) [Al-An’aam: 141-142]

 

 

Mwishowe ndipo Anapomwambia Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  

 

((قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ...))

 

((Sema: Njooni nikusomeeni Aliyokuharamishieni Mola wenu Mlezi..)) hadi kumalizika hizo Aayah tatu zenye wasiya huu wa mambo kumi.

 

Zingatia kwamba katika kila mwisho wa Aayah hizo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anataja kuwa ni Wasiya ili …..

 

((Hayo Amekuusieni ili myatie akilini))

((Hayo Amekuusieni ili mpate kukumbuka

((Hayo Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu))

 

Tutaendelea  kutaja wasiya au amri zote kwa kuelezea moja moja kila wiki ili zifahamike vizuri na kwa upana zaidi, hadi tuzimalize zote Inshaa-Allaah. Ni matumaini yetu kuwa huu wasiya au hizi amri zitatekelezwa kama zllivyo maamrisho yake na kutegemea thawabu kutoka kwa Mola wetu Mtukufu.

 

 

Itaendelea InshaAllaah…/

 

Assalam Aleikum

Assalam Aleikum warahamatualla wabarakatu

Mimi Nilifiwa na mtoto wangu wakiume anaitwa Luqman

je ninaruhusiwa inshaalah amin kulieta jina hili Tena

Assalaamu 'alaykum Tafadhali

Assalaamu 'alaykum

Tafadhali tuma swali lako kupitia maswali@alhidaaya.com . Hapa ni mahali pa kuweka maoni tu yanayohusu makala iliyoko hapa.

Ndugu Zako
AL HIDAAYA