05 Wasiya Kumi Wa Allaah Wasiya wa Kwanza Kutokumshirikisha Allaah - 2
Tunaendelea kuelezea kuhusu makatazo ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
Ni haki Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kutoka kwa waja Wake kutokumshirikisha, kwani Yeye Pekee Ndiye Muumba wetu:
عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رضي الله عنه قَالَ: ((كُنْتُ رِدْفَ النّبِيّ صلى الله عليه وسلم ليس بيني وبينه إِلا مؤخرة الرّحْلِ، فقال: يا معاذ بن جبل قلت: لبيك رسول اللّهِ وَسَعْدَيْكَ. ثُمّ سَارَ سَاعَةً، ثُمّ قَالَ: يَا مُعَاذُ بْنَ جَبَلٍ قُلْتُ: لَبّيْكَ رَسُولَ اللّهِ وَسَعْدَيْكَ. ثُمّ سَارَ سَاعَةً، ثُمّ قَالَ: يَا مُعَاذُ بْنَ جَبَلٍ قُلْتُ: لَبّيْكَ رَسُولَ اللّهِ وَسَعْدَيْكَ. قَالَ: هل تَدْرِي مَا حَقّ الله عَلَى الْعِبَادِ؟ قَالَ: قُلْتُ: الله وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: فَإِنّ حَقّ الله عَلَى الْعِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئا. ثُمّ سَارَ سَاعَةً، ثُمّ قَالَ: يَا مُعَاذُ بْنَ جَبَلٍ قُلْتُ: لَبّيْكَ رَسولَ اللّهِ وَسَعْدَيْكَ. قَالَ: هَلْ تَدْرِي مَا حَقّ الْعِبَادِ عَلَى الله إِذَا فَعَلُوا ذَلِكَ؟ قَالَ: قُلْتُ: الله وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ: أَنْ لاَ يُعَذّبَهُمْ)) البخاري
Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nilikuwa nimepanda (mnyama) nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hakukuwa na chochote baina yetu isipokuwa mwisho wa tandiko la farasi akasema: ((Ewe Mu’aadh bin Jabal)) Nikasema. Labayka wa Sa’dayka ewe Mjumbe wa Allaah. Kisha akaenda muda wa saa kisha akasema: ((Ewe Mu’aadh bin Jabal)) Nikasema. Labayka wa Sa’dayka ewe Mjumbe wa Allaah. Kisha akaenda muda wa saa kisha akasema: ((Ewe Mu’aadh bin Jabal)) Nikasema. Labayka wa Sa’dayka ewe Mjumbe wa Allaah. Akasema: ((Je unajua haki ya Allaah kutoka kwa waja?)) Nikasema: Allaah na Mjumbe Wake Wanajua zaidi: Akasema: ((Basi haki ya Allaah kwa waja Zake ni wamuabudu na wasimshirikishe Naye chochote)). Kisha Akaenda muda wa saa kisha akasema: ((Ewe Mu’aadh bin Jabal)) Nikasema. Labayka wa Sa’dayka ewe Mjumbe wa Allaah. Akasema: ((Je, unajua haki ya waja kwa Allaah ikiwa watafanya hivyo?)) Nikasema: Allaah na Mjumbe wake Wanajua zaidi. Akasema: ((Kwamba Asiwaadhibu)) [Al-Bukhaariy]
Haki ya Allaah kutoka kwa mja wake (mja anapaswa kumfanyia) ni kumuabudu bila ya kumshirikisha. Kufanya kinyume chake ni kumfanyia dhulma Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
((الَّذِينَ آمَنُواْ وَلَمْ يَلْبِسُواْ إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُوْلَئِكَ لَهُمُ الأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُون))
((Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani
Aayah hii iliwatia shaka Maswahaba wakamuuliza “Ewe Mjumbe wa Allaah nani katika sisi asiyejidhulumu?” Akasema: ((Sivyo hivyo mlivyofahamu, hamkusikia mja mwema (Luqmaan) alivyosema:
((يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ))
((Ewe mwanangu! Usimshirikishe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa)) [Luqmaan 31:13]
Itaendelea InshaAllaah…/
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


