Umefika Wakati Wa Kujifunza Kiarabu, Lugha Ya Qur-aan!
Assalaamu ‘Alaykum ndugu wapenzi Waislam
Umefika wakati wa kila mmoja wetu kujifunza Lugha ya Qur-aan! Hakutakuwa tena na hoja mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwamba hukupata njia ya kufunza Lugha hii muhimu ili uweze kufahamu maneno ya Mola wako Mtukufu, hivyo uisome Qur-aan haqqa tilaawatihi (
Tumewakusanyia mafunzo ya Lugha ya Kiarabu kwa video ambayo yanafunzwa katika Chuo Kikuu Cha Kiislamu Madiynah miaka 30 hadi sasa, kwa kutumia Vitabu Vitatu Vya Madiynah Vya Lugha Ya Kiarabu nayo yamo katika kiungo kifuatacho:
Mafunzo haya yameandaliwa kwa ajili watu waweze kuyapata popote walipo duniani na waweze kujifunza Lugha hii wakiwa majumbani mwao. Juu ya hivyo, ni bure bila ya gharama yoyote. Walioandaa mafunzo haya ni watu waliojitolea kwa hali na
Wanafuzi wengi waliomaliza masomo haya ambayo yanaendeshwa zaidi ya miaka kumi, wameishia nao kuwa waalimu wa Lugha hii na kufungua madarasa sehemu mbali mbali wanakoishi.
Vitabu vyake pia vinapatikana bure katika mtandao, navyo tunawawekea viungo vyake. Hali kadhalika kuna baraza ‘forum’ ambayo utaweza kuuliza maswali moja kwa moja kwa Dr. Abdur-Rahiym mwenyewe (Mwandishi wa Vitabu) au waalimu wengineo kuhusu kuhusu masomo hayo pindi utakapokabiliana na jambo usilolifahamu. Bonyeza kiungo kifuatacho:
Ask your questions in our new FORUM
Kwa Nini Utilie Hima Muislamu Kujifunza Lugha Ya Qur-aan?
Ili uweze kuifahamu Qur-aan khaswa kama Anavyokusudia Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), hakuna budi kuisoma kwa Lugha yake ya asili kwani Lugha ya Kiarabu ni Lugha pana, yenye ufasaha wa aina ya pekee na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa hikma Yake, Akaichagua Lugha hii kuwa ni Lugha ya Qur-aan na kuituma kwa Mjumbe Mwarabu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Vyovyote itakavyofasiriwa Qur-aan katika Lugha nyingine, haiwezakani
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
(( بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ )) ((حم)) (( وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ)) (( إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ))
((Kwa Jina La Allaah,
((Haa Miym)) ((Naapa kwa Kitabu kinachobainisha)) ((Hakika Sisi tumeifanya Qur-aan kwa Kiarabu ili mfahamu)) [Az-Zukhruf: 1-3]
‘Kwa Kiarabu’ kwa maana: Kwa Lugha ya Kiarabu iliyo fasaha na inayoeleza dhahiri, wazi. “Ili mfahamu” kwa maana: Ili muifahamu na mzingatie
((بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِين))
((Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi)) [Ash-Shu’araa: 195] [Ibn Kathiyr]
Asiyejua Lugha ya Qur-aan atakuwa ameharamishwa na utamu halisi wa ufahamu wa Qur-aan na Baraka zake. Maswahaba na Salafus Swaalih walikuwa ni wenye asili ya Kiarabu lakini walitilia mkazo kujifunza Lugha ya Kiarabu. ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: “Jifunzeni Kiarabu kwani ni sehemu ya dini yenu” [Iqtidaa’ As-Swiraatw Al-Mustaqiym 2/207].
Ubay bin Ka’b (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema: “Jifunzeni Kiarabu kama mnavyojifunza kuhifadhi Qur-aan” [Ibn Abiy Shaybah Al-Muswannaf Vol. 7 Uk. 150]
Kujifunza Kiarabu ni waajib kwa kila Muislamu, kwani Lugha hii sio Lugha ya Waarabu pekee, bali ni Lugha ya walimwengu wote, kwani Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametumwa kwa walimwengu wote na sio Waarabu pekee:
((وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيراً وَنَذِيراً وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ))
((Na Hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui)) [Sabaa: 27]
Wala haina tabu kujifunza Lugha hii ya Qur-aan ikiwa mtu atatilia juhudi kwani Ameahidi Mwenyewe Mola Mtukufu kwa kusisitiza mara nne katika Surah moja Anaposema:
((وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ))
((Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-aan iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka)) [Al-Qamar: 17, 22, 32, 40]
Nani basi msemaye kweli zaidi ya Mola Muumba? Hapana shaka tunaamini kauli Zake (Subhaanahu wa Ta’ala) na kuwa na yakini nazo.
