Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya wa 5 - Kutokuua Nafsi Aliyoharamisha Allaah, Ila Kwa Haki
Tunaendelea na mfululizo wa kutaja Wasia Kumi wa Allaah, na watano ni: ‘Kutokuua nafsi Aliyoharamisha Allaah ila kwa haki:
((... وَلاَ تَقْتُلُواْ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ ...))
((Wala msiuwe nafsi ambayo Allaah Ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki)) [Al-An’aam: 151]
Kumuua Muumini kwa makusudi kumekatazwa kwa maonyo makali na kwamba mwenye kufanya hivyo mambo manne yatamsibu
((وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا))
((Na mwenye kumuua Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Allaah Amemkasirikia, na Amemlaani, na Amemuandalia adhabu kubwa)) [An-Nisaa: 92-93]
1- Kuingizwa motoni na kudumu milele.
2- Kughadhibiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
3- Kulaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
4- Kuandaliwa adhabu kubwa.
Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya pia:
عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ)). رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alisema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Damu ya Muislamu haipasi kumwagwa isipokuwa katika hali tatu: Mzinzi Muolewa (Mtu mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa yule anayeacha Dini na akajifarikisha na jama’ah (kundi) (amejitenga na watu wa Dini yake)) [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Hata kuua wasio Waislamu pia imekatazwa pasi na haki. Mwenye kufanya hivyo hataisikia harufu ya Pepo:
((عَنْ عَبْد اللَّه بْن عُمَر عَنْ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرْفُوعًا مَنْ قَتْل مُعَاهَدًا لَمْ يُرَحْ رَائِحَة الْجَنَّة وَإِنَّ رِيحهَا لَيُوجَد مِنْ مَسِيرَة أَرْبَعِينَ عَامًا))
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar ambaye amesema: ((Yeyote aliyeua mtu ambaye alikuwa katika agano na kuhifadhiwa na Waislamu, hatasikia harufu ya Pepo, japokuwa harufu yake inasikika umbali wa miaka arubaini)) [Al-Bukhaariy]
((وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَة عَنْ النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ مَنْ قَتَلَ مُعَاهَدًا لَهُ ذِمَّة اللَّه وَذِمَّة رَسُوله فَقَدْ أَخْفَرَ بِذِمَّةِ اللَّه فَلَا يُرَحْ رَائِحَة الْجَنَّة وَإِنَّ رِيحهَا لَيُوجَد مِنْ مَسِيرَة سَبْعِينَ خَرِيفًا))
Na kutoka wa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote aliyeua mtu akiwa katika agano la kuhifadhiwa na Waislamu, na ambaye ananufaika na dhamana ya Allaah na Mjumbe Wake, atakuwa ameharibu dhamana ya Allaah, (kwake). Hatasikia harufu ya Pepo japokuwa harufu yake inasikika kutoka umbali wa miaka sabini)) [al-Bukhaariy]
Ufafanuzi zaidi wa Hadiyth hiyo unapatikana katika kiungo kifuatacho:
Sharh (maelezo) Ya Hadiyth Nambari 14 An-Nawawy - Damu Ya Muislam Haimwagiki Ila Kwa Mambo Matatu
Itaendelea InshaAllaah…/
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


