Wasiya Kumi Wa Allaah - Wasiya Wa Mwisho - Kufuata Njia Iliyonyooka Na Sio Njia Nyinginezo
Wasia wa kumi wa Allaah na ambao ni mwisho katika somo hili, ni kufuata Swiraatul-Mustaqiym (Njia iliyonyooka) na sio njia nyinginezo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
((... وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ))
((…Na kwa hakika hii ndiyo Njia Yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Hayo Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu)) [Al-An’aam: 153]
Wasiya huu wa kumi ni muhimu kabisa kutekelezwa kwani ni asili ya kujiweka Muislamu katika usalama wa Dini yake kwa kubakia katika Tawhiyd, Dini safi, katika Iymaan na Taqwa, kujieupusha na shari za Shaytwaan, na kubakia katika njia ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nyendo za Maswahaba zake pamoja na Salafus-Swaalih (Wema waliopita).
Ufafanuzi wa Swiraatul-Mustaqiym kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ جَابِر قَالَ : "كُنَّا جُلُوسًا عِنْد النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَخَطَّ خَطًّا هَكَذَا أَمَامه فَقَالَ ((هَذَا سَبِيل اللَّه)) وَخَطَّيْنِ عَنْ يَمِينه وَخَطَّيْنِ عَنْ شِمَاله وَقَالَ ((هَذِهِ سُبُل الشَّيْطَان)) ثُمَّ وَضَعَ يَده فِي الْخَطّ الْأَوْسَط ثُمَّ تَلَا هَذِهِ الْآيَة" ((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُل فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيله ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)) وَرَوَاهُ أَحْمَد وَابْن مَاجَهْ
Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Tulikuwa tumekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akachora mstari mbele yake, akasema: ((Hii ni njia ya Allaah)). Kisha akachora mistari miwili upande wa kulia (wa huo mstari mkuu) na miwili upande wa kushoto yake, kisha akasema: ((Hizi njia za Shaytwaan)) Kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasoma Aayah hii: ((Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia Yake. Hayo Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu)) [Ahmad na Ibn Maajah]
Maonyo mengi kabisa ametupa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kututahadharisha tusitoke nje ya Swiraatul-Mustaqiym, kwani kufanya hivyo ndio sababu kuu ya Waislamu kutafarukiana na kusababisha ufisadi wa Dini.
عَنْ النَّوَّاس بْن سَمْعَان عَنْ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((ضَرَبَ اللَّه مَثَلًا صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا وَعَنْ جَنْبَيْ الصِّرَاط سُورَانِ فِيهِمَا أَبْوَاب مُفَتَّحَة وَعَلَى الْأَبْوَاب سُتُور مُرْخَاة وَعَلَى بَاب الصِّرَاط دَاعٍ يَقُول يَا أَيّهَا النَّاس اُدْخُلُوا الصِّرَاط الْمُسْتَقِيم جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا وَدَاع يَدْعُو مِنْ فَوْق الصِّرَاط فَإِذَا أَرَادَ الْإِنْسَان أَنْ يَفْتَح شَيْئًا مِنْ تِلْكَ الْأَبْوَاب قَالَ وَيْحك لَا تَفْتَحهُ فَإِنَّك إِنْ تَفْتَحهُ تَلِجهُ فَالصِّرَاط الْإِسْلَام وَالسُّورَانِ حُدُود اللَّه وَالْأَبْوَاب الْمُفَتَّحَة مَحَارِم اللَّه وَذَلِكَ الدَّاعِي عَلَى رَأْس الصِّرَاط كِتَاب اللَّه وَالدَّاعِي مِنْ فَوْق الصِّرَاط وَاعِظ اللَّه فِي قَلْب كُلّ مُسْلِم)) وَرَوَاهُ التِّرْمِذِيّ وَالنَّسَائِيّ
Kutoka kwa An-Nawwaas bin Sam’aan kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Ametoa mfano wa Swiratul-Mustaqiym [njia iliyonyooka] na katika pande mbili za hii njia, kuna kuta mbili zilizokuwa na milango ya kutokea. Katika milango hiyo, kuna mapazia yaliyoteremshwa chini. Na katika mlango wa njia hii kuna muitaji “Enyi watu! Njooni muingie katika Njia Iliyonyooka pamoja msigawanyike”. Kisha kuna muitaji mwengine anayeita kutoka juu ya njia ambaye humwambia mtu anapotaka kuondosha pazia katika milango yoyote hii. “Ole wako! Usifungue mlango huu, kwani ukiufungua utakuja kuingia humo. Njia Iliyonyooka ni Uislamu. Kuta mbili ni mipaka ya Allaah. Milango iliyofunguliwa inaongoza katika maharimisho ya Allaah. Muitaji katika lango la njia ni kitabu cha Allaah (Qur-aan), na muitaji kutoka juu ya njia ni mawaidha ya Allaah katika moyo wa kila Muislamu)) [Ahmad]
Vitu viwili muhimu alivyotuachia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tubakie katika Swiraatul-Mustaqiym:
((تَرَكْتُ فِيكُمْ مَا اِنْ تَمَسَّكْتُمْ بِهِ لَنْ تَضِلُّوا بَعْدِي اَبَداً كِتَابُ الله وَسُنََّتِي))
((Nakuachieni kile ambacho mkikishikilia hamtapotea
Shaytwaan naye yumo katika jihaad kubwa kututoa katika Swiraatul-Mustaqiym:
((قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ)) (( ثُمَّ لآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَآئِلِهِمْ وَلاَ تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ))
((Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia Yako Iliyonyooka))
((Kisha nitawazukia mbele
Hizi ndizo Wasiya kumi au amri kumi
Mwisho
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


