Skip navigation.
Home kabah

Simu Zitatuangamiza

 

 

‘Abdun-Naaswir Hikmany

 

Kwa vile tupo kwenye “utandawazi” wa ukafiri ndani ya jamii zetu, imekuwa ni vigumu kuepukana na usawa wa maadili ya Magharibi. Hata hivyo, bado tuna nafasi ya kushindana na ukafiri kwa vitendo na kauli zetu. Ni vyema kila mmoja akachukua hadhi yake aliyonayo kukomesha maadili potofu angalau kwa kukemea na kuachana nayo. Kwani hakuna anayelazimishwa kuyafuata kwa mtutu wa bunduki.

Uislamu wetu ni njia maridhawa ya kuifuata kwa kila hatua tunayopiga. Ni njia isiyokubali mfumo wowote wa kuhamasisha muziki, ikiwa ni kwa kuimba, kutia miziki, kununua, kubeba au vyenginevyo. Vivyo hivyo, haifai kwa Muislamu kuwa na yale mawazo ya watu wa Magharibi wanaosema: “When You Are In Rome, Do As The Romans Do” – Unapokuwa Roma Fanya Kama Warumi Wafanyavyo. Bila ya kuona hayaa, Waswahili nao wameanzisha msemo unaofanana nao “Liingialo Mjini Si Haramu”. Yote haya ni maneno ya uzushi yasiyolingana na mafunzo ya Uislamu na yanafaa kupigwa vita kwa vitendo na kauli.

Ni kutokana na misemo hiyo, tunaona vijana kwa wazee wakibeba simu zenye kushehena kila aina ya muziki, sio tu majumbani bali mpaka misikitini Subhaana Allaah! Wengine wanakwenda mbali hadi kuingiza ndani ya simu zao mambo ya kuchefua roho kama vile picha au michezo ya kuhamasisha uasharati. Hapa ndipo tunapojiangamiza kwa kujua au wengine kwa ujinga wetu tu.

Je! Kuna tofauti ya Muislamu aliyeingia msikitini akiwa amebeba seti nzima ya redio na yule ambaye amebeba simu yake yenye miziki ya waimbaji wa kila namna? Waislamu tutafakari kwa kutumia kanuni za Kiislamu katika kila hatua ya maamuzi tunayofanya juu ya maisha yetu. Ama si hivyo, tutageuza misikiti yetu sawa na makanisa yaliyojaa kila aina ya ala za muziki. Huenda Waislamu wakawashinda hata Wakristo kwa kuingia na sinema zenye uasharati ndani ya misikiti yao.

Sio vyema kuvamia kila aina ya teknolojia na kuitaka kuitumia hata kama ikiwa ni yenye kupelekea kwenye maadili potofu. Tunachohitaji kuzingatia hapa; sio kwenda msikitini bila ya simu, kuitoa sauti au kuizima simu pale tu unapoingia msikitini. Laa hasha! Lengo ni kuondosha huu uovu kwa kufuta aina zote ya maadili maovu ndani ya simu zetu na kuachana kabisa kuweka miziki ndani ya simu zetu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba:

“Kutakuwa na watu miongoni mwa ummah wangu watakaofanya kuwa ni ruhusa uzinifu, Hariri, ulevi na ala za muziki...” Imesimuliwa na al-Bukhaariy, 5590.

 

Hadiyth hii inaonesha kwamba ala za muziki ni haramu kwa njia mbili. Kwanza, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: watakaofanya kuwa ni ruhusa,” ambayo inaonesha wazi kwamba vitu vilivyoainishwa – vikiwemo ala za muziki – haviruhusiwi ndani ya Shari’ah, lakini watu watavifanya kuwa ni vyenye kuruhusiwa. Pili, ala za muziki zinatajwa pamoja na vitu vyengine ambavyo haviruhusiwi, navyo ni uzinifu na ulevi. Kama ala za muziki zisingelikuwa ni haramu, zisingelitajwa pamoja navyo. (as-Silsilah as-Swahiyhah ya Imaam al-Albaaniy, 1/140-141)

Hapa ndipo inapoonekana tofauti ya Muislamu na Muumini. Kwani wanapoambiwa waumini husema: “tumesikia na tunatii” [2:285].

