Msichana Kumfundisha Mvulana Masomo Inafaa?
SW
Asalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu
ndugu zangu waislamu nauliza swali mimi ni msichana namfundisha mvulana mmoja ni jamaa yetu kijana mvulana mkubwa kwangu kwa miaka 8 namfundisha computer nyumbani kwetu kila siku muda ya masaa mawili lakini huwa hatuko peke yetu imma awe mamangu na sisi ama ndugu yangu nataka kujua nini hukumu yake washukran nijibuni tafadhali. Waalaikum salam warahmatullahi wabarakatu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumfundisha mvulana masomo.
Uislamu umeweka mipaka ya kukaa faragha baina msichana na mvulana ambao wanaweza kuoana. Haifai kabisa kwa watu hao wawili kukaa faragha hata kusomeshana Qur-aan kwani watatu wao ni Shaytwaan, naye hutembea ndani ya miili yetu
Hata hivyo,
1. Usilegeze sauti yako wakati wa kumfundisha.
2. Uvae nguo za heshima kama zilivyoamrishwa na Uislaam,
3. Usifanye naye mzaha wala kuzungumza mengine mbali na kumsomesha.
Ikiwa utafuata maagizo hayo kutakuwa hakuna tatizo la kumsomesha.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