Kwa hiyo hakutakuwa na hoja kwa mtu kutokuweza kujifunza Lugha hii tukufu ya Qur-aan na Siku ya Qiyaamah tutakaposimamishwa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuulizwa kwa nini tumeitupa Qur-aan au kwa nini hatukuisoma kwa kuipa haki ya kusomwa kwake, kila mmoja wetu itabidi ajibu swali hili na hatakuwa mtu na kisingizio kuwa hakupata njia za kujifunza Lugha hii ili afahamu kauli na maneno ya Mola wake Mtukufu.
Umuhimu Na Faida Ya Kujifunza Qur-aan Neno Kwa Neno
Tukizingatia historia ya Ma’ulamaa, tutaona kuwa Ma’ulamaa wakubwa kabisa waliokusanya mafunzo makuu ambayo Waislamu wanafaidika nayo hadi siku ya Qiyaamah, wengi wao hawakuwa na asili ya Kiarabu. Wachache miongoni mwao ni: Imaam Abu Haniyfah, Imaam Al-Bukhaariy, Imaam Muslim, Imaam An-Nasaaiy, Abu Daawuud, Imaam At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Siybawayhi, Atw-Twabariy, Al-Qurtwubiy, Shaykh Al-Baaniy na wengi wengineo. Bila ya kumsahau mwenyewe aliyeandika vitabu hivyo vitatu vya Madiynah Dr. V. Abdur Rahim. Na hii inasadikisha kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na inadhihirisha wazi wazi kwamba lugha hii haikukusudiwa kwa Waarabu pekee bali kwa makabila yote ulimwenguni.
Wapi Kuanza Kujifunza?
Sehemu mbili kuu za kujifunza Kiarabu;
1-Kujifunza sarufi (grammar),
2- Kujifunza misamiati (vocabulary), ikiwa ni mtu asiyezungumza Lugha ya Kiarabu.
Iliyo bora zaidi ni kuanza kujifunza sarufi kisha mwanafunzi ataweza kujenga misamiati wakati anasoma na baada ya kusoma akaendelea nayo atakaposoma Qur-aan, vitabu, magazeti, hata kusikia watu wakizungumza akiwa anaishi nao au katika televisheni na radio. Na njia iliyo bora kabisa yenye fadhila na nyepesi ni kujifunza kupitia Qur-aan.
Kuanza kwa sarufi ndio bora zaidi, kwa sababu sarufi katika Lugha yoyote ni somo pana na khaswa katika Lugha ya Kiarabu ni zaidi, na pia ndio asasi. Kujifunza sarufi mwanafunzi ataweza kufafanua sentensi kabla ya kufahamu inasema nini kwa kuitazama tu. Huenda hii ikawa ni ajabu kwa wasiozungumza Kiarabu, kwa sababu hivyo sivyo ilivyo hali katika Lugha nyingine. Lakini baada ya kujifunza sarufi, pole pole mwanafunzi ataweza kufahamu kila sentensi kwa undani.
Inasemekana kwamba mwenye kujua Lugha ya Kiarabu hakika ni mwerevu. Kwa nini? Kwa sababu anapozungumza au kuandika sentensi akili yake huwa inatangulia hatua mbili mbele kuwaza aina zote za sarufi zinazohusiana na sentensi katika nomino, kitenzi na herufi. Kadhalika anajua kama inapasa kuwa ni ya umoja (singular), au uwili (dual), uwingi (plural), kike (feminine), ume (masculine), wanaume kwa ujumla (masculine plural), wanawake kwa ujumla (feminine plural), mzungumzaji (1st personal) anayesemeshwa (2nd person) au aliye ghaibu (3rd person) na mengi mengi mengineyo yaliyo na upana wa ajabu katika Lugha hii ya ufasaha wa pekee.
Nyenzo Za Kukusaidia Kujifunza Lugha Ya Qur-aan.
