Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya Wa 7- Kutimiza Vipimo Na Mizani Kwa Uadilifu
Wasia wa Saba ni kutimiza vipimo na mizani kwa uadilifu
((... وَأَوْفُواْ الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ...))
((…Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu…)) [Al-An'aam: 152]
Ni amri ya kutekeleza haki wakati wa kutoa na kupokea, kununua na kuuza. Kutokupima kwa uadilifu ni kumdhulumu mtu haki yake ambayo ni dhulma isiyosameheka hadi umrudishie uliyemdhulumu hapa hapa duniani, laa sivyo basi Akhera itasimama mizani ya haki na hapo dhulma zote zitadhihirika na kila aliyemdhulumu mwenziwe atamlipa kwa mema yake na kutupiwa yeye madhambi ya mwenziwe. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaonya mwenye kufanya dhulma hiyo:
((وَيْل لِلْمُطَفِّفِينَ )) ((الَّذِينَ إِذَا اِكْتَالُوا عَلَى النَّاس يَسْتَوْفُونَ)) ((وَإِذَا كَالُوهُمْ أَوْ وَزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ)) ((أَلَا يَظُنّ أُولَئِكَ أَنَّهُمْ مَبْعُوثُونَ)) ((لِيَوْمٍ عَظِيم)) ((يَوْم يَقُوم النَّاس لِرَبِّ الْعَالَمِينَ))
((Ole wao hao wapunjao!)) ((Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe)) ((Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza)) ((Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa)) ((Katika Siku iliyo kuu)) ((Siku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?)) [Al-Mutwaffifiyn: 1-6]
Anahimiza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kupima kwa haki katika Aayah nyinginezo kwenye Qur-aan:
((وَأَوْفُوا الْكَيْلَ إِذا كِلْتُمْ وَزِنُواْ بِالقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً))
((Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na khatimaye ndio bora)) [Al-Israa: 35]
(( أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ)) (( وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ))
((
((Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani)) [Ar-Rahmaan: 8-9]
Makatazo haya yanawahusu zaidi wenye kufanya biashara wawe wanapima kwa kiasi cha haki yake, wasipunguze ikawa ni kumdhulumu anayemuuzia. Mfano ikiwa unampimia mtu chakula cha kilo 2 basi ufanye hivyo hivyo, isipungue ikawa kilo 1.9 au chini yake, kuongeza inafaa kwa mapendekezo yako ama kupunguza haifai kabisa. Vile vile inakusudiwa kuuza kitu kibaya aina yoyote, au kuchanganya kibaya juu ya kizuri ili kupata wingi wa kitu. Yote hayo inakuwa ni dhulma katika kumuuzia mtu kitu. Watu wa kale wa Madyan mojawapo ya maovu
((كَذَّبَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ الْمُرْسَلِين)) ((إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ)) ((إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ)) ((فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُون)) ((وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ)) ((أَوْفُوا الْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُخْسِرِينَ)) ((وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ)) ((وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ))
((Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume))
((Shu’ayb alipowaambia: Je! Hamfanyi mkamcha Mungu?))
((Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu))
((Basi mcheni Allaah na nitiini mimi))
((Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote))
((Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanaopunja))
((Na pimeni kwa haki iliyonyooka))
((Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi)) [As-Shu’araa: 176-183]
((وَإِلَى مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْباً قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَوْفُواْ الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلاَ تَبْخَسُواْ النَّاسَ أَشْيَاءهُمْ وَلاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ بَعْدَ إِصْلاَحِهَا ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ))
Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu
Itaendelea InshaAllaah…/
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


