Zingatio La Wiki - Mgeni Bora
'Abdun-Naaswir Hikmany
Kwa hakika tumejiwa na mgeni bora kuliko wote. Hayupo kwa muda mrefu na siku chache tu atatuacha. Huyu si mwengine bali ni mwezi mtukufu wa Ramadhaan. Kama tulivyoanza kwa hisabu ya Ramadhaan ya kwanza ndivyo tutakavyofika hadi Ramadhaan ya 29 au 30 insha Allaah.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelezea kuhusu fadhila za mwezi huu: ((Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni Fardh, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytwaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi alfu. Atakayenyimwa kheri zake hakika kanyimwa [yote ya kheri])) [Ahmad]
Lengo la ujio wa Ramadhaan si jengine ila kuwatoa Waislamu kwenye fikra za Shaytwaan kwenda katika ucha Mungu. Huu ni mwezi wa kuomba toba, kuifikiria Akhera zaidi kuliko dunia. Ni mwezi wa kufikiriana baina ya Waislamu kwa kila mwenye kuhitajia msaada ukiwa wa hali au
Huu si mwezi wa kununua mikeka ukitaraji futari huku jirani yako amelala njaa siku tatu. Si mwezi wa kwenda kutafuta hijabu ukitaraji kuigeuza jina na kuwa 'tambara' baada ya Ramadhaan. Wala si mwezi wa kwenda kutafuta karata na kuvingarisha vibaraza vya keram. Hao ni wachache wa akili wanaochukulia mwezi huu kuwa ni mzigo na adhabu kwao. Na bila ya kuwasahau wanaojali kujilimibikizia
Wenye akili huutumia mwezi huu kwa kufuta dhambi, kuongeza mema, kuzidisha kisimamo cha usiku, kuhudhuria darsa, kuhama vitanda kwa kuomba maghfira usiku, kukithiri i’tikafu na mengineyo mazuri. Na wapo pia wanaopata angalau juzuu moja kwa siku kila baada ya alfajiri na kupata uchangamfu mzuri wa mwili bila ya kurudia tena kitandani.
Unadhifu wa matendo ya Ramadhaan ni kuitimiza amri ya Swawm bila ya kutafuta hoja. Kwani Waumini wa kweli husema:
“Tumesikia na tunatii” [2: 285]
Itakuwa ni hasara kubwa kumaliza Ramadhaan tukiwa bado tumo kwenye usajili wa watu wa Motoni. Allaah Atukinge na adhabu hiyo!
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


