Weka Matumaini Kwa Allaah
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Hakika kalimah ya Uislamu ambayo tunaiamini Waislamu, ndio ufunguo wa Pepo. Kalimah ambayo yatakiwa kutamkwa kwa ulimi, kuwekwa ndani ya moyo na kusadikishwa kwa vitendo. Kalimah hiyo ni Laa ilaaha illa Allaah Muhammadun Rasuulu Llaah – Hakuna Mola Apasaye Kuabudiwa ila Allaah na Muhammad ndiye Mjumbe Wake.
Kinachotakiwa hapo ni kumsadikisha Mola Mlezi kwa vitendo sio kwa kutamkwa
Hata kama tutakuwa na vitendo viovu na makosa ya hapa na pale, bado (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaweza kututakabalia toba zetu na kutufungulia milango ya khayr. Kitu kikubwa kinachohimizwa hapa ni kutomshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kiumbe chochote
((Ewe Mwana wa Aadam utakaponiomba na kuweka matumaini kwangu, basi Nitakusamehe makosa uliyoyafanya na sitojali. Ewe Mwana wa Aadam
Rahma Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Zimetawala ndani ya maisha yetu, kwani bila ya shaka hakuna neema kubwa tuliyopatiwa kuliko uhai. Neema ambayo inapokatika hairudi tena. Kilichokusanywa ndicho kinachopokelewa. Hakuna tunachoweza kukiongeza baada ya hapo ila yale mambo matatu yanayomfaa Muislamu baada ya kutoka roho (swadaqah yenye kuendelea, mtoto anayekuombea na elimu yenye manufaa). Tujitahidi kuwa na himma ya diyn yetu hii tukufu kwa kuweka matumaini yetu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


