Utawala Wa Kifalme Unafaa Katika Uislamu? Tunaweza Kupiga Kura?
SW
Assalam aleykum.. nimejitokeza tena katika ukumbi huu wa maswali lengo ni kutaka kutoka wasiwasi wangu wa moyo.. swali langu ni je.. huu utawala wa kifalme ni halali mbele ya M/Mungu au tunawajibika kupiga kura
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa maswali yako kuhusu utawala wa kifalme na kupiga kura. Ama kuhusu suala la kwanza ni kuwa Uislamu hautambui utawala wa kifalme kabisa. Utawala ulio sahihi wa Kiislamu ni kuwa Waislamu wawe ni wenye kumchagua au baraza la shuura liwe ni lenye kumchagua kiongozi aliye na sifa za Kiislamu bila kujali ukoo, kabila na hadhi yake katika jamii. Lau kungekuwa na ufalme basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angemchagua jamaa yake kushika wadhifa huo muhimu. Wapo jamaa zake waliokufa baada yake
Alipoaga dunia, Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliona anayefaa ni Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), naye alipofariki akamchagua ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Maswahaba wakakubali
Wakati wa dola ya kifalme ya Banu Umayyah, ‘Umar bin ‘Abdil-‘Aziyz alichaguliwa na binamu yake, Sulaymaan bin ‘Abdil-Maalik, kwa kuwa watoto wake walikuwa ni wadogo. Baada ya kushika mamlaka aliwaambia raia yeye hatakubali uongozi huo mpaka waamue
Mtume Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametabiri jinsi gani Ummah huu utakavyokwenda kuanzia wakati wake. Na Ummah utanawiri utakaporudi ukhalifa kwa mara nyingine tena. Alisema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Utume utabaki miongoni mwenu kwa muda ambao Allaah Atataka ubaki kisha utaondoka Anapotaka uondoke. Baadaye utakuja ukhalifa kwa njia ya aliyofuata Mtume na utabaki kwa muda ambao Allaah Atataka ubaki kisha utaondoka pale Anapotaka. Kisha kutakuja kipindi cha ufalme na kitabaki nanyi kwa muda ambao Allaah Anataka ubaki kisha utaondoka pale Anapotaka Allaah. Kisha kitakuja kipindi cha udikteta na viongozi madhalimu na kipindi hicho kitabaki nanyi muda ambao Allaah Atataka Kibaki nanyi kisha utaondoka pale Allaah Anapotaka uondoke. Kisha utakuja ukhalifa kwa muongozo unaomfuata Mtume. Kisha baada ya hapo akanyamaza.” (Hadiyth Sahihi iliyonukuliwa na Ahmad 4/273 kutoka kwa an-Nu‘maan bin Bashiyr – Radhiya Allaahu ‘anhuma).
Ama kuhusu swali lako la pili ni kuwa wanazuoni wa sasa wamegawanyika makundi mawili kuna wanaopinga upigaji kura na wengine wenye kuunga. Kila mmoja anatoa dalili zake, na zinazoonyesha kuwa inafaa zina nguvu kwa kiasi chake. Majma’ al-Fiqhiy al-Islaamiy katika mwaka wa 2002 (1423 Hijri) walikutana kujadili suala
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


