Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya Wa 4 - Kutokukaribia Machafu (sehemu ya kwanza)
Wasiya wa nne ni kutokukaribia fawaahish (machafu). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
((..وَلاَ تَقْرَبُواْ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ...))
((…Wala msikaribie mambo machafu, yanayoonekana, na yanayofichikana...))
Maana ya fuhsh:
Kila tabia na kitendo kibaya ikiwa ni cha kutendwa au cha kutamkwa ambacho kinatoka nje na fitrah (maumbile asili) ya binaadamu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ وَإِيتَاء ذِي الْقُرْبَى وَيَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاء وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ))
((Hakika Allaah Anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na Anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka)) [An-Nahl: 90]
((إِنَّ اللّهَ لاَ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاء))
((Hakika Allaah Haamrishi mambo machafu)) [Al-A’raaf: 28]
((آتْلُ مَآ أُوحِىَ إِلَيْكَ مِنَ آلْكِتَابِ وَ أَقِمِ آلصَّلاَةَ إِنَّ آلصَّلاَةَ تَنْهَى عَنِ آلْفَحْشَآءِ وَ آلْمُنْكَرِ))
((Soma uliyofunuliwa katika Kitabu, na ushike Swalah. Hakika Swalah inazuilia mambo machafu na maovu)) [Al-'Ankabuut: 45]
Mara nyingine katika Qur-aan fahshaa (kwa matamshi ya ujumla) inakusudiwa ni zinaa au liwaatw nayo haikatazwi tu kutenda bali hata kukaribia.
((وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً))
((Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya)) [Al-Israa: 32]
(( وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّن الْعَالَمِينَ))
((Na Tulimtuma Luutw, alipowaambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!)) [Al-A’raaf: 80]
Na katika Sunnah:
عَنْ اِبْن مَسْعُود رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((لَا أَحَد أَغْيَر مِنْ اللَّه مِنْ أَجْل ذَلِكَ حَرَّمَ الْفَوَاحِش مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ)) متفق عليه
Kutoka kwa Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna mtu mwenye wivu zaidi ya Allaah. Ndio maana Akaharamisha vitendo vichafu vinavyotendwa kwa dhahiri na kwa siri)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
عن سَعْد بْن عُبَادَة قال: لَوْ رَأَيْت مَعَ اِمْرَأَتِي رَجُلًا لَضَرَبْته بِالسَّيْفِ غَيْر مُصَفَّح فَبَلَغَ ذَلِكَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ ((أَتَعْجَبُونَ مِنْ غَيْرَة سَعْد ؟ فَوَاَللَّهِ لَأَنَا أَغْيَر مِنْ سَعْد وَاَللَّه أَغْيَر مِنِّي مِنْ أَجْل ذَلِكَ حَرَّمَ الْفَوَاحِش مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ)) متفق عليه
Kutoka kwa Sa’ad bin ‘Ubaadah ambaye amesema: “Nikimuona mtu na mke wangu [wakifanya zinaa] nitamuua kwa upanga”. Ilipomfikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) habari hii alisema: ((Je, mnastaajabu wivu wa Sa’ad? Naapa kwa Allaah, mimi nina wivu zaidi kuliko Sa’ad, na Allaah Ana wivu zaidi yangu. Ndio maana Akaharamisha madhambi machafu yanayotendwa kwa dhahiri na kwa siri)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Itaendelea InshaAllaah…/
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


