Skip navigation.
Home kabah

Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya Wa 3 - Kutokuua Watoto

 

  Wasiya wa tatu ni makatazo ya kuua watoto:

((...وَلاَ تَقْتُلُواْ أَوْلاَدَكُم مِّنْ إمْلاَقٍ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ))

 

((…Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi Tunakuruzukuni nyinyi na wao….))

Amri hii asili yake ni kutokana na Makafiri waliokuwa wakiwaua watoto wao ima kwa khofu ya kuwa hawatoweza kuwapatia chakula au kuwaua wasichana kwa sababu ya kuwadhalilisha. Haya yote ni muongozo wa Shaytwaan kwao. Siku ya Qiyaamah wataulizwa kuhusu dhulma hii:

((وَإِذَا الْمَوْؤُودَةُ سُئِلَتْ))   (( بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ))

((Na msichana aliyezikwa hai atapoulizwa)) 

 

 ((Kwa kosa gani aliuliwa?)) [At-Takwiyr: 8-9]

 

Mapokezi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

عَبْد اللَّه بْن مَسْعُود رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّهُ سَأَلَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَآله وَسَلَّمَ ((أَيّ الذَّنْب أَعْظَم ؟)) قَالَ ((أَنْ تَجْعَل لِلَّهِ نِدًّا وَهُوَ خَلَقَك)) قُلْت ثُمَّ أَيّ  قَالَ ((أَنْ تَقْتُل وَلَدَك خَشْيَة أَنْ يُطْعَم مَعَك)) قُلْت ثُمَّ أَيّ ؟ قَالَ ((أَنْ تُزَانِي حَلِيلَة جَارك))  ثُمَّ تَلَا رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ   ((وَاَلَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّه إِلَهًا آخَر وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْس الَّتِي حَرَّمَ اللَّه إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Dhambi gani kubwa? Akasema: ((Kumfanyia Allaah mshirika na hali Yeye Amekuumba)) Nikasema: Kisha ipi? Akasema: ((Kumuua mtoto wako kwa khofu ya kutoweza kumpatia chakula chake)) Nikasema kisha ipi? Akasema: ((Kuzini na mke wa jirani yako)) Kisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasoma: ((Na wale wasiomuomba mungu mwengine pamoja na Allaah wala hawaui nafsi Aliyoiharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini)) [al-Bukhaariy na Muslim]

Ibn ‘Abbaas, Qataadah na As-Suddi na wengineo wamesema kuhusu: 

مِّنْ إمْلاَقٍ

 

((kwa sababu ya umasikini))

“Sio kuwaua kwa sababu nyinyi ni masikini. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema katika Suratul-Israa:

((وَلاَ تَقْتُلُواْ أَوْلادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلاقٍ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُم إنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْءًا كَبِير))

((Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi Tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa)) [al-Israa: 31]

Kutajwa wao kwanza kuwa Allaah Anawaruzuku kuna maana kwamba msikhofu umasikini kwa sababu ya kuwalisha watoto wenu, kwani hakika rizki yao inatoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)”.

 

  

Itaendelea InshaAllaah…/