Skip navigation.
Home kabah

Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya wa 4 Kutokukaribia Machafu - Sehemu Ya Pili

 

 

Tunaendelea kuelezea Wasia wa nne kuhusu ‘Kutokukaribia machafu’ kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

 

 ((..وَلاَ تَقْرَبُواْ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ...))

((…Wala msikaribie mambo machafu, yanayoonekana, na yanayofichikana…)) [Al-An'aam: 151]

 

Makala iliyopita tulidhihirisha kuwa fahshaa imekusudiwa ni zinaa, na makala hiii tunabainisha kwamba fahshaa inaweza kuwa kutokana na maneno machafu, kama kutukana, kulaani, ghiybah (kusengenya) n.k. Kisha tutamaliza kutaja fahshaa kwa ujumla ilivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah na kutaja madhara yake:

 

((إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ))

((Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu kali katika dunia na Akhera. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui)) [An-Nuur: 19]

 

عبد الله بن مسعود  رضي الله عنه  أن رسول الله  صلى الله عليه وسلم  قال: ((ليس المؤمن بالطعان ولا اللعان ولا الفاحش ولا البذيء))  رواه أحمد و إسناده صحيح

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muumini siye mwenye kutukana, wala kulaani, wala al-faahish [mwenye kufanya machafu] wala mwenye ujeuri)) [Imesimuliwa na Imaam Ahmad kwa isnaad Swahiyh]

 

Kutoka katika Qur-aan:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ))

((Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa khafifu)) [An-Najm: 32]

 

 

((وَالَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الإثم وَالْفَوَاحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُوا هُمْ يَغْفِرُونَ))

((Na wanaoyaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapokasirika wao husamehe)) [Ash-Shuura: 37]

 

 

Tahadhari na Shaytwaan kwani yeye ndiye mwenye kuamrisha al-fahshaa

 

((الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاء))

((Shaytwaan anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu)) [Al-Baqarah: 268]

 

 

((يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِي الأَرْضِ حَلاَلاً طَيِّباً وَلاَ تَتَّبِعُواْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ))

  (( إِنَّمَا يَأْمُرُكُمْ بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاء وَأَن تَقُولُواْ عَلَى اللّهِ مَا لاَ تَعْلَمُونَ ))

 

((Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shaytwaan. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri)) 

 

((Yeye anakuamrisheni maovu na machafu, na mumsingizie Allaah mambo msiyoyajua)) [Al-Baqarah: 168-169]. 

 

 

Kutoka Katika Sunnah:

 

عَنْ عَائِشَة قَالَتْ دَخَلَ عَلَى رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَهُود فَقَالُوا: السَّام عَلَيْك يَا أَبَا الْقَاسِم" فَقَالَتْ عَائِشَة : وَعَلَيْكُمْ السَّام قَالَتْ : فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ " ((يَا عَائِشَة إِنَّ اللَّه لَا يُحِبّ الْفُحْش وَلَا التَّفَحُّش)) قُلْت أَلَا تَسْمَعهُمْ يَقُولُونَ السَّام عَلَيْك" ؟ فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  (( أَوَمَا سَمِعْت أَقُول وَعَلَيْكُمْ)) البخاري

 

Kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye amesema: Baadhi ya Mayahudi walikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakamuamkia kwa kumwambia: “As-saam ‘alayka yaa Abal Qaasim” [kwa maana mauti yakufikie Ee baba wa Qaasim]. Basi nikasema: “Wa ‘alaykumus-saam” [kwa maana na mauti yakufikieni]. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ewe ‘Aaishah, hakika Allaah, Hapendi al-fuhsh wala at-tafahhush [uchafu na kutoa maneno machafu)). Nikasema: Je, hukuwasikia walivyosema “As-saam ‘alayka?” Akasema: ((Je, hukusikia nimewajibu “Wa ‘alaykum” [Na juu yenu])) [Al-Bukhaariy] 

 

Hadiyth hii inatufunza kwamba mtu anapokutukana ni bora ima kunyamaza au kumjibu bila ya kurudia maneno machafu aliyotamka yeye, bali kwa njia nyingine hata kama ni kumkejeli lakini sio kutamka maneno machafu.

 

وعن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال  ((إياكم و الفحش؛ فإن الله لا يحب الفاحش و المتفحش)) رواه أبو داود و أحمد و إسناده صحيح.

 

((Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Tahadharini na uchafu, kwani Allaah Hapendi mwenye kufanya uchafu na mwenye kutamka machafu)) [Abu Daawuud, Ahmad kwa isnaad Swahiyh]

 

 

Madhara ya al-fuhsh:

  1. Kujitenga mbali na Allaah kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hapendi wenye kutenda uovu huu kutokana na makatazo Yake.

 

  1. Kujitenga mbali na watu kwani husababisha ugomvi, chuki na uadui.

 

  1. Kujipatia malipo mabaya duniani na Akhera.

 

  1. Mojawapo ya kuharibu mujtamaa kwani fuhsh ni sababu ya kufarikisha      Watu ima kwa kukhasimiana na kuharibu undugu, ujamaa au urafiki  baina ya watu

 

  1. Suul-Khaatimah (mwisho mbaya) wa maisha ya binaadamu.

 

Itaendelea InshaAllaah…/