Kutumia Dawa Za kuzuia Hedhi Wakati Wa Hija
SWALI
Kuna uhalali gani kwa wanawake kuchelewesha au kusogeza mbele siku zao za hedhi kwa kutumia dawa wakati wa hija? Hii inafanyika ili kutimiza ibada nzima ya hija.
JIBU:
Maulamaa wengi wametoa ruhusa mwanamke kutumia dawa za
kuzuia hedhi ikiwa anakwenda kutimiza nguzo ya Fardhi ya Hajj,
na hoja zao ni
Inafaa kutumia dawa kuzuwia hedhi ili mwanamke aweze
kukamilisha nguzo yake ya tano ya Kiislamu ikiwa atakhofu
kupatwa hedhi wakati yuko katika taratibu za Hajj, kwa sababu
ya kutokana na umbali wa masafa wa kusafiri na gharama
zake nyingi ambazo pengine atashindwa tena kurudia kuitimiza
nguzo yake miaka mingine.
Hapa inafaa tutaje kuhusu wale wanaotaka kutumia dawa hizo kwa kuwawezesha kufunga mwezi mzima wa Ramadhani.
Rai za Ma'ulamaa kuhusu jambo hili zime ikhtilafiana, kuna
wachache waliokubali na wengi wamepinga mwanamke
kutumia dawa hizo katika mwezi wa Ramadhani.
Wale waliokubali wamesema kwamba shuruti za kutumia dawa hizo ni kwamba mwanamke apate ruhusa kwa Daktari kuwa akitumia dawa hizo hazitomfanyia madhara yoyote kwani sheria ya dini yetu haipendi madhara kwa mtu.
لا ضرر ولا ضرار
Hakuna kuleta madhara wala kudhuriana" "
Wale waliopinga kabisa kwa kusema kwamba hii na amri ya
Allaah aliyowaandikia binaadamu, kwa hiyo sio sawa kubadilisha
maumbile ya mwanamke kama alivyoambiwa bibi 'Aysha رضي الله عنها ilipomjia hedhi wakati wa Hajj
((Imetoka kwa Bibi 'Aishah na Jaabir bin 'Abdillah kuwa katika
tarehe nane ya mwezi wa Dhul Hijjah siku ijulikanayo kuwa ni
ya 'Tarwiyah' walipokuwa wakielekea Minaa na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wakaleta talbiya ya Hijja, kisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akaenda kwa Bi 'Aishah r.a. akamkuta analia, akamuuliza: ''una nini?'' akajibu (Bi 'Aishah r.a.) ''Nimepatwa na hedhi na watu
wamehirimia na wamefanya twawaaf nami sijafanya vyote
hivyo! Na sasa watu wanaelekea kuhiji hivi sasa!!''
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamwambia:
فإن ذلك شيء كتبه الله على بنات آدم، فافعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي بالبيت حتى تطهري
"Hili ni jambo aliloliandika Mwenyeezi Mungu kwa wanawake
(mabint Adam), basi nenda kaoge halafu kahirimie kisha Hiji
na fanya yale anayofanya Mwenye kuhiji isipokuwa kutufu
na kuswali". Bi 'Aishah akafanya matendo yote ya Hajj
isipokuwa kufanya Twawaaf na Swalah.))
Vile vile kwa Rahma ya Allaah سبحانه وتعالى Ametusahilishia
dini yetu kwa kuturuhusu kuweza kulipa siku za Ramadhani
ambazo mtu akishindwa kufunga ikiwa yuko safarini au ni mgonjwa na hali
}}فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ
يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ
عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {{
{{Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge.
Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize
hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni
yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize
hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa
amekuongoeni ili mpate kushukuru.}} Al-Baqarah 185
Wallaahu A'alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


