Mwanamke Anayetoa Nyusi Ambaye Keshalaaniwa, Ibada Yake Inakubaliwa?

 

Mwanamke Anayetoa Nyusi Ambaye Keshalaaniwa, Ibada Yake Inakubaliwa?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asslam Aleykuom,

 

Namshukuru Allaah Subhanahu wa Ta'aalaa kwa kunipa fursa hii ya kuuliza Masuala yangu. Jee aliyelaaniwa ibada zake zinafaa? Mtowa nyusi na mtolewa wamelaaniwa, Dada yangu ametowa nyusi na anasali Ibada zake vipi?  Jee kama umekufa na nyusi umezitowa upo hasarani?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hakika ni kuwa aliyelaaniwa yuko mahali pabaya sana hapa duniani na Aakhirah. Hasa aliyelaaniwa na Allaah Aliyetukuka na Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi hasara yake ni kubwa sana. Aliyelaaniwa yuko katika maangamivu yasiyo na kifani.

 

 

Miongoni mwa wale waliolaaniwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni wale wenye kutoa nyusi na mwenye kutoa. Sasa mwanzo kabla ya yote ni jukumu na wajibu wako kuweza kumuelimisha dada yako kuhusu katazo hilo la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Huenda ikawa hajui, ikiwa ni hivyo basi atakuwa amesamehewa na Allaah Aliyetukuka kwa kosa hilo. Lakini ikiwa utamwambia naye atajiweka katika kutenda hilo huo utakuwa ni ujeuri na adhabu yake itakuwa kali.

 

 

Unaweza pia kumpatia majibu haya yafuatayo kwenye viungo:

 

Kunyoa Nyusi Ni Kulaaniwa na Allah!

 

Kuzinyoa Nyusi Za Katikati Zilizozidi Sana Na Kuungana

 

 

Hata hivyo, kukata kwake nyusi haimanishi kuwa Ibadah zake hazikubaliwi lakini ibadah hizo zitakuwa zinapungua fadhila na thawabu zake. Na lau hataswali kwa kuwa amelaaniwa kwa kukata nyusi basi madhambi yake yatakuwa makubwa. Hii inafanana na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayosema kuwa mwenye kunywa pombe Swaalah zake za siku arobaini hazikubaliwi lakini anatakiwa aswali, asiposwali madhambi yake yatakuwa makubwa. Kutoswali ni dhambi jengine ambalo ni kubwa sana lenye kumtoa mtu kutoka katika Uislamu. Hivyo, mtu mbali na kuwa Ibadah yake haitokubaliwa kwa sababu ya kosa fulani ni lazima atekeleze Ibadah hiyo ili apate unafuu.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share