Nasaha zetu kwa Waislamu ni kuweka milio ya kawaida tu isiyo na miziki. Hili litatutofautisha na Makafiri, kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kujifanananisha nao. Kukosa kufuata maagizo ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kujitakia maangamizi ambayo ndio tunayaona kila pembe ya dunia hii. Mara kimbunga, tetemeko la ardhi, mvua kali, ajali za ndege na mengineyo. Maafa ambayo yamechaga kwa ufedhuli wa matendo yetu.

Waalaykumu salaam

Waalaykumu salaam warahmatuLlaahi wabarakatuh;

Jazaakumu Llaau khayra kwa maoni na michango yenu. Allaah Atujaalie nasi tuwe mfano kwa jamii inayotuzunguka na Atujaalie himma ya diyn yetu tukufu insha Allaah.

Ndugu Assalam Alaykum! Shekh

Ndugu Assalam Alaykum!

Shekh Mwenyezi Mungu Akujalie Pepo Yake kwa uamsho huu mzuri tena wa bure unaotupa.
Hakika mimi nilikuwa nikifikiri eti "huko nyumbani ni afadhali". Sisi huku Magharibi ni kama tu twaishi ndani ya jahanamu sababu ya (newteknolojia) haswa kwa sisi wazazi ambao tuna watoto.
Tulipokuja hapa magharibi badhi yetu tulifikiri kuwa tutapata nafu. La asha! Hatukupata lolote ila kufirisika kiimani.
Je wale ambao tumejaliwa kuona ya kuwa yatufa sisi kufanya hijra tutakwenda wapi na hayo tunayoyasikia huko nyumbani? Nauliza swali hili sababu hata ndugu zetu waliobaki Africa hawatusapoti kurudi nyumbani ili tushirikiane kukarabati imani zetu (kama vikundi vya daawa). Badala yake nao wanapendelea kuja hapa magharibi(jahanamu)eti tushirikiane kupotea na kuhiriki.

Hivyo kwa wale ambao wanaota kuja kufaulu hapa magharibi (kwenye chemchemu ya newteknolojia), nawasihi waachane na ndoto hiyo potofu(wapoze mizuka) sababu hata sisi twajuta kuwa hapa.
Badhi wamebadilisha Dini, majina, desturi ili kuepuka ubaguzi lakini hawakufaulu.
Mimi niko tayari kuja kushirikiana na ndugu zangu katika kuijenga jaami kama ile aliyotufunza Mtume wetu Swalla Allahu alayihi wa aalihi wa salam.

Ma ssalam

Mohamed Abdillah Baranyikwa (Canada)

ASALAM ALAYKUM, Maoni yangu

ASALAM ALAYKUM,

Maoni yangu kwa newteknoloji hii ya sasa tulionayo ya hizi simu kwakweli tunaangamia wazi kabisa haitaki hata kushereheswa, iko wazi kabisa ili kuweza kuchukuwa hatuwa japo kulipunguza japo kwa 25% tutalazimika kuandaa Midahala Maalum kuhusu hili, kwasababu hiyi newteknoloji inakuwa kila leo, kwakweli tunaangamia vibaya, imekuwa ni jambo la kawaida kupatikana Music katika Miskiti yetu yote sasa tumepiga hatuwa sana Makanisa sasa yako nyuma yetu takriban 65% kama sikosei. Tunajua sote niujinga wetu tu kama ulivyosema hapo kabla, Liingialo Mjini si Haramu, {Inna lillah wa inna Illah Ra-jiun} tunaangamia. Mmoja wetu akimsiki mwenzake kapigiwa simu naimelia Music katika msikiti kubwa atamcheka na kumpongeza atamwambia he, pale Mzee umetutumbwiza bado kidogo Imamu aanze kucheza hi basi hakuna la ziada.Mtihani

ASALAM ALAYKUM
AHSANT
SALUM SULEIMAN NASSOR