Maiti Kukamuliwa Ni Lazima? – Ameusia Asikurubishiwe Moto
SWALI:
Assalamu alaikum warahmatullahi,
Hivi majuzi niliandika wasia wangu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kukamuliwa wakati unaoshwa baada ya kuaga dunia. Vitabu mbalimbali maarufu vya Fiqhi kama Swahiyhu Fiqhus Sunnah cha Shaykh Abu Maalik, Minhaajul Muslim cha Shaykh Abu Bakr Jaabir al-Jazaairiy na pia al-Mulakhkhasw al-Fiqhiy cha Shaykh Dkt. Swaalih Fawzaan aal-Fawzaan.
Vitabu hivi ambavyo tumevitaja na venginevyo vinatueleza njia ambayo inafaa kufuatwa ili kumtayarisha Muislamu aliyekufa kwa mazishi. Katika moja ya njia hiyo ni kukamuliwa maiti ili kukamilisha tendo la kuoshwa, kuswaliwa na kisha kuzikwa. Lakini fahamu kuwa kukamuliwa huko si kukamuliwa kama wanavyofanya baadhi ya watu au vitabu vinavyosema kuwa anakamuliwa kwa nguvu, na hadi wengine wanamkunja maiti na kuminya tumbo
Muislamu aliye hai anafaa kujisafisha na kuondoa uchafu kwa juhudi yake kubwa. Lakini pindi anapofariki huwa hawezi kujitwahirisha wala kujisafisha hivyo inafaa walio hai wamkirimu kwa kumsafisha na kumtayarisha kwa ajili ya mazishi. Katika kumsafisha ni kumtoa uchafu ulio ndani ya matumbo. Na inafaa tufahamu kuwa kukamuliwa huko kunafanywa kwa taratibu ili asiumizwe kwa njia yoyote ile.
Ama kuwekwa moto na kufukizwa si jambo lenye kupendeza wakati wowote ule, lakini kwa kama kuna harufu au kunachelewa
Kwa faida zaidi ya mas-ala ya maiti, ingia kwenye viungo vifuatavyo:
Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
