Skip navigation.
Home kabah

04 Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya wa Kwanza Kutokumshirikisha Allaah – 1

 

((قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلاَّ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئًا ..))

 

((Sema: Njooni nikusomeeni Aliyokuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote…))

 

Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni madhambi makubwa mno ambayo Hayasamehewi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ikiwa mtu hakuleta tawbah ya kweli.

 

 ((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء وَمَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدِ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا))

((Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na Husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa)) [An-Nisaa: 48]

Hadiyth ifuatayo inathibitisha pia kauli hiyo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

 

أَبِي ذَرّ رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  ((أَتَانِي جِبْرِيل فَبَشَّرَنِي أَنَّهُ مَنْ مَاتَ لَا يُشْرِك بِاَللَّهِ شَيْئًا مِنْ أُمَّتك دَخَلَ الْجَنَّة قُلْت وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ قُلْت وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ قُلْت وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ وَإِنْ شَرِبَ الْخَمْر)) متفق عقيه

 

Kutoka kwa Abu Dharr (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl akanibashiria kwamba yeyote katika Ummah wangu atakayefariki akiwa hakumshirikisha Allaah na chochote, ataingia Peponi. Nikasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba? Akasema: Hata kama ikiwa amezini na ameiba. Nikasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba? Akasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba. Nikasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba?  Akasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba na ikiwa amekunywa pombe)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na katika Hadiythul-Qudsiy

 

عن أنس رضي الله عنه   قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم  يَقُولُ:  ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي. يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ . يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لاَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.  

Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nilimsikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akisema: ((Allaah Amesema: Ewe Mwana wa Aadam utakaponiomba na kuweka matumaini kwangu, basi Nitakusamehe makosa uliyoyafanya na sitojali. Ewe Mwana wa Aadam kama dhambi zako zingefika mawingu ya mbingu na wewe ukaomba msamaha kwangu, ningekusamehe. Ewe Mwana wa Aadam kama ungelinijia na dhambi kubwa kama dunia na ukanikabili bila ya kunishirikisha nitakupa maghfira)) [Imesimuliwa na  At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Kutokumshirikisha Allaah ni ufunguo wa Pepo:

 عَنْ اِبْن مَسْعُود رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ مَاتَ لَا يُشْرِك بِاَللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّة))  مُسْلِم

Kutoka kwa ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ((Atakayefariki akiwa hakumshirkisha kitu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ataingia Peponi)) [Muslim]

 

 

 

 

 

Itaendelea InshaAllaah…/