Kinachosikitisha ni kwamba hadi sasa hatuna na nyenzo nyingi na nzuri za kujifunza Kiarabu katika Lugha yetu ya Kiswahili, hivyo hatuna budi kutafuta nyenzo kwa Lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo iliyojaa mafunzo mbali mbali. Na nyingine zimo katika kuandaliwa. Na kila tutakapojaaliwa kuzipata tutakuwa tunaziongezea hapa InshaAllaah. Baadhi ya nyenzo hizi zinapatikana bure, na baadhi yake ni za kuuzwa unaweza kuagiza ukatumiwa kwa posta.
Bonyeza kila kiungo kwa maelezo yake:
VITABU:
Vitabu Vitatu Vya Madiynah Vya Kujifunza Lugha Ya Kiarabu .
Ambavyo ndivyo vinavyotumiwa katika video hizi tulizowaekea humu, utakuwa unafuatilia navyo pamoja na Video zake.
Qur'anic Language Made Easy - Hafiza Iffath Hasan
Kitabu hiki kina mafunzo mepesi kufuatilia. Ni kitabu muhimu kwa kila mwanafunzi khaswa kwa anayeanza kujifunza Lugha ya Kiarabu na aliye dhaifu katika Lugha ya Kiingereza au kwa wanafunzi wachanga. Ni kitabu kitakachofaa khaswa kwa mwenye kujifunza mwenyewe. Mazoezi yake yamepangwa kwa kutumia Qur-aan ambayo itamfanyia mwanafunzi wepesi na moja kwa moja kuanza kujifunza Qur-aan.
Tovuti inayofafanua sarufi ya Kiarabu kwa wepesi kabisa. Inaendeshwa na mwanafunzi aliyehitimu Chuo Kikuu Cha Madiynah.
KAMUSI
Kila mwanafunzi atahitaji kuwa na kamusi itakayomsaidia kutafuta maana ya neno au kupata ufahamu zaidi wa sarufi. Kamusi chache zifuatazo unaweza kununua au kuzipata katika viungo vyake.
Tarjuma Ya Qur-aan Tukufu Neno Kwa Neno Kwa Lugha Ya Kiswahili
Inaendelea kuandaliwa Insha-Allaah.
Al-Mawrid - Munir Baalbaki, Dr. Rohi Baalbaki
The Hans Wehr Dictionary Of Modern Written Arabic
Inasemekana kuwa ni kamusi bora kabisa, na itamsaidia mwanafunzi kujua mzizi wa neno (root word) na minyambuliko mbali mbali ya maneno katika taratibu za kisarufi. Inaanzia neno kwa mzizi wake (root word).
Vocabulary of the Holy Qur'an - Dr. Abdullah Abbas Nadawi,
Kamusi jepesi kufuatilia la misimiati ya Qur-aan, linaloanzia neno kwa mzizi wake (root word) na linatoa maana asasi na kutoka mifano katika Qur-aan.
Easy Dictionary of the Qur'an – Shaykh ‘Abdul Karim Pareck
Kamusi lililoandaliwa kwa ki-Urdu ‘Lughatul-Qur-aan’ (Lugha ya Qur-aan). Kamusi zuri lenye kuashiria katika kujifunza Qur-aan na Lugha ya Kirabu. Pia litamsaidia mwanafunzi hatua kwa hatua kujifunza Qur-aan, likiwa na matini za Kiarabu na tarjuma yake kwa Kiingereza. Hukmu za kisarufi pia zimebainishwa kwa ufupi.
Tanbihi
Tutakuwa tunaendelea kujaza hapa nyenzo nyinginezo kila tutakapojaaliwa kuzipata, lakini tunaamini kwamba haya machache tuliyowakusanyia yanatosha kabisa kwa mwenye kutilia azma kujifunza Lugha hii tukufu ya Qur-aan.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



Jazaakum Llah Khayran kwa
Jazaakum Llah Khayran kwa yote mliotuandalia. Ni changamoto zuri kwa yeyote mwenye kutaka kukifahamu vizuri kitabu hiki kitukufu. Nimeangalia sehemu ya mwanzo tu, mashaAllah ni yenye kueleweka vizuri tu kama kwamba mwalimu unae face to face.
Tunamuomba Allah akuzidishieni nguvu na tawfiyq mzidi kutuandalia zaidi na zaidi na kukuongezeeni katika miyzann zenu njema inshaallah, Amiyn.